Monday, July 31, 2017

KWANINI UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA

JE WAJUA KUHUSU SIGARA?

HAYA NDIO MADHARA YA UVUTAJI WA SIGARA KATIKA MWILI WA BINADAMU

MADHARA YA UVUTAJI WA SIGARA
Katika moshi wa sigara, zaidi ya kemikali 400
zimegundulika kuwa na madhara makubwa
katika afya. Mvutaji mdogo hutumia nusu ya
pakiti ya sigara kwa siku na kujikuta akiathiri
mwili wake kwa kemikali hizi mara 3500 kwa
mwaka. Hata hivyo,

VITU VITATU HATARI ZAIDI
KATIKA SIGARA NI:
▪1. Tar: hiki ni kisababisha kansa katika mwili.

▪2. Nicotine: Hiki ni kitu chenye sumu ambacho
kwa muda mrefu sana kimetumiwa kama
dawa ya kuuwa wadudu na sumu ya panya.
Inachukua nafasi ya pili kama sumu kali
kabisa kwa athari yake mbaya katika mwili
wa binadamu.

▪3. Carbonmonoxide: Hii ni gesi
inayopatikana katika moshi wa sigara.

MADHARA MBALIMBALI YA  VITU  VINAVYOPATIKANA
KATIKA MOSHI WA SIGARA NI KAMA YAFUATAYO:

🔹1. Kuharibika kwa utando mlaini katika njia za
hewa: katika njia ambayo pumzi hupita kuna
kama tabaka fulani ambalo ni laini
limezunguka katika njia.
Tabaka hili hufanyakazi ya kuzuia vumbi vumbi linaloingia
pamoja na hewa. Ile tabia ya uvutaji hufanya
vile vitu vinavyopatikana katika moshi wa
sigara kuganda katika utando huu na
kusababisha njia kuwa nyembamba kwa kule
kuongezeka kwa takataka na kemikali katika
njia, hivyo kumfanya mvutaji apate shida ya
pumzi hapo baadaye.

🔹2. Vidonda vya tumbo: uvutaji wa sigara
huchochea utengenezaji wa acid ambayo
huweza kumletea mvutaji huyo vidonda vya
tumbo.

🔹3. Matatizo katika mfumo wa upumuaji:
wavutaji hupata shida katika koo na mapafu
hivyo kupata kifua mara kwa mara na
maumivu na mwishowe kupata madhara
makubwa katika mfumo mzima wa upumuaji
kutokana na kuharibika kwa mapafu kama
tutakavyozungumzia katika pointi namba 7
hapo chini. Hali ya hewa huwaathiri sana
wavutaji sigara kwani hupata pneumonia na
asthma.

🔹4. Udhaifu katika mifupa (Osteoporosis):
katika moshi kuna metali ijulikanayo kama
cadmium ambayo inaweza kusababisha
matatizo katika mifupa, hii husababisha
kupoteza asilimia 30 ya calcium katika mifupa.
Kwa wanawake uvutaji wa sigara
umeonekana kuzuia shughuli ya estrogen na
kitu chochote kinachozuia estrogen kufanya
kazi husababisha udhaifu katika mifupa
(Osteoporosis) na hii huweza kusababisha
maumivu ya mara kwa mara katika mifupa.

🔹5. Kuwahi kumaliza kufikia mzunguko wa
mwezi (Menopause): Menopause ni ile hali ya
mwanamke kufikia mwisho wa mzunguko
wake wa kila mwezi ambao humpelekea
kushika ujauzito, hali hii huanza kutokea
akifikia umri wa miaka 45 – 55, hutofautiana.
wanawake wanaovuta sigara hufikia
menopause miaka mitano mapema zaidi ya
wasiovuta.

🔹6. Athari kwa wenye mimba: wanawake
wanaovuta sigara huwa katika hatari kubwa
sana ya mtoto kutoka kabla ya siku zake
(Abortion) au kuua mtoto tumboni. Au hata
mtoto kufa mapema zaidi pindi
atakapozaliwa.

🔹7. Kuharibika kwa Alveoli za mapafu
(Emphysema): ile harufu kali ya moshi
huharibu alveoli ndogo ndogo katika mapafu.
Hii kwa kiasi kikubwa sana hupunguza eneo
ambalo Oxygen hukutana na damu na hivyo
kusababisha hali inayoitwa Emphysema. Hali
hii hujitengeneza taratibu sana na kimya kwa
muda mrefu.
Wavutaji wote wana
Emphysema kwa kiwango fulani Lakini
kutokana na eneo kubwa wanaloishi ambalo
hupatikana Oxygen, watu wengi hawajui
kwamba wana hali hii. (watu wengi wana
takriban alveoli milioni 300 katika mapafu
yao) hivyo ni vigumu kugundua hali hii na
baadhi hujijua pale wanapofanya mazoezi
kwa mfano, na kuhisi ugumu wa pumzi.

🔹8. Upungufu wa uwezo wa kubeba oxygen
katika damu: Carbon Monoxide (CO)
inapatikana katika moshi. Uhusiano wa
Carbon Monoxide kwa Haemoglobin ni
mkubwa mara 200 zaidi ya Oxygen. Hivyo
baadhi ya haemoglobin ya damu huzuiwa na
Carbon Monoxide kwa wavutaji kwani
haemoglobin badala ya kuchukua Oxygen
huenda katika Carbon Monoxide na hivyo
uwezo wa kubeba oxygen katika damu
hupungua.

🔹9. Kansa/ Saratani: Katika asilimia kubwa ya
watu wenye kansa hupatikana kutoka kwa
wavutaji wa sigara, saratani za ngozi, koo,
utumbo, kibofu, mdomo n.k. vilevile saratani
ya figo, kongosho, tumbo na kizazi
imeonekana mara chache kwa wavutaji wa
sigara.

🔹10.Kupungukiwa na vitamin: Uvutaji wa
sigara husababisha upungukiwaji wa Vitamin
hasahasa...

Wakumbushe na wengine ikumbukwe kwamba sio tu anaevuta sigara ila hata yule aliye karbu na mvutaj yuko hatarini kupata haya matatizo

Friday, July 28, 2017

FAIDA 48 ZA JUISI YA TANGAWIZI AMBAZO WENGI HAMZIFAHAMU

FAIDA 48 ZA JUISI YA TANGAWIZI AMBAZO ULIKUWA HUZIJUI

1. Huondoa sumu mwilini haraka sana
2. Huua bakteria wa aina nyingi mwilini hata salmonella ndani ya mwili hata juu ya ngozi
3. Kuna viua vijisumu (antibiotics) vya asili viwili kwenye tangawizi
4. Huondoa uvimbe mwilini
5. Huondoa msongamano mapafuni
6. Tangawizi inayo ‘zingibain’ ambayo huua vimelea mbalimbali vya magonjwa na mayai yake
7. Huondoa maumivu ya koo
8. Huua virusi wa homa
9. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini
10. Huondoa homa hata homa ya baridi (chills)
11. Hutibu saratani ya tezi dume. Tangawizi huua kimeng’enya ambacho ni chakula cha seli za kansa ya tezi dume kiitwacho ‘5-LO enzymes’ na seli hizo za kansa hufa ndani ya masaa mawili au manne bila hicho kimeng’enya.
12. Tangawizi ina kiinilishe muhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho kiitwacho kwa kitaalamu kama ‘gingerol”
13. Hutibu kansa zinazoweza kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu (constipation-r
elated cancer)
14. Ni dawa nzuri kwa kansa ya kwenye damu (leukemia)
15. Ni dawa nzuri dhidi ya kansa ya mapafu (lung cancer)
16. Huzuia kujizalisha kwa bakteria aitwaye ‘Helicobacter pylori’, bakteria huyu ndiye husababisha vidonda vya tumbo mwilini, pia hutibu kiungulia, na kansa mbalimbali za tumbo
17. Ni msaada sana katika kuzuia na kutibu kansa ya titi
18. Hutibu kansa za kwenye kizazi na kansa za kwenye mirija ya uzazi
19. Huongeza msukumo wa damu
20. Husaidia kuzuia shambulio la moyo
21. Huzuia damu kuganda
22. Hushusha kolestro
23. Husafisha damu
24. Husaidia watu wenye kukakamaa kwa mishipa
25. Hutibu shinikizo la juu la damu
26. Husafisha utumbo mpana
27. Hupunguza mishtuko kwenye utumbo mpana na tumbo kuunguruma
28. Huondoa GESI TUMBONI KIRAHISI ZAIDI
29. Husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
30. Dawa nzuri ya kuondoa uchovu
31. Husaidia kuzuia kutapika. Husaidia hata wale wanaosafiri baharini wasipatwe na kichefuchefu
32. Husaidia kuondoa maumivu kutokana na mkao mmoja wa mrefu ama kusimama au kukaa
33. Husaidia uzalishwaji wa juisi vimeng’enya kwa ajili ya kumeng’enya chakula
34. Husaidia kuzuia kuharisha
35. Husaidia mfumo wa upumuaji na kutuliza dalili za pumu
36. Hutibu tatizo la miguu kuwaka moto
37. Hutibu homa ya kichwa
38. Hutibu maumivu ya tumbo wakati wa hedhi
39. Hutibu homa za asubuhi hata kwa mama mjamzito
40. Husaidia kupunguza homa ya baridi yabisi (helps reduce inflammation of arthritis)
41. Huimarisha afya ya figo
42. Husaidia kupunguza uchovu unaotokana na matibabu yaliyopita ya mionzi
43. Ina madini ya potassium ya kutosha
44. Ina madini ya manganese ambayo ni muhimu katika kuuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita
45. Ina kitu kinaitwa ‘silicon’ ambacho chenyewe kazi yake hasa ni kuongeza afya ya ngozi, nywele, meno na kucha
46. Husaidia umeng’enywaji wa madini ya calcium
47. Pia ina vitamini A, C, E, B-complex, chuma, zinki , magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na beta-carotene
48. Hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita

BLEND KAMA UNAVYO TENGENEZA JUICE YA KAWAIDA  KISHA KUNYWA  GLASS MOJA KWA SIKU.

AU UNAWEZA KUJENGA MAZOEA YA KUTAFUNA VIPANDE KADHAA KILA SIKU ASUBUHI KABLA HUJALA KITU.

Tafadhari share kwa ajili ya wengine

Wednesday, July 26, 2017

FAHAMU VYAKULA VINAVYO ONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

VYAKULA VINAVYOONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

PILIPILI
Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho kutoka au kamasi kutoka. Kwenye pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali ambao huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo katika hali ya juu huleta mguso wa hisia za raha.
Pia pilipili husisimua mfumo wa ufahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kumshwa haraka hisia za kimapenzi (kunyegeka) na pia ili ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au kupapaswa uweze kupata hisia kila sehemu.

NAFAKA
Nafaka zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili.
Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu. Na pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo. Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes(zilizokobolewa) ni jambo zuri linalokuhakikisha afya njema na mahusiano mazuri ya ndoa yako

MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI.
Mlo wenye matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Kwanza; matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol), kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu. Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balance ya uzito kwani unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homoni za testosterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika na kuwa na hisia kidogo. Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya kufurahia au kutaka au hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua.

TANGAWIZI
Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume. Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.

ASALI
Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke. Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na hamu ya tendo la ndoa au libido.

KARANGA
Karanga huhusika moja kwa moja na kutunza mfumo wa mzunguko wa damu kuwa na afya (vascular system). Pia mfumo wenye afya (mzunguko wa damu) katika uke na uume huwezesha mwanaume' na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa zuri. Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika uzalishaji wa mbegu za mwanaume.

OYSTERS
Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa wanaume. Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinc huwa na matatizo ya nguvu za kiume na wakati huohuo kuwa na madini mengi ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa.

SOYA
Pamoja na kuwa na kiwango kidogo sana cha fat na pia kuwa na kiwango kizuri cha protein, soya zina phytoestrogens ambayo husaidia sana wanawake ambao wamefikia menopause kutengeneza homoni ya estrogen ya ziada. Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) mwanamke akisisimliwa wakati wa tendo la ndoa.
KUMBUKA: SOYA NI NZURI KWA MWANAMKE TU.

CHOCOLATE
Chocolate ina phenylethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume kufika kileleni (orgasm)

NOTE; kama wewe ni mnene tambua kuwa vyakula vya Wanga na Sukari kwako siyo rafiki kwani husababisha uzito usipungue au kuongezeka kabisa. Chagua vyakula sahihi vyenye Protin, Fat, Mboga zote za Majani na Matunda yasiyo matamu.

Unene ni adui wa tendo la ndoa, ni vyema kuwa na uzito wa kawaida ili kurahisisha hata homoni zako za uzazi kufanya kazi kwa usafiri.

Na endapo wewe siyo mnene basi unaweza kutumia vyakula vyote tulivyotaja katika somo hili, kumbuka kuwa tiba ya vyakula ni tiba ya taratibu hadi kufikia malengo.

Kama kuna makala utataka uandaliwe kuhusu ugonjwa wowote usisite kuacha comment yako chini nasi tutakuandalia au waweza tuandikia katika email na whatsapp hapo chini

Email:ephrakirumba8@gmail.com
Whatsapp:+255717064639

Tuesday, July 25, 2017

EAT TWO BANANAS A DAY AND YOU WILL NOTICE SEVEN CHANGES IN YOURSELF

1.The vitamins and minerals found in bananas keep your body in good condition and the potassium helps to prevent muscle cramps.

2.Your body transforms the amino acid tryptophan into serotonin and releases it in your brain. This so-called happiness hormone helps us to be content and more satisfied.

3.Bananas contain very little sodium and lots of potassium which makes them the perfect food for people with heart conditions.

4.Bananas are rich in iron which your body needs to create red blood cells and hemoglobin. This helps to boost your blood supply.

5.Bananas help to regulate your blood sugar level. They also contain Vitamin B which has a calming effect on your nerves.

6.When its hot out you can cool yourself down by eating a banana. They can even help to reduce your body temperature. If you have fever.

7.Bananas are natural acid reflux Inhibitors. Eating a banana can instantly relieve heartburn.

Friday, July 21, 2017

JINSI YA KUTAMBUA KAMA UZITO WAKO UNAENDANA NA UREFU WAKO

JINSI YA KUTAMBUA KAMA UZITO WAKO UNAENDANA NA UREFU WA MWILI WAKO(BODY MASS INDEX)

By: Ephraim Kirumba
whatsapp 0717064639
Email: ephrakirumba8@gmail.com

Watu wengi tumekuwa tukiishi kwa kutojua miili yetu kama ipo sawa, hii ni kutokana na kile kitendo pengine cha kutougua hutufanya tujisahau kabisa katika kujua undani wa Afya yetu.

Leo napenda tujifunze namna ya kujua jinsi gani utatambua kuwa UZITO WAKO UNAENDANA NA UREFU WA MWILI WAKO(BODY MASS INDEX kwa kifupi BMI)

Kwa kifupi kitendo hiki huhusisha vitu viwili ambavyo ni uzito wako katika kilogram(kg) pamoja na urefu wako katika mita(m). Tutajifunza kwa kutumia mfano.

Uhusiano huo upo katika mpangilio kama ifuatavyo:
BMI ikiwa chini ya 18.50 hapa inakuwa mtu huyu uzito wake upo chini kuliko kawaida(UNDER WEIGHT)

BMI kuanzia 18.50 hadi 24.99 huyu mtu ni mwenye Afya njema na yuko vizuri kabisa(HEALTHY)

BMI kuanzia 25.00 hadi 29.99 huyu ni mtu ambaye amezidi uzito(OVER WEIGHT) hivyo uzito wake na urefu wake haviendani kabisa.

BMI kuanzia 30.00 na kuendelea basi huyu mtu ni yule aliyepitiliza kabisa kiwango cha uzito na anaingia katika kundi la Obesity.

Sasa unapata vipi uhusiano wa uzito na urefu wako(BMI)?

Angalia hapa chini
Kanuni(BMI)=uzito ÷ (urefu)kipeo cha pili
      
Tuangalie mfano mimi Ephraim nikiwa nina uzito wa kg 64 na urefu wa sentimeta 162 ambao ni sawa na mita 1.62

BMI ya Ephraim=64/1.62×1.62
BMI=64/2.6244
BMI=24.386

Kwa mfano huo basi Ephraim yupo kwenye kundi salama japo bado kidogo tu afikie 25 ambapo siyo pazuri.

Sasa tufanye ya kwamba Ephraim ana uzito wa kilo 74 na urefu uleule

BMI= 74/2.6244
BMI=28.196
Hapa anakuwa OVER WEIGHT

Na endapo Ephraim ana uzito wa kg 91;
BMI=91/2.6244
BMI=34.6745
Hapa ni OBESITY!!

Ndugu msomaji wa makala hii nadhani sasa umeshafahamu namna ya kujua kama una uzito unaoendana na urefu wako, hivyo unaweza kujifanyia tathimini wewe mwenyewe.
NOTE: Urefu wako uwe katika kipimo cha mita(metre)

YAFUATAYO NI BAADHI YA MADHARA YA KUWA NA UZITO ULIOZIDI(KUANZIA BMI 25 NA KUENDELEA)
-Magonjwa/matatizo ya Ini na Figo
-Magonjwa ya Kisukari, Shinikizo la damu, Kiharusi na matatizo ya Moyo
-Tatizo la kutopumua vizuri wakati wa usingizi
-Kiwanjo cha juu cha mafuta mabaya(cholesterols)
-Ugonjwa wa mifupa kama yabisi(osteoarthritis)
-Matatizo ya hedhi kwa akinamama na upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume

Unaweza ku-share zaidi makala hii kwa watu wengi kadri uwezavyo ili nao waweze kujifunza kama ulivyojifunza wewe.

Mawasiliano yetu yapo hapo mwanzo kabisa mwa makala hii.

Wednesday, July 19, 2017

ZIJUE TARATIBU ZA ULAJI WA MATUNDA

======*******USHAURI JUU YA ULAJI WA MATUNDA*******======
**************************************************************************************
    Matunda yana faida nyingi mwilini na ni miongoni mwa vyakula vinavyopaswa kupewa kipaumbele katika milo yetu ya kila siku. Lakini kwa bahati mbaya, siyo watu wote wanaelewa umuhimu wa matunda na jinsi ya kula ili kupata faida zake.

    Kutokana na kula matunda kinyume na utaratibu, watu wengi huyachukia matunda baada ya kujikuta wakiumwa tumbo au kujisikia kichefuchefu na kutapika mara baada ya kula. Wengine husikia tumbo kujaa gesi na kusikia kiungulia.
    Halikadhalika, watu wengi wamefundishwa na kuzoeshwa kulishwa matunda baada ya mlo, mazoea ambayo ni kinyume kabisa na kanuni za ulaji sahihi wa matunda. Katika makala haya, utaelewa njia sahihi ya kula matunda ili kupata faida zake.

KULA MATUNDA TUMBO LIKIWA TUPU
===============================
-- Ili kunufaika na matunda, kula matunda wakati ukiwa na njaa na tumbo likiwa tupu. Unapokula matunda katika hali hii, matunda husagika haraka na virutubisho vyake husambaa mwilini kwa urahisi. Baada ya saa moja au zaidi, unaruhusiwa kula mlo wako mwingine kama kawaida.

USILE BAADA YA KULA
===================
-- Imezoeleka na watu wengi kula matunda baada ya mlo kamili. Hata kwenye hafla na tafrija kubwa mbalimbali, utaona matunda huliwa mwishoni baada ya chakula. HII SIYO SAHIHI na hayo ni makosa miongoni mwa makosa mengi yanayofanyika kwa sababu ya mazoea tu.

-- Inaelezwa kuwa ulaji wa matunda baada ya mlo siyo sahihi kwa sababu matunda huyeyuka haraka kuliko chakula cha kawaida. Tunda linapokuwa tayari kupita tumboni kuelekea kwenye utumbo mwembamba, huzuiwa na chakula. Baada ya muda tunda linachanganyika na chakula na kuoza na hatimaye kuzalisha asidi  ambayo humfanya mtu kuumwa tumbo baada ya kula matunda. Lakini pia virutubisho vyake hupotea.

-- Ili kuepukana na hali hiyo ya msongamano kwenye tumbo, kula matunda saa moja kabla au kama utakula baada ya mlo, angalau kula baada ya masaa mawili. Ukila baada ya muda huo, utakuwa umetoa nafasi ya chakula kusagika na bila kuzuia uyayukaji wa matunda.

ZINGATIA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE MATUNDA
===========================================
--> Baadhi ya matunda, kama vile papai, ndizi mbivu, yana kiwango kingi cha sukari, karibu matunda yote yana sukari, lakini mengine huwa na kiwango kingi zaidi. Hivyo inashauriwa kula matunda kwa kiwango cha wastani kila siku bila kuzidisha kiwango cha sukari cha gramu 25 kinachohitajika kwa siku.

--> Aidha, unapokula tunda, hakikisha unakula tunda kwa ukamilifu wake ili kupata virutubisho vyote. Kwa mfano unapokula chungwa, ni vizuri pia ukala pamoja na nyama zake ili kupata virutubisho vyote muhimu vilivyomo.

--> Jiwekee tabia ya kula matunda ya aina mbalimbali kwa nyakati tofauti ili kupata vitamini na madini tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya mwili. Kwa kuwa matunda ndiyo yanayojenga na kuimarisha kinga ya mwili, ulaji wa matunda ya aina mbalimbali kutakuhakikishia mwili wako kinga imara dhidi ya maradhi na kamwe hutasumbuliwa na magonjwa mara kwa mara.

SHARE KM WEWE SIO MCHOYO,WAKUMBUSHE NA WENZIO,,SUBSCRIBE BLOG YETU PIA KUPATA VITU ADIMU KM IVI KILA SIKU

Sunday, July 16, 2017

PID(PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI)

FAHAMU UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI)

PID ni kifupi cha Pelvic Inflammatory Disease ambayo ni maambukizi ya vijududu vya bakteria katika mfumo wa ndani wa uzazi wa mwanamke. Maambukizi yanaweza kuwa katika mji wa uzazi, mirija ya uzazi, ovari au shingo ya uzazi.

PID husababishwa na vijidudu vya bakteria kuingia kwenye mji wa mimba kupitia mlango wa shingo ya uzazi. Vijidudu hivi hutokana na magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa kama kisonono au klamidia. Huingia kwenye mji wa uzazi na kisha kuweza kushambulia ovari,mirija au mji wa mimba wenyewe.

Dalili

P.I.D huleta dalili zifuatazo. Mgonjwa anaweza kupata zote au baadhi ya dalili hizi;

=>Maumivu ya kiuno
=>Kutokwa na uchafu ukeni
=>Maumivu wakati wa kufanya ngono
=>Kutokwa damu baada ya kufanya ngono
=>Maumivu chini ya kitovu baaada ya kufanya ngono
=>Maumivu wakati wa kukojoa
Mara nyingi dalili huwa sio kali na wakati mwingine zinaweza kutokea kwa kipindi cha muda mrefu. Wakati mwingine mwanamke anaweza kupatwa na dalili ghafla na kali hasa maumivu ya tumbo.

Vipimo
Vipimo hivi vinaweza kufanyika kujua kama kuna ugonjwa wa PID.

=>Kipimo cha ultrasound
=>Kipimo cha magonjwa ya zinaa (VDRL)
=>Kuotesha uchafu wa kwenye uke (Cervical/vaginal swab for culture)

Matibabu
Mara nyingi tatizo hili hutibiwa kwa njia ya dawa za antibiotics kwa muda wa siku 14 ni muhimu kuzingatia matumizi na kukamilisha dozi ya dawa ili kuhakikisha umepona kabisa.

Madhara
PID isipotibiwa huleta madhara kwa mgonjwa hasa ikiwa ni hali ya ugumba na hata utasa.

Kujikinga
Kujikinga na PID, ni muhimu kujikinga na magonjwa ya zinaa kwa;

kuwa na mpenzi mmoja uliyepima nae afya na magonjwa ya zinaa.
kutumia kondomu kila mara unapofanya ngono.
kuacha tabia ya kuwa na wapenzi wengi.
Unaposhisi dalili za magonjwa ya zinaa, wahi hospitali kupata matibabu sahihi na hakikisha umepona.

Friday, July 14, 2017

JINSI YA KUREKEBISHA MZUNGUKO WA HEDHI

Jinsi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi

Tatizo la kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi huanza ghafla au polepole ambapo mwanzo mwanamke alikuwa akipata siku zake katika utaratibu unaoeleweka lakini mara haelewi au hajielewi namna mzunguko wake unavyoenda.

Kuvurugika kwa hedhi ni kitendo cha mwanamke kuanza kuona siku zake bila tarehe au mzunguko maalumu na matokeo yake ni kuwa mwanamke atashindwa kutimiza malengo yake kwa kutumia mzunguko huo sababu ni haueleweki.

Unaweza kutokewa ghafla tu unapata hedhi mahali usipotarajia jambo linakufanya ubaki na woga na huelewi nini cha kufanya kwani hukuwa umejiandaa kwa tukio hilo kama matokeo ya siku zako kutokuwa mzunguko maalumu. Wakati mwingine unaweza kupitiliza mwezi hata miezi kadhaa bila kuona kabisa siku zako na hata ukipima ujauzito unakutwa huna ujauzito wala dalili huna.

Madhara ya kuvurugika kwa mzunguko ni pamoja na;  kushindwa kupata ujauzito, maambukizi katika kizazi na kuziba kwa mirija ya uzazi.

Kwanini unahitaji mzunguko wa hedhi ulio sawa?

Faida za kuwa na mzunguko wa hedhi ulio sawa:

Utakusaidia kupata ujaouzito ulioupangilia
Utakuepusha kupata ujauzito ambao hukuupangilia
Utaweza kuamua jinsia ya mtoto unayemtaka
Nini husababisha kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi

Ni rahisi kugundua kama mzunguko wako umevurugika ikiwa tu unauafahamu vizuri mzunguko wako ulio sahihi. Kufahamu mzunguko unahitaji uifahamu siku ambayo ulianza kuona damu hadi siku utakapoona tena katika mzunguko unaofuata. Karibu kila mwanamke huwa na mzunguko wake usiofanana na wa mwingine.

Tatizo linaweza kuanza kwa kurukaruka siku, mwanamke pia anaweza kupoteza siku yaani mwezi mwingine anaona na mwezi mwingine haoni, au anaingia mara mbili kwa mwezi au anaona damu ya hedhi kwa siku nyingi hata zaidi ya siku arobaini mfululizo. Damu yake inaweza kutokea kidogo kidogo kila siku au nyingi huku ikiambatana na mabongemabonge na maumivu pia. Maumivu haya ya wakati wa hedhi huenea chini ya tumbo mpaka miguuni na kiunoni.

Kuvurugika kwa hedhi kunaweza kutokea kutokana na sababu zifuatazo:

Mabadiliko ya mazingira ambayo hupelekea mfumo wa mwili hubadilika pia hasa mwanamke akitoka sehemu ya joto kwenda mikoa ya baridi au toka mikoa ya baridi kwenda mikoa ya joto.

1.Msongo wa mawazo (stress)
2.Hofu
3.Woga
4.Mabadiliko ya kisikolojia
5.Uvimbe kwenye kizazi
6.Matatizo kwenye mfumo wa homoni
7.Matatizo kwenye vifuko vya mayai
8.Mimba kuharibika
9.Maambukizi sugu ya kizazi pia ni mojawapo ya sababu.
Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ya mara kwa mara na kila ukipima unaambiwa ni ugonjwa wa U.T.I kumbe siyo yutiai
Kutokwa na uchafu ukeni
Maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Jinsi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi

Kabla ya yote unapopatwa na tatizo hili kwa muda mrefu ni vizuri ukaonana na daktari uweze kupata uchunguzi wa kutosha kubaini nini hasa inaweza kuwa ndiyo sababu hasa ya tatizo kwa upande wako.

Zifuatazo ni dawa mbadala 6 unazoweza kuzitumia ukiwa nyumbani ili kurekebisha tatizo hili

1. Papai

Papai ni moja ya dawa nzuri sana katika kutibu tatizo la kuvurugika kwa hedhi. Ina viinilishe mhimu kama carotene, chuma ( iron), Kalsiamu (calcium) na vitamini A na C ambavyo husaidia kulainisha na kunywea kirahisi kwa kuta za mji wa uzazi.
Siku 2 au 3 kabla ya kuanza kula papai kila siku nusu papai papai zima kutegemea na ukubwa wake au uwezo wako.

Kwa mtu mwelevu sababu ameshagundua papai laweza kumsaidia hivyo basi atalifanya papai kuwa sehemu ya chakula chake kila siku na si mpaka aumwe tu.

2. Mdalasini

Mdalasini unayo sifa ya kuondoa tatizo la damu kuganda sifa inayoweza kusaidia kuondoa tatizo la maumivu wakati wa hedhi.
Mdalasini ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (fiber), kalsiamu (calcium), chuma (iron) manganizi (manganese).

• Tengeneza chai ya tangawizi kwa kutumia kijiko kidogo cha mdalasini ya unga na maji kikombe kimoja (robo lita), ipua na uache ipowe kidogo, ongeza asali kijiko kikubwa kimoja ndani yake na unywe. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka mara tatu siku 2 au 3 kabla ya kuanza siku zako.

• Au changanya kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na kijiko kidogo kimoja cha asali katika glasi moja ya maji ya uvuguvugu na unywe kutwa mara 2 siku za mwanzoni unapoanza au kukaribia kuingia katika siku zako.

3. Tangawizi

Tangawizi ni dawa ya asili yenye maajabu katika kutibu tatizo la mvurugiko wa hedhi. Tangawizi hufanya kazi mhimu kabisa katika kushusha kiwango cha homoni inayosababisha maumivu ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘prostaglandins’. Tangawizi husaidia pia katika kupigana na uchovu uletwao na mzunguko wa hedhi katika siku zile za mwanzo au siku 2 hivi kabla ya kuanza siku zako na huweza pia kufanya mzunguko usio sawa wa hedhi kuwa sawa

• Tengeneza chai ya tangawizi ukitumia tangawizi mbichi, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 wakati wa siku zako au siku yoyote tu kama kinga. Kamulia ndimu kidogo ndani yake na utumie asali kupata radha badala ya sukari.

• Unaweza pia kuongeza tangawizi kwenye vyakula na mboga mboga nyingi unazopika kila siku.

4. KOTIMIRI (Parsley):

Tengeneza juisi ya kotimiri, viazi pori (Beet Root), karoti au matango. Tumia asali mbichi ukitengeneza juisi hii. Hii kotimiri inapatikana kirahisi Dar na Zanzibar ni mboga mboga inayotumika zaidi kwenye mahoteli ya kitalii. Mboga hii inacho kitu mhimu sana kijulikanacho kama ‘Apiol’ amabcho kazi yake kuu ni kurekebisha na kuweka sawa homoni za kike.

Changanya kwa ujazo sawa yaani kama juisi ya kotimiri ni kikombe kimoja basi ya kiazi pori nayo kikombe kimoja kadharika kwa matango. Juisi hii ni dawa tosha ya maumivu wakati wa siku za hedhi, hurekebisha mzunguko wa hedhi na imethibitika kuwa bora kuliko dawa nyingi za kizungu.

Kunywa glasi moja ya juisi hii kutwa mara 2.

5. MREHANI

Mrehani au Basil kwa Kiingereza ni mmea mwingine mzuri sana katika kuondoa maumivu wakati wa hedhi na kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa ujumla. Mmea huu unatumika sana jikoni kwenye mahotel ya kitalii Dar na Zanzibar. Unao sifa kuu ya kuzuia au kuondoa maumivu mwilini.

• Ongeza kijiko kikubwa kimoja cha majani freshi ya mrehani yaliyokatwakatwa na kisu (chop) kwenye kikombe kimoja cha maji ya moto, funika vizuri na usubiri ipowe. Kunywa yote ikishapoa na ufanye zoezi hili kutwa mara 3 kwa wiki 3 mpaka 4 au mpaka tatizo lako limeisha.

• Au tengeneza juisi ya majani haya. Yatwange kwenye kinu au kwenye blenda ya umee kupata majimaji yake kisha chota vijiko vya chai viwili uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto na unywe yote. Fanya zoezi hili kutwa mara 3.

• Unaweza pia kuongeza majani freshi ya mrehani kwenye vyakula vingi unavyokula kila siku.

6. MAJI YA KUNYWA

Matatizo karibu yote mwilini chanzo chake ni mwili kutokuwa na maji ya kutosha. Maji ni uhai. Unachohitaji hapa ni kutokusubiri kiu. Kiu ni ishara ya mwili iliyochelewa kuhitaji maji.

Matatizo mengi ya kiafya tumeyaona kwa watu wasiopenda kunywa maji ya kutosha kila siku.

Jitahidi hata iweje iwe unaumwa au huumwi chochote unywe maji lita mbili mpaka tatu kila siku iendayo kwa Mungu na utaniletea mrejesho hapa hapa.

Kama una swali au unahitaji ushauri wowote liulize hapo kwenye comment nitakujibu.

Tuesday, July 11, 2017

MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI NA SULUHU ZAKE ILI KUPATA MTOTO

FAHAMU TATIZO LA MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI NA KUZIBA PAMOJA NA SULUHU YAKE ILI KUPATA MTOTO

MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI NI NINI?
Hali ya kujaa maji kwa mirija ya uzazi ya wanawake huitwa hydrosalpinx kwa kitaalamu. Ni tatizo ambalo hujitokeza kwa wanawake kutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa (pelvic inflammatory disease). Mara nyingi husababisha tatizo la ugumba na maumivu ya kiuno.
Mirija ya uzazi hujishikiza kwenye upande wa kulia na kushoto wa tumbo la uzazi, hupitisha mayai kila mwezi kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mji wa uzazi. Urutubishaji wa yai la uzazi hutokea katika mirija hii.

SABABU ZA MIRIJA YA UZAZI KUZIBA

Mara nyingi mirija ya uzazi kuziba hutokana na;
Pelvic inflammatory disease unaotokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa kama kisonono na klamidia.TB ya mirija ya uzaziUpasuaji maeneo ya kiunoni (pelvic surgery)EndometriosisMaambukizi ya apendiksi (appendicitis)Saratani ya mirija ya uzazi

DALILI ZA TATIZO HILI
Wanawake wengi wanaweza wasiwe na dalili zozote, isipokuwa kupata matatizo katika kupata mtoto. Dalili zinazojitokeza mara nyingi huwa ni;
Maumivu ya kiuno
Hujitokeza mara kwa mara hasa siku chache kabla au baada ya kuingia kwenye hedhi.
Uchafu kutoka sehemu za siri

JINSI YA KUGUNDUA TATIZO HILI
Kuna vipimo kadhaa vya kuwezesha kujua kama mirija yako ya uzazi imeziba na kujaa maji:
Hysterosalpingogram
Hii ni aina maalumu ya X-ray ya kiuno, ambayo kimiminika maalumu huingizwa ndani ya mji wa uzazi kwa kupitia shingo ya uzazi. Kama mirija haijaziba, kimiminika huweza kupita mpaka ndani ya kiuno na kama imeziba haitaweza kupita. Hii itaonekana kwenye hiyohysterosalpingogram.
Ultrasound ya kiunoni (Pelvic Ultrasound)
Ultrasound itaweza kuonesha kama mirija yako imeziba na kujaa, na ukubwa wake. Pia itaweza kuonesha kama kuna matatizo mengine kwenye via vya uzazi vya ndani.
Upasuaji wa Tumbo(Laparoscopy)
Upasuaji huu hufanyika kwa kutumia mirija maalumu yenye kamera ili kutazama mirija hiyo. Matundu mawili hutobolewa tumboni ili kupitisha mirija hii.

JE,NAWEZA KUPATA MTOTO ?
Tatizo hili likitibiwa unaweza ukapata mtoto. Pale mirija inapokuwa imeharibika sana uwezekano wa kupata ujauzito huwa ni mdogo sana. Njia nyingine saidizi kama In Vitro Fertilization zinaweza kutumika.

MADAHARA YA TATIZO HILI
Mirija ya uzazi ikiziba, mayai ya uzazi hushindwa kusafiri kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mji wa uzazi. Hivyo tatizo la ugumba hujitokeza.Mimba kutunga nje ya mfuko wa mimba (Ectopic pregnancy)
Maumivu ya kiuno
Vaginal Atrophy (kusinyaa kwa uke na kushindwa kufanya tendo la ndoa)
Kukosa hamu ya tendo la ndoa
Kuwa mkavu Ukeni, na kuhisi maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.

MATIBABU
Matibabu ya kuziba mirija hufanyika kwa njia ya upasuaji ili kuondoa sehemu iliyoziba. Upasuaji kwa njia ya matundu (laparoscopy ) unaweza kufanyika kutibu tatizo hili. Katika upasuaji sehemu zilizoziba au kushikamana huondolewa na zilizo nzima kuunganishwa tena.

Monday, July 10, 2017

FAIDA ZA PARACHICHI NA JUISI YAKE

Tupate Elimu Juu PARACHICHI
Parachichi ni tunda ambalo mti wake hujulikana kisayansi kama Persea amerikana.  Tunda hili lina aminika kuwa na asili kutoka jimbo la Puebla, bara Amerika ya kusini kunako nchi ya Mexico. Ushahidi wa kale kabisa, takribani miaka 10000 BC umeonyesha parachichi lilitumika katika jimbo la Puebla nchini Mexico. Lakini kutokana na faida nyingi kiafya zipatikanazo kwa ulaji wa tunda hili, tunda hili sasa hupatikana na kutumika kwa lishe sehemu nyingi duniani hususani barani Afrika.

Parachichi ni tunda la pekee ukilinganisha na matunda mengine, kimsingi matunda mengine huwa yana wanga(carbohydrate) kwa wingi, wakati parachichi lina aina ya mafuta ambayo yana faida kwa afya.

Parachichi katika tafiti nyingi limeonekana kuwa na faida katika afya ya moyo. Wagonjwa wa moyo wamekuwa katika makatazo ya kutumia aina ya mafuta ambayo yamekuwa yakichangia kuongezeka kwa lehemu katika damu(mafuta hayo kitaalam kama polysaturated fat), na kuongeza matumizi ya mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu (monosaturated fat). Parachichi ni chanzo kizuri cha mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu. Utafiti unaonyesha kuwa matumizi ya mafuta haya  katika parachi hupunguza lehemu iliyo hatari ( kitaalam kama, Low density lipoprotein), na huchangia katika ongezeko la lehemu isiyo hatari( High density lipoprotein).
Madini ya Potasiamu ni aina ambayo huwa watu hawapati ya kutosha kutoka katika vyakula. Parachichi lina kiwango kikubwa cha madini ya potassium kuliko ndizi. Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa matumizi ya madini haya huambatana na kupungua kwa shinikizo la damu, shinikizo la juu la damu laweza kupelekea mtu kupata kiharusi, shambulizi la moyo hata figo kushindwa kufanya kazi.

Parachichi lina kiwango kikubwa cha fiba. Fiba ni kirutubisho kutoka katika vyakula vya jamii ya mimea, fiba huwa hazimeng’enywi tumboni lakini huwa zina umuhimu mkubwa sana, kama kusaidia kupunguza uzito wa mwili, kusaidia urekebishaji wa kiwango cha sukari mwilini na kupunguza hatari ya kupata magonjwa mengi mwilini. Kuna aina fulani ya fiba ambazo huwa ni virutubisho kwa ajili ya bakteria wenye faida tumboni, hii huimarisha kinga ya mwili na kusaidia mwili kufanya kazi katika kiwango kinachotakiwa. Kwa kuwa parachichi lina kiwango kikubwa cha fiba, husaidia kuboresha mmeng’enyo na kupata choo katika hali ya kawaida.

Aina ya mafuta na virutubisho tulivyoviona awali katika parachichi vinasaidia afya ya ngozi yako. Husaidia ngozi yako kutokuwa kavu na kuwa na unyevu unaotakiwa na kuifanya ngozi kuwa laini na yenye afya. Vitamini C husaidia katika kusaidia uponaji haraka wa ngozi na kujijenga upya kwa seli za ngozi zilizoharibika,husaidia kujenga elastini na collageni ambazo ni muhimu katika ngozi. Uwepo wa virutubisho viondoavyo sumu(antioxidants) katika parachichi kama carotenoidi na vitamini E, hutusaidia kutukinga na mionzi mikali ya jua, kwa hiyo huzuia makunyanzi katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuwa na mwonekano mzuri wakati wote.

Tunda hili ni lishe bora kwa wale wenye kisukari. Parachichi lina kiwango kidogo cha sukari ukilinganisha na matunda mengine. Pia uwepo wa mafuta aina ya ‘monosaturated’ husaidia kuboresha ufanyaji kazi wa homoni ya insulini, katika urekebishaji wa kiwango cha sukari mwilini. Faida nyingine ni kuwa Vitamini C  katika parachichi husaidia kuimarisha mishipa ya damu na kuboresha kinga ya mwili ambayo ni faida kubwa kwa wagonjwa wenye kisukari.

Faida katika afya ya uzazi ni dhahiri. Parachichi lina Vitamini E ambayo ni “antioxidant”  Potasiamu, Vitamini B6,Vitamini C ambazo hutusaidia kutukinga na magonjwa ya moyo hata yale ya kisukari. Chochote kile kinachosaidia afya ya moyo pia husaidia afya ya uzazi. Wanaume wenye magonjwa ya moyo na kisukari huwa tatizo kubwa la upungufu wa nguvu za kiume.

Parachichi pia limeonekana kuwa na faida nyingi katika kuboresha afya ya macho, viungo vya mwili na nyinginezo nyingi. Katika utafiti mmoja uko Marekani, ulionyesha kuwa watu walao parachichi walionekana kuwa na afya bora ukilinganisha na wale wasiokula parachichi. Waliokula parachichi hawakupatwa  na matatizo ya mmeng’enyo  ukilinganisha na wale wasiokula. Matatizo ya mmeng’enyo huchangia watu kupatwa na magonjwa ya moyo na kisukari.

Hapo ni kwa mafupi tu, Ila kwa ushauri Tuwe tunapendelea kutumia matunda mara kwa mara ili kuweza kupata faida za kiafya na kuboresha miili yetu dhidi ya matatizo madogo madogo ambayo yakikua yanakua ni makubwa na yasiyokua rahisi kuyakabili.
Ukienda sokoni usisahau parachichi aka Avocado.

Waweza ku subscribe katika blog hii ili uwe wa kwanza kupata makala hizi za afya kwa kuingiza email yako..

Saturday, July 8, 2017

NJIA RAHISI YA KUNG'ARISHA MENO YAKO

NAMNA RAHISI YA KUNG'ARISHA MENO YAKO

Katika somo hili nakuletea mbinu rahisi kabisa ya kung’arisha meno yako na yakaonekana meupe na yenye kupendeza.

Unahitaji vitu viwili, limau na baking soda au wengine huiita bicarbonate of soda nayo ni ile wamama huitumia wanapopika maandazi au mikate, inapatikana maduka ya kawaida hata kwa Mangi hapo nje ipo.

Namna ya kuandaa:

Chukua limau kubwa moja ikate katikati, chuja kupata maji maji yake (juisi) kisha changanya baking soda ya unga kijiko kidogo kimoja cha chai. Changanya vizuri mchanganyiko huo.

Sukutua kinywa chako vizuri ukitumia mswaki na huo mchanganyiko ndiyo iwe dawa yako ya meno. Sukutua (piga mswaki) taratibu kama dakika 3 hadi 5 hivi na mwisho jisafishe kinywa na maji safi.

Mhimu: Fanya zoezi hili nyakati za jioni au usiku unapokaribia kwenda kulala na ufanye mara moja tu kwa wiki na si zaidi ya hapo kwani unaweza kuharibu fizi zako kwa dawa hii usipokuwa makini.

Njia hii pia haisaidii kwa wale ambao wamezaliwa na meno ya rangi hivyo au kama matokeo ya kutumia maji yenye madini kwa muda mrefu kama vile watu wa mikoa ya Arusha au Moshi.

Ukifanya hivi mara 2 au 4 yaani mwezi mmoja utaona tayari meno yako yameanza kuwa meupe na yanayong’aa na kupendeza.

Vyakula kadhaa vifuatavyo vinasaidia kung’arisha meno yako navyo ni pamoja na machungwa, strawberry, mapeazi, maziwa, mtindi, maji ya kunywa, jibini (cheese), broccoli, celery, karoti, tufaa (apple), kitunguu maji, mbegu mbegu (kama korosho, karanga, almonds) nk .

Vyakula au vitu vinavyoharibu rangi ya meno ni pamoja na uvutaji tumbaku au sigara, chokoleti, chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi na vinywaji vingine baridi vyenye caffeine

Thursday, July 6, 2017

JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIKE AU WA KIUME KWA NJIA ZA KIBAILOJIA

MTOTO WA KIUME AU WA KIKE ANATOKEAJE?

Katika urutubishaji yai la mwanamke linabeba chromosome X yani XX
Na mbegu ya mwanaume inabeba chromosome XY
Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na Y kutoka kwa mwanaume mtoto wa kiume hupatikana
Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na X kutoka kwa mwanaume mtoto wa kike hupatikana
FAHAMU SIFA ZA CHROMOSOMES X na Y za mwanaume
Ili uweze kufanikiwa kuchagua mtoto wa kiume au wa kike lazima ujue sifa za chromosomes hizi zinazoamua jinsia ya mtoto
SIFA ZA CHROMOSOMES Y
1.Zina spidi kubwa sana kwahiyo kama yai lipo tayari zenyewe zitawahi kwenda kurutubisha
2.Zina maisha mafupi sana kulinganisha na X
SIFA ZA CHROMOSOMES X
1.Zina spidi ndogo sana
2.Zina maisha marefu kulinganisha na Y
Baada ya kujua sifa za chromosome ambazo ndo zinatusaidia kuamua jinsia twende moja kwa moja kwenye jinsi ya kupata mtoto wa jinsia unayotaka
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUAMUA JINSIA
1.Lazima mwanamke ajue mzunguko wake (menstrual cycle)siku ya 1-28
2.Lazima mzunguko wako uwe na mpangilio sahihi(unaweza ukachunguza mzunguko wako kwa miezi minne mfululizo)
3.PH ya uke lazima iwe kiwango sahihi 4-5.5(Tumia neplily pad kwa kuwa na PH sahihi
4.Ushirikiano kati ya mwanamke na mwanaume

JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIUME
Ili uweze kupata mtoto wa kiume kisayansi unashauriwa kushiriki tendo la ndoa siku ambayo yai litakuwa limetoka kama mzunguko wako uko sahihi ni siku ya 14
Njia nyingine ya kujua yai limetoka baba anaingiza vidole viwili ukeni wakati wa asubuhi na ukikuta uteute ujue yai limetoka kwahiyo jioni mnashiriki tendo la ndoa kwa ajili ya kupata mtoto wa kiume

KWANINI USHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI YAI LIMETOKA ILI KUPATA MTOTO WA KIUME?
Kisayansi chromosome Y ambayo inahusika katika kutunga mimba ya mtoto wa kiume ina spidi kubwa sana ni nyepesi na haiwezi kuishi mda mrefu kwahiyo ukishiriki tendo la ndoa wakati yai limetoka maana ake unaongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume

JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIKE
Ili ufanikiwe kupata mtoto wa kike utatakiwa ushiriki tendo la ndoa siku tatu kabla ya yai kupevuka yani hapa ni baada ya kujua mzunguko
KWANINI USHIRIKI TENDO LA NDOA SIKU TATU KABLA
Hii ni kwasababu chromosome X ambazo ndo zinaunda mtoto wa kike huwa zina sifa ya kuwa na maisha marefu na kutembea taratibu hivyo yai likitolewa litakuta chromosome X ziko hai

KUNA BAADHI YA WAZEE WA ZAMANI WANAAMINI HAYA KATIKA KUPATA MTOTO WA JINSIA UNAYOTAKA
KUPATA WA KIKE
Kula samaki ,mboga za majani,matunda,bidhaa za maziwa,mbegu za matikiti maji na alzeti nk
Wakati wa kufanya tendo la ndoa mwanamke akae juu nk

KUPATA WA KIUME
Kula nyama, ndizi ,Vyakula vya chumvi kama chips ila usizidishe chumvi,karanga na vyakula vingine vya potassium na sodium
Chromosomes Y zinahitaji pH ya alkane kuliko asidi ndio maana wazee waliona hili
Kuna mengi kuhusu wazee wa zamani ila nmeongelea haya ya mlo kwa maana yana mantiki kibaiolojia

MAMBO YANAYOWEZA ATHIRI KUPATA MTOTO UNAYEMTAKA
1.Kushindwa kuhesabu siku( tumia chart niliyokuwekea)
2.Mzunguko mbovu wa hedhi(Tumia neplily pad)
3.KUtokuwa na PH sahihi ukeni tumia Neplily

Tuesday, July 4, 2017

DAWA KUMI ZENYE MADHARA KWA MAMA MJAMZITO

DAWA KUMI AMBAZO MAMA MJAMZITO HATAKIWI KUZITUMIA KABISA:

Leo tutaangalia dawa ambazo jamii yetu hupenda
sana kuzitumia lakini  bahati mbaya baadhi ya
dawa hizo hazitakiwi kupewa kwa wajawazito
kabisa kulingana na madhara makubwa
yanayoambatana na dawa hizo kwa mtoto
aliyepo tumboni.
Zifuatazo ni dawa hizo.

1.Albendazole; hii ni dawa ya minyoo ambayo
hutumika mara kwa mara kujitibu lakini ni dawa
mbaya sana kwa akina mama wajawazito kwani
una uwezo wa kutoa mimba kabisa hivyo
mebendazole hutumika kama mbadala.
2.Gentamycin: hii ni dawa ambayo iko kwenye
mfumo wa sindano tu, mara nyingi hutumika
kutibu magonjwa ya mfumo wa mkojo. Dawa hii
huharibu kabisa mishipa ya fahamu kitaalamu
kama auditory nerve ambayo hutufanya sisi
kusikia. Hivyo matumizi ya dawa hii huweza
kusababisha mtoto kuzaliwa akiwa hasikii yaani
kiziwi.
3.Ciproflaxin; hii ni dawa ambayo hupatikana
kwenye mfumo wa vidonge na sindano, mara
nyingi hutumika kutibu typhoid, UTI au magonjwa
ya njia za mkojo na magonjwa baadhi ya zinaa.
Dawa hii huharibu ukuuji wa mifupa ya mtoto na
huweza kutoa mtoto asiyetembea mwishoni.
4.Doxycline: hii ni dawa ambayo hupatikana kwa
mfumo wa dawa za kumeza kitaaalamu kama
capsules, dawa hizi ni antibiyotiki yaani hutumika
kuua bakteria wa aina tofauti. Bahati mbaya
huweza kuingilia mfumo wa utengenezaji wa
mtoto ikitumika miezi mitatu ya mwanzo na
kusababisha kuzaliwa na mtoto mwenye viungo
pungufu au zaidi.
5.Dawa ya mseto ya malaria au ALU; dawa hii ni
salama kipindi chote cha ujauzito isipokua miezi
mitatu ya kwanza ambapo dawa hii huweza
kuingilia ukuaji wa maumbile ya kwanza ya
mtoto[organogenesis} na kutoa mtoto asiye na
viungo vya kawaida.
6.Metronidazole au fragile; hii dawa ipo kwenye
kikundi cha antibayotiki yaani hushambulia
bakteria. Dawa hii hutumika mara nyingi kuua
minyoo ya amiba na kutibu magonjwa ya mfuko
wa uzazi wa mwanamke na ikitumika miezi
mitatu ya kwanza ya ujauzito huingilia mfumo wa
utengenezaji wa viungo vya mtoto.
7.Mesoprostol: hii ni dawa ambayo iko kwenye
kikundi maarufu cha prostanglandins analogue,
hutumika sana kuongeza njia ya mlango wa uzazi
kipindi cha kujifungua na pia hutumika kutibu
Vidonda ya tumboni hivyo matumizi ya dawa hii
kipindi cha ujauzito yana madhara makubwa mno
ikiwemo kutoa mimba kabisa.
8.Aspirin: hii ni dawa ya maumivu ambayo
humezwa mara kwa mara na hupatikana kirahisi
tu, lakini dawa hii ina uwezo wa kusababisha
kuvuja kwa damu nyingi hasa mama akipata
matatizo flani ya uzazi kama placenta previa. Sio
dawa nzuri sana kipindi cha ujauzito.
9.Praziquantel: hii ni dawa inayotumika kutibu
minyoo flani inayopatikana kwenye sehemu za
maji yaliyotuama, ni hatari sana kwa wamama
wajawazito kwani huiingilia mfumo wa ukuaji wa
mtoto.
10.Furesamide: hii ni dawa ambayo inapatikana
kwenye kikundi cha diuretic.. mara nyingi
hutumika kushusha ongezeko la maji nje ya
mfumo husika wa damu [oedema] na kutibu
presha kubwa ya damu. Sio dawa nzuri kwa
akina mama wajawazito kwani wajawazito hua na
presha ya chini kidogo hivyo huweza kuishusha
chini kabisa[intravascular volume depletion].

Usiache kutembelea kila siku kwenye blog hii kwa makala nyingi na bora za afya... Pia waweza ku subscribe kwa kuingiza email yako hapo chini na utapata makala zetu kwa urahisi zaidi punde tu inapopostiwa....

Sunday, July 2, 2017

SABABU,DALILI NA MADHARA YA SHINIKIZO LA DAMU[PRESSURE]

UGONJWA WA PRESSURE (SHINIKIZO LA DAMU )

Nini maana ya shinikizo la damu?

Ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa uchafu.

Shinikizo la damu hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa Sphygmomanometer

Shinikizo la damu husababishwa na nini?

Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu:

- Uvutaji sigara
- Unene na uzito kupita kiasi
- Unywaji wa pombe
- Upungufu wa madini ya potassium
- Upungufu wa vitamin D
- Umri mkubwa
- Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
- Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin

*Uanishaji wa shinikizo la damu

- Presha ya kawaida <120 <80
- Presha inayoelekea kupanda 120-139 80-89
- Presha hatua ya 1 140-159 90-99
- Presha hatua ya 2 160-179 100-109
- Presha hatua ya 3 ≥180 ≥110

Shinikizo la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi sana duniani na hii ni kutokana na kutokujuwa ni nini hasa husababisha ugonjwa huu mwilini. Shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata masharti.

Katika makala hii tutaona uhusiano mkubwa uliopo kati ya upungufu wa maji mwilini na ugonjwa huu, mwishoni utakuwa umeelewa sasa ni jinsi gani ilivyo rahisi kabisa kujiepusha na kujiponya ugonjwa huu. Endelea kusoma.

Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku likisababisha mshtuko wa moyo (Heart Attacks), kupooza na kiharusi (Strokes).

Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.

Dalili za shinikizo la damu:

- Maumivu ya kichwa (Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi nyakati za asubuhi),
- Kuchanganyikiwa,
- Kizunguzungu,
- Kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni),
- Kutoweza kuona vizuri au
- Matukio ya kuzirai.
- Uchovu/kujisikia kuchokachoka
- Mapigo ya moyo kwenda haraka
- Kutokuweza kuona vizuri
- Damu kutoka puani
Uonapo dalili hizi unapaswa kuwahi hospitali kupata vipimo.

‘Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi, una kiu, usiitibu kiu na madawa – dr. Batmanghelidj’.

Shinikizo la damu (hasa la juu) ni kiashiria cha mwili kupungukiwa maji kwa kiwango kikubwa, ni wakati ambapo mwili unajaribu kujizoesha na upungufu wa jumla wa maji wakati kunapokuwa hakuna maji ya kutosha kuijaza mishipa ya damu yenye kazi ya kusambaza maji kwenye seli mhimu.

Mishipa ya damu imebuniwa maalumu kuendana na mtiririko uliosawa wa ujazo wake wa damu na mahitaji mbalimbali ya tishu kwa kufunga na kufungua mishipa mbalimbali ya damu ndani ya mwili.

Figo hushtuka upesi kulingana na mtiririko wa damu. Hili linaposhindikana, yaani iwapo mtiririko au ujazo wa damu utapungua, basi Figo huitoa homoni iitwayo ‘renini’ ambayo yenyewe huzarisha kitu kiitwacho ‘angiotensini’ ambayo huwa na matokeo mawili; kwanza huzibana ateri na kupandisha shinikizo la damu, pili huisababisha tezi ya ‘adreno’ kutoa homoni iitwayo ‘aldosteroni’ ambayo huzifanya figo kuishikilia chumvi na hivyo kusababisha kupanda kwa shinikizo la damu.

Asilimia 94 ya damu ni maji. Kwa ujumla kila seli ndani ya miili yetu ina bahari ya maji baridi ndani yake na bahari ya maji chumvi nje yake. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa maji ya bahari hizo mbili.

Chumvi inayashikilia na kuyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli (osmotic retention) na potasiamu inayashikilia maji ndani ya seli.

Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji (yaani haunywi maji ya kutosha kila siku) mwili utaongeza ujazo wa maji chumvi kwenye bahari ya nje ya seli.

Kupitia mfumo maalumu, homoni iitwayo ‘vasopressini’ hutolewa ambayo inaweza kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli na kuyachoma maji hayo baridi (baada ya kuwa yamechujwa) ndani katikati ya bahari ya ndani ya seli kama yanavyohitajika ili kuutunza uwiano sawa wa maji ndani na nje ya seli.

Lakini ili mbinu hii ifanikiwe, mbinu gani, mbinu ya kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli, vasopressini husababisha kapilari na mishipa ya damu kujikaza au kupunguza vipenyo vyake na kukupatia wewe shinikizo la juu la damu (BP) ambalo ni mhimu ili kuyachuja na kuyachoma maji baridi ndani ya seli toka katika bahari ya maji chumvi iliyopo nje ya seli.

Kama mishipa ya damu haitapunguza vipenyo vyake, baadhi ya gesi itaachana na damu ili kuziba nafasi zilizowazi kutokana na kupungua kwa umajimaji mwilini na hatimaye kukusababishia msongamano wa Gesi (Gas locks).

Sifa hii ya vipenyo vya mishipa ya damu kujirekebisha kwa ajili ya mzunguko wa damu, ndiyo mtindo unaotumika zaidi katika kanuni za kihaidroliki wakati ambapo mzunguko wa damu mwilini umejirekebisha kuendana na kiasi cha umajimaji kinachopatikana.

Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji kwa mfano kutokana na kutokunywa maji ya kutosha; asilimia 66 ya kuishiwa maji inajionesha kwa kupungua kwa ujazo wa seli, asilimia 26 inapotea toka ujazo wa umajimaji uliopo sehemu ya nje ya seli na asilimia 8 tu inapotea toka katika ujazo wa damu.

Shinikizo la juu la damu ni kiashirio cha mwili kupungukiwa maji kwa asilimia 8 tu, lakini madhara yanajitokeza sababu ya asilimia 66 ya kupunguwa kwa ujazo wa seli.

Maji na chumvi vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida.

Hii ndiyo sababu shinikizo la damu linapaswa kutibiwa kwa kuongeza unywaji wa maji pekee. Dr.Batmanghelidj anasema; Maji peke yake, ni dawa bora ya kukojosha, pekee ya asili tuwezayo kuiendea.

Kama watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu wangeongeza kiasi cha uchukuaji maji, hawatazihitaji dawa za kukojosha, watazarisha mkojo wa kutosha na hivyo kuiondoa chumvi iliyokuwa imezidi!. Watatakiwa pia kuacha kula vyakula visivyo na chumvi na hivyo kuepukana na mikakamao ya mishipa (cramps) kwenye miguu yao.

* Madhara yanayoweza kuletwa na shinikizo la damu:

Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, kutokulielewa shinikizo la damu kama moja ya ishara za mwili kupungukiwa maji na kulitibu kwa dawa za kukojosha ambazo zinaukausha mwili zaidi, baada ya muda zitasababisha;

- Kuzibika kwa ateri za moyo na ateri ziendazo kwenye ubongo
- Shambulio la moyo (heart attack)
- Mishtuko midogo midogo au mikubwa inayopelekea kuzimia
- Ugonjwa wa kibofu cha mkojo
- Kiharusi
- Kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wanaume
- Kuharibiwa kwa ubongo na matatizo ya akili kama vile kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Daktari mwingine, Dr.David Brownstein katika kitabu chake kiitwacho; “Salt Your Way to Live”, anasema kwamba alifundishwa katika vyuo vya kiganga kuwa chumvi husababisha shinikizo la damu na kuwa kila mmoja lazima ale vyakula vyenye chumvi kidogo. Na hili watu wengi wamekuwa wakiamini hivi.

Wakati akiwatibu wagonjwa wake, anasema; alianza kuona kuwa wale wanaotumia vyakula vyenye chumvi kidogo wanapata matokeo ya chini au wanapata nafuu ndogo sana kutoka katika vyakula hivyo vyenye chumvi kidogo au bila chumvi kabisa na wengi wao walitokewa kuwa na uhaba mkubwa wa madini katika miili yao.

Katika utafiti wake ili kuwasaidia wagonjwa wake, ndipo akaja na jibu la chumvi ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ambayo huwa na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake, alianza kuona kitu kigeni kinaanza kutokea. Wagonjwa wake hao wakaanza kuona mashinikizo yao ya damu yanaanza kushuka katika kiwango ambacho wanaweza kuachana kabisa na matumizi ya dawa.

Dr.Batmanghelidj anasema, ikiwa watu watajishughulisha na mazoezi hasa mazoezi ya kutembea kwa miguu, watakunywa maji halisi zaidi na kuongeza chumvi (siyo sodiamu) kidogo ya ziada kwenye vyakula vyao, mashinikizo yao ya damu yatarudi katika hali yake ya kawaida.

Swali la kujiuliza; Ni zaidi ya miongo minne sasa tangu tulipoambiwa kula vyakula vyenye chumvi kidogo ili kuepukana na shinikizo la damu, kwanini sasa Idadi ya watu wanaopatwa na ugonjwa huu inazidi kuongezeka?.

Narudia tena, mwili unapoanza kuishikilia chumvi, hufanya hivyo ili kuhifadhi maji, toka katika bahari chumvi hiyo ya nje ya seli, maji huchujwa na kutumika wakati wa mahitaji ya dharura.

Maji na chumvi kwa pamoja vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida. Kuikimbia chumvi kunasababisha shinikizo la damu (BP) kuwa sehemu ya maisha yetu, tutapata nafuu, lakini baada ya muda mfupi hali hurudi ileile na pengine kuwa watumwa wa kuchagua kula hiki au kile.

Tofauti na zamani ambapo shinikizo la juu la damu lilipokuwa ni ugonjwa wa watu wanene au wenye uzito uliozidi pekee, siku hizi wanene kwa wembamba, watoto kwa wakubwa wanaugua BP.

Featured Post

FAIZA ZA KULA PAPAI

 _*Siri usioijua kuhusu utajiri wa tunda la papai katika kukulinda na magonjwa hatarishi kutokana na faida zake lukuki*_  Hizi ndizo FAIDA 1...