Tuesday, June 27, 2017

UGONJWA WA MOYO [CORONARY HEART DISEASE]

HABARI ZENU WADAU WA MAKALA ZANGU ?

Leo nimeona nikushirikishe kuhusu
UGONJWA WA MOYO ( Coronary heart disease )

MAGONJWA ya MOYO yamezidi sana siku hizi.
Tatizo hili huanza katika MISHIPA ya DAMU ,na huweza kuendelea mpaka kuanza kuziba MISHIPA hiyo.Hii hufuatiwa na MOYO kukosa HEWA safi (Oxygen) kwa kiasi kinachotakiwa kwa sababu MISHIPA ya kupitisha DAMU imeziba na DAMU ndiyo inayopeleka HEWA ya OKSIJENI kwenye MOYO .

TAFITI mbalimbali zinaonyesha UGONJWA wa MOYO huanza kumwandama MTU pale MAMBO fulani yanaposababisha sehemu ya ndani ya KUTA za MISHIPA ya DAMU kuharibiwa.
MAMBO hayo fulani ni pamoja na kuwepo kiwango KIKUBWA cha aina fulani cha  MAFUTA pamoja na LEHEMU katika DAMU.

CHANZO kingine KIKUBWA ni kutozingatia utaratibu BORA wa ULAJI .Hii ni moja ya MAMBO yanayoongeza uwezekano wa MTU kupata MAGONJWA ya MOYO .

Mfano ULAJI wa VYAKULA vyenye MAFUTA mengi, VYAKULA vyenye SUKARI nyingi, CHUMVI nyingi na LEHEMU nyingi.
Wakati huo ULAJI wa MBOGAMBOGA na MATUNDA ukiwa ni wa KIWANGO cha CHINI.
Pia kuwa na UZITO uliozidi nalo ni TATIZO linaloweza kukusababishia UGONJWA wa MOYO.
Pia UVUTAJI wa SIGARA au UTUMIAJI tumbaku.
Kutofanya MAZOEZI kila siku japo nusu saa SHINIKIZO kubwa la DAMU (high blood pressure),UGONJWA wa KISUKARI na kadhalika.

LEHEMU inahitajika MWILINI lakini kwa kiasi KIDOGO .Hata  hivyo huwezi kujua una LEHEMU nyingi kupita kiasi MWILINI mpaka upime (inatakiwa iwe chini ya 200mg/dl).

Kiasi KIKUBWA cha LEHEMU mwilini husababisha mkusanyiko wa MAFUTA katika MISHIPA ya DAMU.

Punguza HATARI hii kwa kupunguza utumiaji wa MAFUTA yanayotokana na WANYAMA ikiwa ni pamoja na NYAMA iliyonona (nyama ya mafuta),MAZIWA yenye MAFUTA mengi (whole milk),JIBINI (cheese),NGOZI ya KUKU na SIAGI .

Pia ni VIZURI kupunguza ULAJI wa MAYAI , NYAMA (isizidi nusu kilo kwa wiki),MAFUTA tumia kwa kiasi kidogo.
Ongeza MATUMIZI ya NAFAKA hasa zile ZISIZONG'ARISHWA ( whole grains ) kama UNGA wa DONA na kadhalika. ONGEZA pia MATUMIZI ya aina za VYAKULA jamii ya kunde,maharage,mbogamboga na matunda.

Fanya MAZOEZI japo dakika 30 kila SIKU .
Epuka MATUMIZI ya POMBE kupita kiasi pamoja na UVUTAJI wa sigara/tumbaku kwani VITU hivi vina MADHARA katika MOYO na MISHIPA ya DAMU .
Epuka HASIRA ,shinikizo la AKILI na SONONA .

KIUJUMLA ,wingi wa LEHEMU unakadiriwa kusababisha VIFO vya WATU takribani MILIONI 2.6 DUNIANI kila MWAKA.

Kuwepo kwa SUKARI nyingi katika DAMU ,husababisha UGONJWA wa KISUKARI ,ambao unamweka MTU katika HATARI ya kupata UGONJWA wa MOYO au KUPOOZA/KIHARUSI (stroke) mara MBILI zaidi ya ASIYE na KISUKARI .

Kumbuka UGONJWA wa MOYO huweza kumpata MTU yeyote bila kujali UMRI ,na katika siku za karibuni mtindo wa MAISHA umewafanya WATU wengi kupata MARADHI haya kutokana na ULAJI holela wa MLO usiozingatia AFYA na kuacha kufanya MAZOEZI .

Featured Post

FAIZA ZA KULA PAPAI

 _*Siri usioijua kuhusu utajiri wa tunda la papai katika kukulinda na magonjwa hatarishi kutokana na faida zake lukuki*_  Hizi ndizo FAIDA 1...