UJUE UGONJWA WA KISUKARI (Diabetes)
Kisukari ni ugonjwa unaotokana na mtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati.
Ugonjwa wa Kisukari hutokea pale ambapo tezi ya kongosho inaposhindwa kutengeneza kichocheo (Homoni) aina ya insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka kwa sukari (Hyperglycemia) au kushuka kwa kiwango cha sukari (Hypoglycemia). Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa na kuwa na kiwango kidogo cha insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili
KISUKARI NI NINI HASWA?
Sukari mwilini hutokana na vyakula pamoja na vinywaji tunavyotumia kila siku na hutumika kuupa mwili nguvu. Glukosi ni aina ya sukari ambayo huzipa chembe za mwili nishati. Hata hivyo ili glukosi iingie ndani ya chembe hizo inahitaji insulini. Insulini ni kemikali (Homoni) ambayo hutokezwa na kongosho (Pancrease).
NINI CHANZO HASA CHA KISUKARI?
Ili kuelewa vyema ugonjwa wa kisukari ni muhimu kwanza kuelewa namna chakula kinavyovunjwa vunjwa na kutumiwa na mwili ili kuzalisha nguvu. Wakati chakula kinapoyeyushwa matukio kadhaa hutokea. Moja ni sukari inayoitwa glucosi ambayo ni chanzo cha nishati/nguvu mwilini huingia katika damu. Tukio la pili ni kiungo kinachoitwa kongosho (Pancrease) kutengeneza kichocheo cha insulini. Kazi ya insulini ni kuondoa glucosi katika damu na kuingiza katika misuli, seli za mafuta na ini, ambako hutumika kama nishati.
Watu wenye kisukari huwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kuliko inavyotakiwa kwa sababu miili yao haiwezi kupeleka sukari kwenye seli za mafuta, ini na misuli ili ihifadhiwe kwa ajili ya kuzalisha nguvu. Hii ni kutokana na moja ya sababu zifuatazo, huenda kongosho zao haziwezi kutengeneza insulini ya kutosha au seli za mwili wao haziathiriwi na insini kama inavyotakiwa au sababu zote hizo mbili.
DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
Kama wewe ni mnene kupita kiasi, hufanyi mazoezi kwa ukawaida au una watu wa ukoo walio na kisukari, huenda tayari una kiwango cha juu cha sukari kwenye damu. Ongezeko la sukari kwenye damu mbali na kuwa kisababishi cha kisukari, hali hiyo inahusianishwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa akili uitwao 'DEMENTIA'.
Kula sukari nyingi sio sababu ya ugonjwa wa kisukari. Lakini lazima tuseme kwamba kula sukari nyingi si nzuri kwa afya yako kwani utaongeza uzito wa kuweza kuathiri uwezo wa mwili wako kujikinga na maradhi tofauti. Ugonjwa wa kisukari umeitwa kwa kufaa "ugonjwa unaoathiri kiini cha nishati ya mwili". Mwili unaposhindwa kutumia glukosi, mifumo mbalimbali ya mwili inaweza kuacha kufanya kazi au hata kusababisha kifo
Ugonjwa wa Kisukari kitaalamu hujulikana kama 'DIABETES MELLITUS'. Jina 'Diabetes Mellitus' linatokana na neno la Kigiriki linalomaanisha 'kunyonya' na neno la Kilatini linalomaanisha 'tamu kama asali'. Maneno hayo yanafafanua vizuri sana ugonjwa huo, kwani maji hupita mwilini mwa mtu aliye na ugonjwa wa kisukari kana kwamba yananyonywa na mdomo na kupitia kwenye njia ya mkojo kisha kutoka nje ya mwili. Isitoshe mkojo huwa na ladha tamu kwa kuwa una sukari.
Nyingine ni ngozi kuwa kavu na kuwasha, mgonjwa kupoteza uzito bila sababu, kuwa na ukungu machoni, kuchoka kusiko kwa kawaida, hisia kupungua katika vidole na viganja
mikononi na miguuni na kuwa na ukungu katika fizi, ngozi na kibofu cha mkojo.
NI NANI ANAWEZA KUWA NA UGONJWA WA KISUKARI?
Watu walio katika makundi yafuatayo wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kisukari:
Wenye uzito uliozidi
Wenye historia ya kuwa na wagonjwa wa kisukari katika familia zao,
Wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi,
Watu wasiojishughirisha au wasiofanya mazoezi,
Wenye shinikizo la damu,
Wenye msongo wa mawazo na
Wenye matumizi makubwa ya pombe na sigara
Watu hawa wanashauriwa kupima sukari yao kila mwaka wakiwa na umri wa miaka 45 na kuendelea.
Kuna hatari kubwa ya kuugua ugonjwa huo ikiwa mtu ana mafuta mengi katika tumbo na kiuno chake kuliko katika mapaja yake. Mafuta katika kongosho na ini huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu.
Wavutaji wa sigara wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi kwani zoea hilo hudhuru moyo na mfumo wa mzunguko wa damu na kubana mishipa ya damu. Kitabu kimoja kinasema kwamba asilimia 95 ya watu wanaougua kisukari ambao hulazimika kukatwa viungo ni wavutaji wa sigara.
DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati
Kwenda haja ndogo mara kwa mara. Watoto kukojoa kitandani
Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.
Kupungua uzito au kukonda licha ya kula vizuri.
Kusikia njaa kila wakati na kula sana.
Wanawake kuwashwa ukeni.
Kutoona vizuri.
Kupungua nguvu za kiume au hamu ya kujamiiana kwa wanawake.
Ganzi, kuchomwachomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole
Miguu kuoza na hata kupata gangrini.
Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ganzi katika miguu.
Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.
Majipu mwilini.
Wenye dalili hizi wanashauriwa kupima sukari ili kubaini kama wana kisukari.
Watu wenye kisukari wanapaswa kubadili jinsi wanavyokula na kuishi.Ufuatao ni ushauri wa kuwasaidia kufanya mabadiliko:
• Anza na mabadiliko madogo madogo. Kwa mfano, badala ya kuacha utumiaji wa vinywaji vilivyokolezwa sukari mara moja, jaribu kupunguza matumizi ya vinywaji hivyo taratibu. Kupunguza taratibu kiasi cha sukari unayokula au kuongeza kiasi cha mazoezi ni rahisi kutekeleza na kuna uwezekano mkubwa utazoea na kuendelea na utaratibu huo.
• Amua mwenyewe unataka kubadili nini. Weka lengo kama vile kutembea zaidi, kupunguza uvutaji au kutovuta kabisa, au kuweza kucheza na wajukuu zako.
• Tafuta msaada. Familia, marafiki, au watu wengine wenye kisukari wanaweza kukusaidia kufanya mabadiliko.
• Tafuta msaada kwa matatizo ya kisaikolojia. Ni jambo la kawaida kwa watu wenye kisukari kuogopa maisha ya baadaye, kuhuzunika juu ya kuugua mara kwa mara, au kuwa na hasira juu ya mabadiliko yanayohitajika. Hisia za uchungu, huzuni, au kukosa matumaini vinaweza kumzuia mtu mwenye kisukari kufanya mabadiliko ambayo yanahitajika au ambayo anataka kufanya.
• Tafuta sababu zako za kutaka kuwa na afya bora zaidi. Unataka kufanya nini na unataka kujisikia vizuri namna gani? Kwa mfano, fikiria familia yako na kwa nini unataka kuendelea kuishi ukiwa mwenye afya ya kukuwezesha kuwasaidia wanafamilia kwa muda mrefu zaidi.
• Ugonjwa wa kisukari ni tatizo ambalo siku hizi husababishwa na mfumo wa maisha tunayoishi hasa vijana, tafiti zilizowahi kufanywa zinaonesha kuwa vijana wapo kwenye hatari kubwa ya kupata kisukari kwa sababu ya mfumo usio sahihi wa maisha wanayoishi vijana.
• Kutokufanya mazoezi, kukosa muda wa kupumzika na kutokula mlo sahihi,unywaji wa pombe na uvutaji sigara wa kupitiliza, hizi ni sababu chache zinazochangia vijana kuishi katika mfumo wa maisha hatarishi wa kupata maradhi ya kisukari.
Baadhi ya dawa za mitishamba zinaweza kusaidia kucontrol sukari mwilini
Waulize wataalam wa tiba za asili dawa gani za mitishamba zinapatikana katika eneo lako kwa ajili ya kupunguza sukari kwenye damu na kuwa kawaida, njia bora zaidi za kuzitumia, na kama ni salama kuzitumia sambamba na insulini na dawa zingine.
Duniani kote, wataalam wa tiba za asili wamegundua vyakula na dawa za mitishamba ambazo zinaweza kusaidia kupunguza sukari kwenye damu. Ifuatayo ni mifano kadhaa:
• Bitter melon , Mdalasin, Binzari ya manjano, Majani ya mlonge, Uwatu (Fenugreek), Forosadi (Mulberry) , Tangawizi , Nopal (cactus, Bitter leaf , Siki
SHARE UJUMBE HUU KWA NDGU NA MARAFIKI KWA MSAADA WA ELIMU JUU YA UGONJWA HUU