Powered By Blogger

Tuesday, July 11, 2017

MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI NA SULUHU ZAKE ILI KUPATA MTOTO

FAHAMU TATIZO LA MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI NA KUZIBA PAMOJA NA SULUHU YAKE ILI KUPATA MTOTO

MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI NI NINI?
Hali ya kujaa maji kwa mirija ya uzazi ya wanawake huitwa hydrosalpinx kwa kitaalamu. Ni tatizo ambalo hujitokeza kwa wanawake kutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa (pelvic inflammatory disease). Mara nyingi husababisha tatizo la ugumba na maumivu ya kiuno.
Mirija ya uzazi hujishikiza kwenye upande wa kulia na kushoto wa tumbo la uzazi, hupitisha mayai kila mwezi kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mji wa uzazi. Urutubishaji wa yai la uzazi hutokea katika mirija hii.

SABABU ZA MIRIJA YA UZAZI KUZIBA

Mara nyingi mirija ya uzazi kuziba hutokana na;
Pelvic inflammatory disease unaotokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa kama kisonono na klamidia.TB ya mirija ya uzaziUpasuaji maeneo ya kiunoni (pelvic surgery)EndometriosisMaambukizi ya apendiksi (appendicitis)Saratani ya mirija ya uzazi

DALILI ZA TATIZO HILI
Wanawake wengi wanaweza wasiwe na dalili zozote, isipokuwa kupata matatizo katika kupata mtoto. Dalili zinazojitokeza mara nyingi huwa ni;
Maumivu ya kiuno
Hujitokeza mara kwa mara hasa siku chache kabla au baada ya kuingia kwenye hedhi.
Uchafu kutoka sehemu za siri

JINSI YA KUGUNDUA TATIZO HILI
Kuna vipimo kadhaa vya kuwezesha kujua kama mirija yako ya uzazi imeziba na kujaa maji:
Hysterosalpingogram
Hii ni aina maalumu ya X-ray ya kiuno, ambayo kimiminika maalumu huingizwa ndani ya mji wa uzazi kwa kupitia shingo ya uzazi. Kama mirija haijaziba, kimiminika huweza kupita mpaka ndani ya kiuno na kama imeziba haitaweza kupita. Hii itaonekana kwenye hiyohysterosalpingogram.
Ultrasound ya kiunoni (Pelvic Ultrasound)
Ultrasound itaweza kuonesha kama mirija yako imeziba na kujaa, na ukubwa wake. Pia itaweza kuonesha kama kuna matatizo mengine kwenye via vya uzazi vya ndani.
Upasuaji wa Tumbo(Laparoscopy)
Upasuaji huu hufanyika kwa kutumia mirija maalumu yenye kamera ili kutazama mirija hiyo. Matundu mawili hutobolewa tumboni ili kupitisha mirija hii.

JE,NAWEZA KUPATA MTOTO ?
Tatizo hili likitibiwa unaweza ukapata mtoto. Pale mirija inapokuwa imeharibika sana uwezekano wa kupata ujauzito huwa ni mdogo sana. Njia nyingine saidizi kama In Vitro Fertilization zinaweza kutumika.

MADAHARA YA TATIZO HILI
Mirija ya uzazi ikiziba, mayai ya uzazi hushindwa kusafiri kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mji wa uzazi. Hivyo tatizo la ugumba hujitokeza.Mimba kutunga nje ya mfuko wa mimba (Ectopic pregnancy)
Maumivu ya kiuno
Vaginal Atrophy (kusinyaa kwa uke na kushindwa kufanya tendo la ndoa)
Kukosa hamu ya tendo la ndoa
Kuwa mkavu Ukeni, na kuhisi maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.

MATIBABU
Matibabu ya kuziba mirija hufanyika kwa njia ya upasuaji ili kuondoa sehemu iliyoziba. Upasuaji kwa njia ya matundu (laparoscopy ) unaweza kufanyika kutibu tatizo hili. Katika upasuaji sehemu zilizoziba au kushikamana huondolewa na zilizo nzima kuunganishwa tena.

No comments:

Post a Comment

FEATURED POSTS

AFYA TIPS