Thursday, June 15, 2017

VIDONDA VYA TUMBO NA SABABU ZAKE

HABARI ZENU WADAU WA MAKALA ZANGU..?

LEO NIMEONA NIZUNGUMZIE VIDONDA VYA TUMBO NA SABABU ZAKE.

UGONJWA wa VIDONDA vya TUMBO hutokea iwapo KIDONDA cha UKUBWA wa angalau NUSU sentimita kitatokea kwenye sehemu yeyote ya UKUTA wa TUMBO au UTUMBO wa BINADAMU.

Kwa kawaida TATIZO hili huleta MAUMIVU MAKALI sana ya TUMBO ingawa si lazima kila MAUMIVU ayapatayo MGONJWA husababishwa na VIDONDA vya TUMBO .

Tafiti zimeonesha kwamba karibu ASILIMIA 70% mpaka ASILIMIA 90% ya VIDONDA vya TUMBO husababishwa na aina ya VIMELEA vya BAKTERIA wajulikanao kama Helicobacter pylori.

Aidha MATUMIZI ya baadhi ya DAWA za kutuliza MAUMIVU za JAMII ya Non Steroid Anti-inflamatory Drugs(NSAIDs), kama Aspirin au Diclofenac HUWEZA kusababisha au KUONGEZA uwezekano wa kupata UGONJWA huu.

Kuna DHANA iliyozoeleka kuwa VIDONDA vya TUMBO huathiri zaidi MFUKO wa kuhifadhia CHAKULA yaani TUMBO (stomach). DHANA hii SI KWELI kwani sehemu INAYOATHIRIWA ZAIDI na TATIZO hili ni SEHEMU ya KWANZA ya UTUMBO MDOGO ijulikanayo kama DUODENUM .

Kuna MAKUNDI MAKUU yafuatayo ya UGONJWA huu:-

1.VIDONDA vinavyotokea kwenye MFUKO wa kuhifadhia CHAKULA yaani TUMBO (Gastric ulcers)

2. VIDONDA vinavyotokea kwenye SEHEMU ya KWANZA ya UTUMBO MDOGO (Duodenal Ulcers)

3. VIDONDA vinavyotokea kwenye KOO (Oesophageal ulcers)

4. VIDONDA vijulikanavyo kama Merckel’sDiverticulum ulcers.

VISABABISHI:-

VIDONDA vya TUMBO husababishwa na MAAMBUKIZI ya BAKTERIA aina ya Helicobacter pylori.

Imeonekana kuwa zaidi ya ASILIMIA 50% ya WATU duniani wana VIMELEA hivi katika UTUMBO .

Aidha, MIONGONI mwao, karibu ASILIMIA 80% huwa hawaoneshi DALILI yeyote ya KUUGUA UGONJWA huu.

AINA hii ya VIMELEA vya BACTERIA husababisha karibu ASILIMIA 60% ya VIDONDA vinavyotokea kwenye TUMBO (gastric ulcers) na zaidi ya ASILIMIA 90% ya duodenal ulcers.

HALI hii husababishwa ZAIDI na KUSHINDWA kwa MFUMO wa KINGA MWILINI KUWAUA na KUWAONDOA kabisa VIMELEA hawa NDANI ya MWILI .

MATOKEO ya kushindwa huku HUSABABISHA kuwepo UAMBUKIZI wa KUDUMU katika KUTA za TUMBO (chronic active gastritis), UAMBUKIZI ambao huharibu MFUMO na UWEZO wa KUTA za TUMBO kutunza HOMONI ya GASTRIN, ambayo ni MUHIMU katika kuhakikisha MAZINGIRA ya TUMBO yanakuwa na KIWANGO salama cha TINDIKALI.

Kwa KAWAIDA, KAZI ya GASTRIN ni KUCHOCHEA utolewaji wa TINDIKALI (gastric acid) kutoka kwenye SELI za UKUTA wa TUMBO zijulikanazo kama Parietal cells.

Iwapo BACTERIA hawa WATASHAMBULIA na kuharibu UKUTA wa TUMBO , MFUMO wa GASTRIN pia UHARIBIKA, na hivyo kusababisha GASTRIN kuzalishwa kwa WINGI hali ambayo pia huchochea UZALISHAJI wa GASTRIC ACID kwa WINGI.

MATOKEO ya KUZALISHWA kwa WINGI kwa TINDIKALI hii hupelekea KUCHUBUKA kwa UKUTA wa TUMBO na hivyo kusababisha VIDONDA vya TUMBO .

MATUMIZI ya MUDA MREFU ya DAWA za kuondoa MAUMIVU za kundi la NSAIDs:-

UKUTA wa UTUMBO hujilinda na MADHARA yatokanayo na TINDIKALI ya UTUMBO (gastric acid) kwa kuwa na UTANDO LAINI (mucus) ambao hutolewa na VICHOCHEO vijulikavyo kama Prostaglandins.

DAWA hizi za KUNDI la NSAIDs huharibu MFUMO wa kutengeza VICHOCHEO hivi yaani prostaglandins na hivyo kufanya KUTA za TUMBO kukosa UTANDO wa KUZILINDA na MASHAMBULIZI ya TINDIKALI hali ambayo hupelekea KUTOKEA kwa VIDONDA vya TUMBO.

UVUTAJI wa SIGARA :-

Uvutaji SIGARA sambamba na MAAMBUKIZI ya BAKTERIA aina ya Helicobacter pylori huongeza MADHARA ya UGONJWA wa VIDONDA vya TUMBO.Ifahamike tu kuwa UVUTAJI SIGARA pekee hausababishi VIDONDA vya TUMBO.

VYAKULA au VIUNGO vya CHAKULA vyenye UCHACHU :-

KINYUME na DHANA iliyozoeleka miongoni mwa WATU wengi, baadhi ya VYAKULA vyenye UCHACHU na UPILIPILI kama vile PILIPILI, NDIMU, LIMAO na MASALA, HAVINA UHUSIANO na UWEZEKANO wa kupata VIDONDA vya TUMBO .

WATU walio katika KUNDI la DAMU la O :-

IMEONEKANA pia kwamba KUNDI la DAMU lijulikanalo kama BLOOD GROUP O, HALINA uhusiano wa kusababisha VIDONDA vya TUMBO.

UNYWAJI wa POMBE :-

UNYWAJI wa POMBE pekee hausababishi VIDONDA vya TUMBO. Hata hivyo, UNYWAJI wa POMBE sambamba na MAAMBUKIZI ya VIMELEA vya Helicobacter pylori huongeza MADHARA ya UGONJWA wa VIDONDA vya TUMBO.

VITU vingine:-

VITU vinavyohusishwa na UONGEZAJI wa MADHARA ya VIDONDA vya TUMBO ni pamoja na UPASUAJI wa TUMBO (major abdominal surgeries), KUUNGUA kwa MOTO (burns), UGONJWA wa FIGO ,na KUBADILISHWA kwa VIUNGO vya MWILI kama FIGO au INI .

DALILI au VIASHIRIA vya VIDONDA VYA TUMBO:-

# MAUMIVU MAKALI au KIUNGULIA maeneo ya CHEMBE MOYO (epigastic pains).

# MAUMIVU juu KIDOGO ya TUMBO mara nyingi HUENDANA na MUDA wa KULA CHAKULA . MTU mwenye VIDONDA kwenye TUMBO (gastric ulcers) hupata MAUMIVU MAKALI sana kipindi ANAPOKULA au mara tu BAADA ya KUMALIZA KULA wakati aliye na VIDONDA kwenye SEHEMU ya kwanza ya UTUMBO MDOGO (duodenal ulcers) hupata MAUMIVU MAKALI anapokuwa na NJAA na hupata NAFUU pindi ANAPOKULA .

(i) KUVIMBIWA au TUMBO kujaa GESI. HALI hii pia yaweza KUENDANA na KUBEUA au KUJAMBA mara kwa mara.

(ii) KUCHEUA na KUONGEZEKA kwa MATE yanayoshuka TUMBONI baada ya KUCHEUA .

(iii) KICHEFUCHEFU na KUTAPIKA

(iii) Kupoteza HAMU ya KULA na KUPUNGUA UZITO

(iv) Kutapika DAMU

(v) Kupata HAJA KUBWA cha RANGI NYEUSI au KAHAWIA chenye HARUFU MBAYA SANA.

HII humaanisha MGONJWA anapata HAJA KUBWA au CHOO kilichochanganyika na DAMU kwa mbali

UWEPI wa DALILI kama KIUNGULIA cha MUDA MREFU, KUCHEUA na KUTAPIKA baada ya KULA na HISTORIA ya KUTUMIA DAWA za KUPUNGUZA MAUMIVU (NSAIDs) kwa MUDA MREFU bila KUFUATA ushauri wa DAKTARI ni ISHARA tosha ya kumfanya MGONJWA kumuona DAKTARI kumpima na kumfanyia UCHUNGUZI ili KUJIRIDHISHA kuwa HANA TATIZO la VIDONDA vya TUMBO .

KAMA UNAZO DALILI HIZO USISITE KUFIKA HOSPITALI [KITUO CHA AFYA] KILICHO KARIBU NAWE KWA MSAADA ZAIDI

FAIDA ZA KUNYWA MAJI ASUBUHI(KABLA YA KIFUNGUA KINYWA)

KUNYWA MAJI KABLA YA KIFUNGUA KINYWA ASUBUHI -YANATIBU MARADHI MENGI.

Kiafya binadamu utunatakiwa kunywa glasi 7-8 kwa siku ni muhimu kwa afya zetu.Watu wengi hawajui kama kunywa maji asubuhi pale uamkapo ni kinga moja kubwa mwilini.image.Tiba hii huu inaitwa Ayurvedic treatment inafaida nyingi ya kukuepusha na maradhi.

sehemu kubwa ya mwili wa mwanadamu ni  maji  kwa asilimia 70% ambayo ndio inasaidia mwili Wake ufanye kazi kiufasaha,wakati cell ya ubongo wa binadamu una maji kwa asilimia 85%,damu inakiasi cha maji kwa asilimia 82%,muscles inatumia maji asilimia 75% wakati mifupa inamaji asilimia 25%.Mpaka hapo inaonyesha maji ni muhimu sana kwa mwili wa binadamu .

Umuhimu wa kunywa maji asubuhi kabla ujaingiza chochote tumboni.

Unatakiwa kunywa maji pale uamkapo ukiwa ujakula chochote,itakusaidia kusafisha mfumo wako wa mmeng’enyo (internal system) kwa urahisi. Itatoa uchafu  na sumu kwenye Colon ulizozila kupitia  vyakula tofauti tofauti .Faida nyinginezo ni

Kungarisha ngozi.

Renew cells.

Kusafishwa kwa colon na kufanya unyonywaji wa virutubisho kuwa rahisi.

Inatibu magongwa na maradhi .Unywaji wa maji asubuhi pale uamkapo inakusaidia kutibu maradhi kama matatizo ya ini,TB,kuhara,cancer,matatizo ya macho,maumivu ya kichwa,stress,uti wa mgongo.

Hupunguza uzito.

Kunywa maji pale uamkapo liters 1.5 ( glas 5-6),epuka kunywa kinywaji kingine chochote au kula kabla na baaya ya kunywa maji ,usinywe pombe baada ya siku 2 ndio uendelee na kunywa maji yako kila asubuhi .Mwanzo itakuwa ngumu sana kunywa glas 6 kwa pamoja unachotakiwa kunywa 4 pumzika kidogo kunywa izo 2 zilizobakia.Utafanya hivyo baada ya siku 3 utumbo utaozoea na utakunywa kwa urahisi.

Hii water therapy ilizinduliwa na wajapan baada ya kuifanyia utafiti wa mda mrefu na kubaini inatibu maradhi  mengi iwapo mgonjwa atafatisha sheria zake kama

Uamkapo kunywa maji moja kwa moja bila kupiga mswaki au kula chochote.

Piga mswaki na usile chochote sababu yale maji yanahitaji kutoa uchafu kabla ujaweka chakula au  kinywa tumboni.

Bada ya dakika 45 unaweza kunywa breakfast.

Baada ya breakfast usile kitu chochote baada ya masaa 2.

       Kipimo cha maji kulingana na maradhi.

Constipation-wenye matatizo ya kuapa haya kubwa watafata hii kinga ya maji  kwa siku 10

TB-siku 90

Kisukari siku 30

Gastric -kuwa na gesi nyingi tumboni -siku 10

Pressure (high blood pressure) siku 30.

Unatakiwa kunywa maji kwa wingi haswa wale wanaoishi sehemu za joto .Epuka kuwa dehydrated kwani utakaribisha maradhi kwa urahisi...Endelea kuwa nami kwa makala nyingi za afya

Featured Post

FAIZA ZA KULA PAPAI

 _*Siri usioijua kuhusu utajiri wa tunda la papai katika kukulinda na magonjwa hatarishi kutokana na faida zake lukuki*_  Hizi ndizo FAIDA 1...