Powered By Blogger

Friday, July 21, 2017

JINSI YA KUTAMBUA KAMA UZITO WAKO UNAENDANA NA UREFU WAKO

JINSI YA KUTAMBUA KAMA UZITO WAKO UNAENDANA NA UREFU WA MWILI WAKO(BODY MASS INDEX)

By: Ephraim Kirumba
whatsapp 0717064639
Email: ephrakirumba8@gmail.com

Watu wengi tumekuwa tukiishi kwa kutojua miili yetu kama ipo sawa, hii ni kutokana na kile kitendo pengine cha kutougua hutufanya tujisahau kabisa katika kujua undani wa Afya yetu.

Leo napenda tujifunze namna ya kujua jinsi gani utatambua kuwa UZITO WAKO UNAENDANA NA UREFU WA MWILI WAKO(BODY MASS INDEX kwa kifupi BMI)

Kwa kifupi kitendo hiki huhusisha vitu viwili ambavyo ni uzito wako katika kilogram(kg) pamoja na urefu wako katika mita(m). Tutajifunza kwa kutumia mfano.

Uhusiano huo upo katika mpangilio kama ifuatavyo:
BMI ikiwa chini ya 18.50 hapa inakuwa mtu huyu uzito wake upo chini kuliko kawaida(UNDER WEIGHT)

BMI kuanzia 18.50 hadi 24.99 huyu mtu ni mwenye Afya njema na yuko vizuri kabisa(HEALTHY)

BMI kuanzia 25.00 hadi 29.99 huyu ni mtu ambaye amezidi uzito(OVER WEIGHT) hivyo uzito wake na urefu wake haviendani kabisa.

BMI kuanzia 30.00 na kuendelea basi huyu mtu ni yule aliyepitiliza kabisa kiwango cha uzito na anaingia katika kundi la Obesity.

Sasa unapata vipi uhusiano wa uzito na urefu wako(BMI)?

Angalia hapa chini
Kanuni(BMI)=uzito ÷ (urefu)kipeo cha pili
      
Tuangalie mfano mimi Ephraim nikiwa nina uzito wa kg 64 na urefu wa sentimeta 162 ambao ni sawa na mita 1.62

BMI ya Ephraim=64/1.62×1.62
BMI=64/2.6244
BMI=24.386

Kwa mfano huo basi Ephraim yupo kwenye kundi salama japo bado kidogo tu afikie 25 ambapo siyo pazuri.

Sasa tufanye ya kwamba Ephraim ana uzito wa kilo 74 na urefu uleule

BMI= 74/2.6244
BMI=28.196
Hapa anakuwa OVER WEIGHT

Na endapo Ephraim ana uzito wa kg 91;
BMI=91/2.6244
BMI=34.6745
Hapa ni OBESITY!!

Ndugu msomaji wa makala hii nadhani sasa umeshafahamu namna ya kujua kama una uzito unaoendana na urefu wako, hivyo unaweza kujifanyia tathimini wewe mwenyewe.
NOTE: Urefu wako uwe katika kipimo cha mita(metre)

YAFUATAYO NI BAADHI YA MADHARA YA KUWA NA UZITO ULIOZIDI(KUANZIA BMI 25 NA KUENDELEA)
-Magonjwa/matatizo ya Ini na Figo
-Magonjwa ya Kisukari, Shinikizo la damu, Kiharusi na matatizo ya Moyo
-Tatizo la kutopumua vizuri wakati wa usingizi
-Kiwanjo cha juu cha mafuta mabaya(cholesterols)
-Ugonjwa wa mifupa kama yabisi(osteoarthritis)
-Matatizo ya hedhi kwa akinamama na upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume

Unaweza ku-share zaidi makala hii kwa watu wengi kadri uwezavyo ili nao waweze kujifunza kama ulivyojifunza wewe.

Mawasiliano yetu yapo hapo mwanzo kabisa mwa makala hii.

No comments:

Post a Comment

FEATURED POSTS

AFYA TIPS