Powered By Blogger

Tuesday, July 4, 2017

DAWA KUMI ZENYE MADHARA KWA MAMA MJAMZITO

DAWA KUMI AMBAZO MAMA MJAMZITO HATAKIWI KUZITUMIA KABISA:

Leo tutaangalia dawa ambazo jamii yetu hupenda
sana kuzitumia lakini  bahati mbaya baadhi ya
dawa hizo hazitakiwi kupewa kwa wajawazito
kabisa kulingana na madhara makubwa
yanayoambatana na dawa hizo kwa mtoto
aliyepo tumboni.
Zifuatazo ni dawa hizo.

1.Albendazole; hii ni dawa ya minyoo ambayo
hutumika mara kwa mara kujitibu lakini ni dawa
mbaya sana kwa akina mama wajawazito kwani
una uwezo wa kutoa mimba kabisa hivyo
mebendazole hutumika kama mbadala.
2.Gentamycin: hii ni dawa ambayo iko kwenye
mfumo wa sindano tu, mara nyingi hutumika
kutibu magonjwa ya mfumo wa mkojo. Dawa hii
huharibu kabisa mishipa ya fahamu kitaalamu
kama auditory nerve ambayo hutufanya sisi
kusikia. Hivyo matumizi ya dawa hii huweza
kusababisha mtoto kuzaliwa akiwa hasikii yaani
kiziwi.
3.Ciproflaxin; hii ni dawa ambayo hupatikana
kwenye mfumo wa vidonge na sindano, mara
nyingi hutumika kutibu typhoid, UTI au magonjwa
ya njia za mkojo na magonjwa baadhi ya zinaa.
Dawa hii huharibu ukuuji wa mifupa ya mtoto na
huweza kutoa mtoto asiyetembea mwishoni.
4.Doxycline: hii ni dawa ambayo hupatikana kwa
mfumo wa dawa za kumeza kitaaalamu kama
capsules, dawa hizi ni antibiyotiki yaani hutumika
kuua bakteria wa aina tofauti. Bahati mbaya
huweza kuingilia mfumo wa utengenezaji wa
mtoto ikitumika miezi mitatu ya mwanzo na
kusababisha kuzaliwa na mtoto mwenye viungo
pungufu au zaidi.
5.Dawa ya mseto ya malaria au ALU; dawa hii ni
salama kipindi chote cha ujauzito isipokua miezi
mitatu ya kwanza ambapo dawa hii huweza
kuingilia ukuaji wa maumbile ya kwanza ya
mtoto[organogenesis} na kutoa mtoto asiye na
viungo vya kawaida.
6.Metronidazole au fragile; hii dawa ipo kwenye
kikundi cha antibayotiki yaani hushambulia
bakteria. Dawa hii hutumika mara nyingi kuua
minyoo ya amiba na kutibu magonjwa ya mfuko
wa uzazi wa mwanamke na ikitumika miezi
mitatu ya kwanza ya ujauzito huingilia mfumo wa
utengenezaji wa viungo vya mtoto.
7.Mesoprostol: hii ni dawa ambayo iko kwenye
kikundi maarufu cha prostanglandins analogue,
hutumika sana kuongeza njia ya mlango wa uzazi
kipindi cha kujifungua na pia hutumika kutibu
Vidonda ya tumboni hivyo matumizi ya dawa hii
kipindi cha ujauzito yana madhara makubwa mno
ikiwemo kutoa mimba kabisa.
8.Aspirin: hii ni dawa ya maumivu ambayo
humezwa mara kwa mara na hupatikana kirahisi
tu, lakini dawa hii ina uwezo wa kusababisha
kuvuja kwa damu nyingi hasa mama akipata
matatizo flani ya uzazi kama placenta previa. Sio
dawa nzuri sana kipindi cha ujauzito.
9.Praziquantel: hii ni dawa inayotumika kutibu
minyoo flani inayopatikana kwenye sehemu za
maji yaliyotuama, ni hatari sana kwa wamama
wajawazito kwani huiingilia mfumo wa ukuaji wa
mtoto.
10.Furesamide: hii ni dawa ambayo inapatikana
kwenye kikundi cha diuretic.. mara nyingi
hutumika kushusha ongezeko la maji nje ya
mfumo husika wa damu [oedema] na kutibu
presha kubwa ya damu. Sio dawa nzuri kwa
akina mama wajawazito kwani wajawazito hua na
presha ya chini kidogo hivyo huweza kuishusha
chini kabisa[intravascular volume depletion].

Usiache kutembelea kila siku kwenye blog hii kwa makala nyingi na bora za afya... Pia waweza ku subscribe kwa kuingiza email yako hapo chini na utapata makala zetu kwa urahisi zaidi punde tu inapopostiwa....

No comments:

Post a Comment

FEATURED POSTS

AFYA TIPS