Friday, June 30, 2017

CHANZO CHA MIMBA KUHARIBIKA NA DALILI ZAKE

HABARI ZENU WADAU!!

LEO NATAKA NIZUNGUMZIE
CHANZO CHA KUHARIBIKA KWA MIMBA MARA KWA MARA

KUHARIBIKA kwa MIMBA ni TATIZO linalowapata WANAWAKE wengi.

Si TATIZO linalowapata WANAWAKE MASIKINI TU ,hata MATAJIRI linawakumba.

MIMBA hutoka ikifikisha WIKI 36 hadi WIKI 38 wakati MTOTO anakuwa karibu KUZALIWA.

WENGI wenye MATATIZO haya wamekuwa wakitafuta MATIBABU hospitalini, kwenye MAOMBI maalum na hata kwa WAGANGA wa KIENYEJI .

SABABU za MIMBA kuharibika mara kwa mara KITAALAM hazijulikani ila kuna VYANZO vinavyojulikana kusaidia MIMBA kutoka.

Mbali na MIMBA zinazotolewa KIHARAMU, sababu za MIMBA zinazotoka bila kulazimishwa zinatajwa kuwa ni MAUMBILE ya KURITHI kwa maana ya kuwa na VINASABA ambavyo si vya KAWAIDA na kwa hiyo KIUMBE kinakuwa katika HALI ambayo KWA ASILI MIMBA haiwezi KUKUA na kama itakua na MTOTO kuzaliwa basi MTOTO huyo atakuwa na MATATIZO ya AJABU ya KIMAUMBILE na AKILI. Ni kwa SABABU hiyo MIMBA huharibika na kutoka yenyewe.

SABABU ya PILI ni KUTOKUA kwa YAI lililorutubishwa. Katika UUMBAJI.

YAI hukutana na MBEGU ya MWANAUME na MCHAKATO wa KIUMBE kukua huanza kwa YAI KUJITENGA mara MBILI .
UPANDE mmoja hutengeneza KONDO la NYUMA na KIFUKO cha kutunza MAJI na SEHEMU ya PILI hutengeneza KIUMBE au MTOTO .
HAPA hutokea SEHEMU ya KONDO la NYUMA ikiendelea KUKUA wakati SEHEMU ya MTOTO HAIKUI kabisa.

Katika MAZINGIRA kama haya,kama MAMA hajafanya VIPIMO vinavyoweza KUANGALIA moja kwa moja, anaweza kuendelea KUJIDANGANYA kama ni MJAMZITO kwani KIPIMO cha MKOJO kinaweza kuendelea KUONYESHA kuwa MAMA ni MJAMZITO.
Hata hivyo bado UJAUZITO utapotea kabla ya WIKI ya 24.

UVUTAJI wa SIGARA na UNYWAJI wa POMBE kupita KIASI wakati wa UJAUZITO huchangia MIMBA kuharibika.

Vilevile MSONGO wa MAWAZO na UKOSEFU wa LISHE huchangia kwa kiasi KIKUBWA UHARIBIKAJI wa UJAUZITO .

MAGONJWA yanayoathiri MWILI wa MAMA TUMBONI kama vile MALARIA , KASWENDE , na kadhalika.

DALILI za MIMBA KUHARIBIKA zinaanza na MJAMZITO kutokwa na MATONE ya DAMU na kupata MAUMIVU ya TUMBO chini ya KITOVU .

WAJAWAZITO wengine wanaweza KUTOKWA na DAMU bila KUHISI MAUMIVU ya TUMBO kabisa.

ASILIMIA kubwa ya MIMBA kuharibika hutokea katika KIPINDI cha AWALI kabisa cha UJAUZITO au NDANI ya WIKI 14 za UJAUZITO .

WANAWAKE wengi aidha kwa UELEWA MDOGO au DHARAU, hupuuza DALILI za KUTOKWA DAMU hasa kama ni KIDOGO huchelewa kwenda kumuona DAKTARI na MATOKEO yake MIMBA huharibika wakati ingeweza KUZUILIKA .

Iwapo MIMBA zinatoka bila KUWA na SABABU inayojulikana unatakiwa ufanyiwe UCHUNGUZI wa MAGONJWA ya KURITHI na MAGONJWA mengine yanayosabaisha MIMBA kuharibika.

ENDELEA KUWA NAMI MAKALA IJAYO TUTAJUA JINSI YA KUFANYA ILI MIMBA ISIHARIBIKE

Featured Post

FAIZA ZA KULA PAPAI

 _*Siri usioijua kuhusu utajiri wa tunda la papai katika kukulinda na magonjwa hatarishi kutokana na faida zake lukuki*_  Hizi ndizo FAIDA 1...