Powered By Blogger

Sunday, July 16, 2017

PID(PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI)

FAHAMU UGONJWA WA PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE AU MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI)

PID ni kifupi cha Pelvic Inflammatory Disease ambayo ni maambukizi ya vijududu vya bakteria katika mfumo wa ndani wa uzazi wa mwanamke. Maambukizi yanaweza kuwa katika mji wa uzazi, mirija ya uzazi, ovari au shingo ya uzazi.

PID husababishwa na vijidudu vya bakteria kuingia kwenye mji wa mimba kupitia mlango wa shingo ya uzazi. Vijidudu hivi hutokana na magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa kama kisonono au klamidia. Huingia kwenye mji wa uzazi na kisha kuweza kushambulia ovari,mirija au mji wa mimba wenyewe.

Dalili

P.I.D huleta dalili zifuatazo. Mgonjwa anaweza kupata zote au baadhi ya dalili hizi;

=>Maumivu ya kiuno
=>Kutokwa na uchafu ukeni
=>Maumivu wakati wa kufanya ngono
=>Kutokwa damu baada ya kufanya ngono
=>Maumivu chini ya kitovu baaada ya kufanya ngono
=>Maumivu wakati wa kukojoa
Mara nyingi dalili huwa sio kali na wakati mwingine zinaweza kutokea kwa kipindi cha muda mrefu. Wakati mwingine mwanamke anaweza kupatwa na dalili ghafla na kali hasa maumivu ya tumbo.

Vipimo
Vipimo hivi vinaweza kufanyika kujua kama kuna ugonjwa wa PID.

=>Kipimo cha ultrasound
=>Kipimo cha magonjwa ya zinaa (VDRL)
=>Kuotesha uchafu wa kwenye uke (Cervical/vaginal swab for culture)

Matibabu
Mara nyingi tatizo hili hutibiwa kwa njia ya dawa za antibiotics kwa muda wa siku 14 ni muhimu kuzingatia matumizi na kukamilisha dozi ya dawa ili kuhakikisha umepona kabisa.

Madhara
PID isipotibiwa huleta madhara kwa mgonjwa hasa ikiwa ni hali ya ugumba na hata utasa.

Kujikinga
Kujikinga na PID, ni muhimu kujikinga na magonjwa ya zinaa kwa;

kuwa na mpenzi mmoja uliyepima nae afya na magonjwa ya zinaa.
kutumia kondomu kila mara unapofanya ngono.
kuacha tabia ya kuwa na wapenzi wengi.
Unaposhisi dalili za magonjwa ya zinaa, wahi hospitali kupata matibabu sahihi na hakikisha umepona.

No comments:

Post a Comment

FEATURED POSTS

AFYA TIPS