MAAJABU YA JUISI YA UBUYU
Mungu ameumba miti na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi.
Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.
Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa.
1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya kalsiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini
4. Ina virutubisho vya kulinda mwili
5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili wa binadamu huwa na vitamin B2.
6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
7. Huongeza nuru ya macho
8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
9. Unga wa ubuyu una magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo
Unywe kiasi gani? Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.
Ili upate faida za juisi ya ubuyu, zinazoelezwa hapa, lazima upate ule ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.
Namna ya kuandaa hii juisi: Chukuwa unga wa ubuyu vijiko vikubwa vitatu, weka kwenye kikombe, ongeza maji robo lita na ukoroge vizuri, unaweza kuongeza sukari au asali kidogo kupata radha, tikisa na unywe.
Tuesday, August 8, 2017
Subscribe to:
Posts (Atom)
Featured Post
FAIZA ZA KULA PAPAI
_*Siri usioijua kuhusu utajiri wa tunda la papai katika kukulinda na magonjwa hatarishi kutokana na faida zake lukuki*_ Hizi ndizo FAIDA 1...

-
DAWA KUMI AMBAZO MAMA MJAMZITO HATAKIWI KUZITUMIA KABISA: Leo tutaangalia dawa ambazo jamii yetu hupenda sana kuzitumia lakini bahati mba...
-
FAIDA ZA KULA NANASI KWA AFYA YAKO Hapa tuta angalia faida kuu za kula nanasi na Wote tunajua kuwa kula matunda mazuri inasaidia mwili kupa...
-
LIJARIBU TUNDA HILI UJIONEE HAYA MACHACHE... Tunda hili lina faida nyingi pamoja na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuz...