Powered By Blogger

Saturday, July 8, 2017

NJIA RAHISI YA KUNG'ARISHA MENO YAKO

NAMNA RAHISI YA KUNG'ARISHA MENO YAKO

Katika somo hili nakuletea mbinu rahisi kabisa ya kung’arisha meno yako na yakaonekana meupe na yenye kupendeza.

Unahitaji vitu viwili, limau na baking soda au wengine huiita bicarbonate of soda nayo ni ile wamama huitumia wanapopika maandazi au mikate, inapatikana maduka ya kawaida hata kwa Mangi hapo nje ipo.

Namna ya kuandaa:

Chukua limau kubwa moja ikate katikati, chuja kupata maji maji yake (juisi) kisha changanya baking soda ya unga kijiko kidogo kimoja cha chai. Changanya vizuri mchanganyiko huo.

Sukutua kinywa chako vizuri ukitumia mswaki na huo mchanganyiko ndiyo iwe dawa yako ya meno. Sukutua (piga mswaki) taratibu kama dakika 3 hadi 5 hivi na mwisho jisafishe kinywa na maji safi.

Mhimu: Fanya zoezi hili nyakati za jioni au usiku unapokaribia kwenda kulala na ufanye mara moja tu kwa wiki na si zaidi ya hapo kwani unaweza kuharibu fizi zako kwa dawa hii usipokuwa makini.

Njia hii pia haisaidii kwa wale ambao wamezaliwa na meno ya rangi hivyo au kama matokeo ya kutumia maji yenye madini kwa muda mrefu kama vile watu wa mikoa ya Arusha au Moshi.

Ukifanya hivi mara 2 au 4 yaani mwezi mmoja utaona tayari meno yako yameanza kuwa meupe na yanayong’aa na kupendeza.

Vyakula kadhaa vifuatavyo vinasaidia kung’arisha meno yako navyo ni pamoja na machungwa, strawberry, mapeazi, maziwa, mtindi, maji ya kunywa, jibini (cheese), broccoli, celery, karoti, tufaa (apple), kitunguu maji, mbegu mbegu (kama korosho, karanga, almonds) nk .

Vyakula au vitu vinavyoharibu rangi ya meno ni pamoja na uvutaji tumbaku au sigara, chokoleti, chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi na vinywaji vingine baridi vyenye caffeine

No comments:

Post a Comment

FEATURED POSTS

AFYA TIPS