Friday, July 14, 2017

JINSI YA KUREKEBISHA MZUNGUKO WA HEDHI

Jinsi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi

Tatizo la kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi huanza ghafla au polepole ambapo mwanzo mwanamke alikuwa akipata siku zake katika utaratibu unaoeleweka lakini mara haelewi au hajielewi namna mzunguko wake unavyoenda.

Kuvurugika kwa hedhi ni kitendo cha mwanamke kuanza kuona siku zake bila tarehe au mzunguko maalumu na matokeo yake ni kuwa mwanamke atashindwa kutimiza malengo yake kwa kutumia mzunguko huo sababu ni haueleweki.

Unaweza kutokewa ghafla tu unapata hedhi mahali usipotarajia jambo linakufanya ubaki na woga na huelewi nini cha kufanya kwani hukuwa umejiandaa kwa tukio hilo kama matokeo ya siku zako kutokuwa mzunguko maalumu. Wakati mwingine unaweza kupitiliza mwezi hata miezi kadhaa bila kuona kabisa siku zako na hata ukipima ujauzito unakutwa huna ujauzito wala dalili huna.

Madhara ya kuvurugika kwa mzunguko ni pamoja na;  kushindwa kupata ujauzito, maambukizi katika kizazi na kuziba kwa mirija ya uzazi.

Kwanini unahitaji mzunguko wa hedhi ulio sawa?

Faida za kuwa na mzunguko wa hedhi ulio sawa:

Utakusaidia kupata ujaouzito ulioupangilia
Utakuepusha kupata ujauzito ambao hukuupangilia
Utaweza kuamua jinsia ya mtoto unayemtaka
Nini husababisha kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi

Ni rahisi kugundua kama mzunguko wako umevurugika ikiwa tu unauafahamu vizuri mzunguko wako ulio sahihi. Kufahamu mzunguko unahitaji uifahamu siku ambayo ulianza kuona damu hadi siku utakapoona tena katika mzunguko unaofuata. Karibu kila mwanamke huwa na mzunguko wake usiofanana na wa mwingine.

Tatizo linaweza kuanza kwa kurukaruka siku, mwanamke pia anaweza kupoteza siku yaani mwezi mwingine anaona na mwezi mwingine haoni, au anaingia mara mbili kwa mwezi au anaona damu ya hedhi kwa siku nyingi hata zaidi ya siku arobaini mfululizo. Damu yake inaweza kutokea kidogo kidogo kila siku au nyingi huku ikiambatana na mabongemabonge na maumivu pia. Maumivu haya ya wakati wa hedhi huenea chini ya tumbo mpaka miguuni na kiunoni.

Kuvurugika kwa hedhi kunaweza kutokea kutokana na sababu zifuatazo:

Mabadiliko ya mazingira ambayo hupelekea mfumo wa mwili hubadilika pia hasa mwanamke akitoka sehemu ya joto kwenda mikoa ya baridi au toka mikoa ya baridi kwenda mikoa ya joto.

1.Msongo wa mawazo (stress)
2.Hofu
3.Woga
4.Mabadiliko ya kisikolojia
5.Uvimbe kwenye kizazi
6.Matatizo kwenye mfumo wa homoni
7.Matatizo kwenye vifuko vya mayai
8.Mimba kuharibika
9.Maambukizi sugu ya kizazi pia ni mojawapo ya sababu.
Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ya mara kwa mara na kila ukipima unaambiwa ni ugonjwa wa U.T.I kumbe siyo yutiai
Kutokwa na uchafu ukeni
Maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Jinsi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi

Kabla ya yote unapopatwa na tatizo hili kwa muda mrefu ni vizuri ukaonana na daktari uweze kupata uchunguzi wa kutosha kubaini nini hasa inaweza kuwa ndiyo sababu hasa ya tatizo kwa upande wako.

Zifuatazo ni dawa mbadala 6 unazoweza kuzitumia ukiwa nyumbani ili kurekebisha tatizo hili

1. Papai

Papai ni moja ya dawa nzuri sana katika kutibu tatizo la kuvurugika kwa hedhi. Ina viinilishe mhimu kama carotene, chuma ( iron), Kalsiamu (calcium) na vitamini A na C ambavyo husaidia kulainisha na kunywea kirahisi kwa kuta za mji wa uzazi.
Siku 2 au 3 kabla ya kuanza kula papai kila siku nusu papai papai zima kutegemea na ukubwa wake au uwezo wako.

Kwa mtu mwelevu sababu ameshagundua papai laweza kumsaidia hivyo basi atalifanya papai kuwa sehemu ya chakula chake kila siku na si mpaka aumwe tu.

2. Mdalasini

Mdalasini unayo sifa ya kuondoa tatizo la damu kuganda sifa inayoweza kusaidia kuondoa tatizo la maumivu wakati wa hedhi.
Mdalasini ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (fiber), kalsiamu (calcium), chuma (iron) manganizi (manganese).

• Tengeneza chai ya tangawizi kwa kutumia kijiko kidogo cha mdalasini ya unga na maji kikombe kimoja (robo lita), ipua na uache ipowe kidogo, ongeza asali kijiko kikubwa kimoja ndani yake na unywe. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka mara tatu siku 2 au 3 kabla ya kuanza siku zako.

• Au changanya kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na kijiko kidogo kimoja cha asali katika glasi moja ya maji ya uvuguvugu na unywe kutwa mara 2 siku za mwanzoni unapoanza au kukaribia kuingia katika siku zako.

3. Tangawizi

Tangawizi ni dawa ya asili yenye maajabu katika kutibu tatizo la mvurugiko wa hedhi. Tangawizi hufanya kazi mhimu kabisa katika kushusha kiwango cha homoni inayosababisha maumivu ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘prostaglandins’. Tangawizi husaidia pia katika kupigana na uchovu uletwao na mzunguko wa hedhi katika siku zile za mwanzo au siku 2 hivi kabla ya kuanza siku zako na huweza pia kufanya mzunguko usio sawa wa hedhi kuwa sawa

• Tengeneza chai ya tangawizi ukitumia tangawizi mbichi, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 wakati wa siku zako au siku yoyote tu kama kinga. Kamulia ndimu kidogo ndani yake na utumie asali kupata radha badala ya sukari.

• Unaweza pia kuongeza tangawizi kwenye vyakula na mboga mboga nyingi unazopika kila siku.

4. KOTIMIRI (Parsley):

Tengeneza juisi ya kotimiri, viazi pori (Beet Root), karoti au matango. Tumia asali mbichi ukitengeneza juisi hii. Hii kotimiri inapatikana kirahisi Dar na Zanzibar ni mboga mboga inayotumika zaidi kwenye mahoteli ya kitalii. Mboga hii inacho kitu mhimu sana kijulikanacho kama ‘Apiol’ amabcho kazi yake kuu ni kurekebisha na kuweka sawa homoni za kike.

Changanya kwa ujazo sawa yaani kama juisi ya kotimiri ni kikombe kimoja basi ya kiazi pori nayo kikombe kimoja kadharika kwa matango. Juisi hii ni dawa tosha ya maumivu wakati wa siku za hedhi, hurekebisha mzunguko wa hedhi na imethibitika kuwa bora kuliko dawa nyingi za kizungu.

Kunywa glasi moja ya juisi hii kutwa mara 2.

5. MREHANI

Mrehani au Basil kwa Kiingereza ni mmea mwingine mzuri sana katika kuondoa maumivu wakati wa hedhi na kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa ujumla. Mmea huu unatumika sana jikoni kwenye mahotel ya kitalii Dar na Zanzibar. Unao sifa kuu ya kuzuia au kuondoa maumivu mwilini.

• Ongeza kijiko kikubwa kimoja cha majani freshi ya mrehani yaliyokatwakatwa na kisu (chop) kwenye kikombe kimoja cha maji ya moto, funika vizuri na usubiri ipowe. Kunywa yote ikishapoa na ufanye zoezi hili kutwa mara 3 kwa wiki 3 mpaka 4 au mpaka tatizo lako limeisha.

• Au tengeneza juisi ya majani haya. Yatwange kwenye kinu au kwenye blenda ya umee kupata majimaji yake kisha chota vijiko vya chai viwili uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto na unywe yote. Fanya zoezi hili kutwa mara 3.

• Unaweza pia kuongeza majani freshi ya mrehani kwenye vyakula vingi unavyokula kila siku.

6. MAJI YA KUNYWA

Matatizo karibu yote mwilini chanzo chake ni mwili kutokuwa na maji ya kutosha. Maji ni uhai. Unachohitaji hapa ni kutokusubiri kiu. Kiu ni ishara ya mwili iliyochelewa kuhitaji maji.

Matatizo mengi ya kiafya tumeyaona kwa watu wasiopenda kunywa maji ya kutosha kila siku.

Jitahidi hata iweje iwe unaumwa au huumwi chochote unywe maji lita mbili mpaka tatu kila siku iendayo kwa Mungu na utaniletea mrejesho hapa hapa.

Kama una swali au unahitaji ushauri wowote liulize hapo kwenye comment nitakujibu.

Tuesday, July 11, 2017

MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI NA SULUHU ZAKE ILI KUPATA MTOTO

FAHAMU TATIZO LA MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI NA KUZIBA PAMOJA NA SULUHU YAKE ILI KUPATA MTOTO

MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI NI NINI?
Hali ya kujaa maji kwa mirija ya uzazi ya wanawake huitwa hydrosalpinx kwa kitaalamu. Ni tatizo ambalo hujitokeza kwa wanawake kutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa (pelvic inflammatory disease). Mara nyingi husababisha tatizo la ugumba na maumivu ya kiuno.
Mirija ya uzazi hujishikiza kwenye upande wa kulia na kushoto wa tumbo la uzazi, hupitisha mayai kila mwezi kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mji wa uzazi. Urutubishaji wa yai la uzazi hutokea katika mirija hii.

SABABU ZA MIRIJA YA UZAZI KUZIBA

Mara nyingi mirija ya uzazi kuziba hutokana na;
Pelvic inflammatory disease unaotokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa kama kisonono na klamidia.TB ya mirija ya uzaziUpasuaji maeneo ya kiunoni (pelvic surgery)EndometriosisMaambukizi ya apendiksi (appendicitis)Saratani ya mirija ya uzazi

DALILI ZA TATIZO HILI
Wanawake wengi wanaweza wasiwe na dalili zozote, isipokuwa kupata matatizo katika kupata mtoto. Dalili zinazojitokeza mara nyingi huwa ni;
Maumivu ya kiuno
Hujitokeza mara kwa mara hasa siku chache kabla au baada ya kuingia kwenye hedhi.
Uchafu kutoka sehemu za siri

JINSI YA KUGUNDUA TATIZO HILI
Kuna vipimo kadhaa vya kuwezesha kujua kama mirija yako ya uzazi imeziba na kujaa maji:
Hysterosalpingogram
Hii ni aina maalumu ya X-ray ya kiuno, ambayo kimiminika maalumu huingizwa ndani ya mji wa uzazi kwa kupitia shingo ya uzazi. Kama mirija haijaziba, kimiminika huweza kupita mpaka ndani ya kiuno na kama imeziba haitaweza kupita. Hii itaonekana kwenye hiyohysterosalpingogram.
Ultrasound ya kiunoni (Pelvic Ultrasound)
Ultrasound itaweza kuonesha kama mirija yako imeziba na kujaa, na ukubwa wake. Pia itaweza kuonesha kama kuna matatizo mengine kwenye via vya uzazi vya ndani.
Upasuaji wa Tumbo(Laparoscopy)
Upasuaji huu hufanyika kwa kutumia mirija maalumu yenye kamera ili kutazama mirija hiyo. Matundu mawili hutobolewa tumboni ili kupitisha mirija hii.

JE,NAWEZA KUPATA MTOTO ?
Tatizo hili likitibiwa unaweza ukapata mtoto. Pale mirija inapokuwa imeharibika sana uwezekano wa kupata ujauzito huwa ni mdogo sana. Njia nyingine saidizi kama In Vitro Fertilization zinaweza kutumika.

MADAHARA YA TATIZO HILI
Mirija ya uzazi ikiziba, mayai ya uzazi hushindwa kusafiri kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mji wa uzazi. Hivyo tatizo la ugumba hujitokeza.Mimba kutunga nje ya mfuko wa mimba (Ectopic pregnancy)
Maumivu ya kiuno
Vaginal Atrophy (kusinyaa kwa uke na kushindwa kufanya tendo la ndoa)
Kukosa hamu ya tendo la ndoa
Kuwa mkavu Ukeni, na kuhisi maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.

MATIBABU
Matibabu ya kuziba mirija hufanyika kwa njia ya upasuaji ili kuondoa sehemu iliyoziba. Upasuaji kwa njia ya matundu (laparoscopy ) unaweza kufanyika kutibu tatizo hili. Katika upasuaji sehemu zilizoziba au kushikamana huondolewa na zilizo nzima kuunganishwa tena.

Monday, July 10, 2017

FAIDA ZA PARACHICHI NA JUISI YAKE

Tupate Elimu Juu PARACHICHI
Parachichi ni tunda ambalo mti wake hujulikana kisayansi kama Persea amerikana.  Tunda hili lina aminika kuwa na asili kutoka jimbo la Puebla, bara Amerika ya kusini kunako nchi ya Mexico. Ushahidi wa kale kabisa, takribani miaka 10000 BC umeonyesha parachichi lilitumika katika jimbo la Puebla nchini Mexico. Lakini kutokana na faida nyingi kiafya zipatikanazo kwa ulaji wa tunda hili, tunda hili sasa hupatikana na kutumika kwa lishe sehemu nyingi duniani hususani barani Afrika.

Parachichi ni tunda la pekee ukilinganisha na matunda mengine, kimsingi matunda mengine huwa yana wanga(carbohydrate) kwa wingi, wakati parachichi lina aina ya mafuta ambayo yana faida kwa afya.

Parachichi katika tafiti nyingi limeonekana kuwa na faida katika afya ya moyo. Wagonjwa wa moyo wamekuwa katika makatazo ya kutumia aina ya mafuta ambayo yamekuwa yakichangia kuongezeka kwa lehemu katika damu(mafuta hayo kitaalam kama polysaturated fat), na kuongeza matumizi ya mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu (monosaturated fat). Parachichi ni chanzo kizuri cha mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu. Utafiti unaonyesha kuwa matumizi ya mafuta haya  katika parachi hupunguza lehemu iliyo hatari ( kitaalam kama, Low density lipoprotein), na huchangia katika ongezeko la lehemu isiyo hatari( High density lipoprotein).
Madini ya Potasiamu ni aina ambayo huwa watu hawapati ya kutosha kutoka katika vyakula. Parachichi lina kiwango kikubwa cha madini ya potassium kuliko ndizi. Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa matumizi ya madini haya huambatana na kupungua kwa shinikizo la damu, shinikizo la juu la damu laweza kupelekea mtu kupata kiharusi, shambulizi la moyo hata figo kushindwa kufanya kazi.

Parachichi lina kiwango kikubwa cha fiba. Fiba ni kirutubisho kutoka katika vyakula vya jamii ya mimea, fiba huwa hazimeng’enywi tumboni lakini huwa zina umuhimu mkubwa sana, kama kusaidia kupunguza uzito wa mwili, kusaidia urekebishaji wa kiwango cha sukari mwilini na kupunguza hatari ya kupata magonjwa mengi mwilini. Kuna aina fulani ya fiba ambazo huwa ni virutubisho kwa ajili ya bakteria wenye faida tumboni, hii huimarisha kinga ya mwili na kusaidia mwili kufanya kazi katika kiwango kinachotakiwa. Kwa kuwa parachichi lina kiwango kikubwa cha fiba, husaidia kuboresha mmeng’enyo na kupata choo katika hali ya kawaida.

Aina ya mafuta na virutubisho tulivyoviona awali katika parachichi vinasaidia afya ya ngozi yako. Husaidia ngozi yako kutokuwa kavu na kuwa na unyevu unaotakiwa na kuifanya ngozi kuwa laini na yenye afya. Vitamini C husaidia katika kusaidia uponaji haraka wa ngozi na kujijenga upya kwa seli za ngozi zilizoharibika,husaidia kujenga elastini na collageni ambazo ni muhimu katika ngozi. Uwepo wa virutubisho viondoavyo sumu(antioxidants) katika parachichi kama carotenoidi na vitamini E, hutusaidia kutukinga na mionzi mikali ya jua, kwa hiyo huzuia makunyanzi katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuwa na mwonekano mzuri wakati wote.

Tunda hili ni lishe bora kwa wale wenye kisukari. Parachichi lina kiwango kidogo cha sukari ukilinganisha na matunda mengine. Pia uwepo wa mafuta aina ya ‘monosaturated’ husaidia kuboresha ufanyaji kazi wa homoni ya insulini, katika urekebishaji wa kiwango cha sukari mwilini. Faida nyingine ni kuwa Vitamini C  katika parachichi husaidia kuimarisha mishipa ya damu na kuboresha kinga ya mwili ambayo ni faida kubwa kwa wagonjwa wenye kisukari.

Faida katika afya ya uzazi ni dhahiri. Parachichi lina Vitamini E ambayo ni “antioxidant”  Potasiamu, Vitamini B6,Vitamini C ambazo hutusaidia kutukinga na magonjwa ya moyo hata yale ya kisukari. Chochote kile kinachosaidia afya ya moyo pia husaidia afya ya uzazi. Wanaume wenye magonjwa ya moyo na kisukari huwa tatizo kubwa la upungufu wa nguvu za kiume.

Parachichi pia limeonekana kuwa na faida nyingi katika kuboresha afya ya macho, viungo vya mwili na nyinginezo nyingi. Katika utafiti mmoja uko Marekani, ulionyesha kuwa watu walao parachichi walionekana kuwa na afya bora ukilinganisha na wale wasiokula parachichi. Waliokula parachichi hawakupatwa  na matatizo ya mmeng’enyo  ukilinganisha na wale wasiokula. Matatizo ya mmeng’enyo huchangia watu kupatwa na magonjwa ya moyo na kisukari.

Hapo ni kwa mafupi tu, Ila kwa ushauri Tuwe tunapendelea kutumia matunda mara kwa mara ili kuweza kupata faida za kiafya na kuboresha miili yetu dhidi ya matatizo madogo madogo ambayo yakikua yanakua ni makubwa na yasiyokua rahisi kuyakabili.
Ukienda sokoni usisahau parachichi aka Avocado.

Waweza ku subscribe katika blog hii ili uwe wa kwanza kupata makala hizi za afya kwa kuingiza email yako..

Saturday, July 8, 2017

NJIA RAHISI YA KUNG'ARISHA MENO YAKO

NAMNA RAHISI YA KUNG'ARISHA MENO YAKO

Katika somo hili nakuletea mbinu rahisi kabisa ya kung’arisha meno yako na yakaonekana meupe na yenye kupendeza.

Unahitaji vitu viwili, limau na baking soda au wengine huiita bicarbonate of soda nayo ni ile wamama huitumia wanapopika maandazi au mikate, inapatikana maduka ya kawaida hata kwa Mangi hapo nje ipo.

Namna ya kuandaa:

Chukua limau kubwa moja ikate katikati, chuja kupata maji maji yake (juisi) kisha changanya baking soda ya unga kijiko kidogo kimoja cha chai. Changanya vizuri mchanganyiko huo.

Sukutua kinywa chako vizuri ukitumia mswaki na huo mchanganyiko ndiyo iwe dawa yako ya meno. Sukutua (piga mswaki) taratibu kama dakika 3 hadi 5 hivi na mwisho jisafishe kinywa na maji safi.

Mhimu: Fanya zoezi hili nyakati za jioni au usiku unapokaribia kwenda kulala na ufanye mara moja tu kwa wiki na si zaidi ya hapo kwani unaweza kuharibu fizi zako kwa dawa hii usipokuwa makini.

Njia hii pia haisaidii kwa wale ambao wamezaliwa na meno ya rangi hivyo au kama matokeo ya kutumia maji yenye madini kwa muda mrefu kama vile watu wa mikoa ya Arusha au Moshi.

Ukifanya hivi mara 2 au 4 yaani mwezi mmoja utaona tayari meno yako yameanza kuwa meupe na yanayong’aa na kupendeza.

Vyakula kadhaa vifuatavyo vinasaidia kung’arisha meno yako navyo ni pamoja na machungwa, strawberry, mapeazi, maziwa, mtindi, maji ya kunywa, jibini (cheese), broccoli, celery, karoti, tufaa (apple), kitunguu maji, mbegu mbegu (kama korosho, karanga, almonds) nk .

Vyakula au vitu vinavyoharibu rangi ya meno ni pamoja na uvutaji tumbaku au sigara, chokoleti, chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi na vinywaji vingine baridi vyenye caffeine

Thursday, July 6, 2017

JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIKE AU WA KIUME KWA NJIA ZA KIBAILOJIA

MTOTO WA KIUME AU WA KIKE ANATOKEAJE?

Katika urutubishaji yai la mwanamke linabeba chromosome X yani XX
Na mbegu ya mwanaume inabeba chromosome XY
Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na Y kutoka kwa mwanaume mtoto wa kiume hupatikana
Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na X kutoka kwa mwanaume mtoto wa kike hupatikana
FAHAMU SIFA ZA CHROMOSOMES X na Y za mwanaume
Ili uweze kufanikiwa kuchagua mtoto wa kiume au wa kike lazima ujue sifa za chromosomes hizi zinazoamua jinsia ya mtoto
SIFA ZA CHROMOSOMES Y
1.Zina spidi kubwa sana kwahiyo kama yai lipo tayari zenyewe zitawahi kwenda kurutubisha
2.Zina maisha mafupi sana kulinganisha na X
SIFA ZA CHROMOSOMES X
1.Zina spidi ndogo sana
2.Zina maisha marefu kulinganisha na Y
Baada ya kujua sifa za chromosome ambazo ndo zinatusaidia kuamua jinsia twende moja kwa moja kwenye jinsi ya kupata mtoto wa jinsia unayotaka
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUAMUA JINSIA
1.Lazima mwanamke ajue mzunguko wake (menstrual cycle)siku ya 1-28
2.Lazima mzunguko wako uwe na mpangilio sahihi(unaweza ukachunguza mzunguko wako kwa miezi minne mfululizo)
3.PH ya uke lazima iwe kiwango sahihi 4-5.5(Tumia neplily pad kwa kuwa na PH sahihi
4.Ushirikiano kati ya mwanamke na mwanaume

JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIUME
Ili uweze kupata mtoto wa kiume kisayansi unashauriwa kushiriki tendo la ndoa siku ambayo yai litakuwa limetoka kama mzunguko wako uko sahihi ni siku ya 14
Njia nyingine ya kujua yai limetoka baba anaingiza vidole viwili ukeni wakati wa asubuhi na ukikuta uteute ujue yai limetoka kwahiyo jioni mnashiriki tendo la ndoa kwa ajili ya kupata mtoto wa kiume

KWANINI USHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI YAI LIMETOKA ILI KUPATA MTOTO WA KIUME?
Kisayansi chromosome Y ambayo inahusika katika kutunga mimba ya mtoto wa kiume ina spidi kubwa sana ni nyepesi na haiwezi kuishi mda mrefu kwahiyo ukishiriki tendo la ndoa wakati yai limetoka maana ake unaongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume

JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIKE
Ili ufanikiwe kupata mtoto wa kike utatakiwa ushiriki tendo la ndoa siku tatu kabla ya yai kupevuka yani hapa ni baada ya kujua mzunguko
KWANINI USHIRIKI TENDO LA NDOA SIKU TATU KABLA
Hii ni kwasababu chromosome X ambazo ndo zinaunda mtoto wa kike huwa zina sifa ya kuwa na maisha marefu na kutembea taratibu hivyo yai likitolewa litakuta chromosome X ziko hai

KUNA BAADHI YA WAZEE WA ZAMANI WANAAMINI HAYA KATIKA KUPATA MTOTO WA JINSIA UNAYOTAKA
KUPATA WA KIKE
Kula samaki ,mboga za majani,matunda,bidhaa za maziwa,mbegu za matikiti maji na alzeti nk
Wakati wa kufanya tendo la ndoa mwanamke akae juu nk

KUPATA WA KIUME
Kula nyama, ndizi ,Vyakula vya chumvi kama chips ila usizidishe chumvi,karanga na vyakula vingine vya potassium na sodium
Chromosomes Y zinahitaji pH ya alkane kuliko asidi ndio maana wazee waliona hili
Kuna mengi kuhusu wazee wa zamani ila nmeongelea haya ya mlo kwa maana yana mantiki kibaiolojia

MAMBO YANAYOWEZA ATHIRI KUPATA MTOTO UNAYEMTAKA
1.Kushindwa kuhesabu siku( tumia chart niliyokuwekea)
2.Mzunguko mbovu wa hedhi(Tumia neplily pad)
3.KUtokuwa na PH sahihi ukeni tumia Neplily

Tuesday, July 4, 2017

DAWA KUMI ZENYE MADHARA KWA MAMA MJAMZITO

DAWA KUMI AMBAZO MAMA MJAMZITO HATAKIWI KUZITUMIA KABISA:

Leo tutaangalia dawa ambazo jamii yetu hupenda
sana kuzitumia lakini  bahati mbaya baadhi ya
dawa hizo hazitakiwi kupewa kwa wajawazito
kabisa kulingana na madhara makubwa
yanayoambatana na dawa hizo kwa mtoto
aliyepo tumboni.
Zifuatazo ni dawa hizo.

1.Albendazole; hii ni dawa ya minyoo ambayo
hutumika mara kwa mara kujitibu lakini ni dawa
mbaya sana kwa akina mama wajawazito kwani
una uwezo wa kutoa mimba kabisa hivyo
mebendazole hutumika kama mbadala.
2.Gentamycin: hii ni dawa ambayo iko kwenye
mfumo wa sindano tu, mara nyingi hutumika
kutibu magonjwa ya mfumo wa mkojo. Dawa hii
huharibu kabisa mishipa ya fahamu kitaalamu
kama auditory nerve ambayo hutufanya sisi
kusikia. Hivyo matumizi ya dawa hii huweza
kusababisha mtoto kuzaliwa akiwa hasikii yaani
kiziwi.
3.Ciproflaxin; hii ni dawa ambayo hupatikana
kwenye mfumo wa vidonge na sindano, mara
nyingi hutumika kutibu typhoid, UTI au magonjwa
ya njia za mkojo na magonjwa baadhi ya zinaa.
Dawa hii huharibu ukuuji wa mifupa ya mtoto na
huweza kutoa mtoto asiyetembea mwishoni.
4.Doxycline: hii ni dawa ambayo hupatikana kwa
mfumo wa dawa za kumeza kitaaalamu kama
capsules, dawa hizi ni antibiyotiki yaani hutumika
kuua bakteria wa aina tofauti. Bahati mbaya
huweza kuingilia mfumo wa utengenezaji wa
mtoto ikitumika miezi mitatu ya mwanzo na
kusababisha kuzaliwa na mtoto mwenye viungo
pungufu au zaidi.
5.Dawa ya mseto ya malaria au ALU; dawa hii ni
salama kipindi chote cha ujauzito isipokua miezi
mitatu ya kwanza ambapo dawa hii huweza
kuingilia ukuaji wa maumbile ya kwanza ya
mtoto[organogenesis} na kutoa mtoto asiye na
viungo vya kawaida.
6.Metronidazole au fragile; hii dawa ipo kwenye
kikundi cha antibayotiki yaani hushambulia
bakteria. Dawa hii hutumika mara nyingi kuua
minyoo ya amiba na kutibu magonjwa ya mfuko
wa uzazi wa mwanamke na ikitumika miezi
mitatu ya kwanza ya ujauzito huingilia mfumo wa
utengenezaji wa viungo vya mtoto.
7.Mesoprostol: hii ni dawa ambayo iko kwenye
kikundi maarufu cha prostanglandins analogue,
hutumika sana kuongeza njia ya mlango wa uzazi
kipindi cha kujifungua na pia hutumika kutibu
Vidonda ya tumboni hivyo matumizi ya dawa hii
kipindi cha ujauzito yana madhara makubwa mno
ikiwemo kutoa mimba kabisa.
8.Aspirin: hii ni dawa ya maumivu ambayo
humezwa mara kwa mara na hupatikana kirahisi
tu, lakini dawa hii ina uwezo wa kusababisha
kuvuja kwa damu nyingi hasa mama akipata
matatizo flani ya uzazi kama placenta previa. Sio
dawa nzuri sana kipindi cha ujauzito.
9.Praziquantel: hii ni dawa inayotumika kutibu
minyoo flani inayopatikana kwenye sehemu za
maji yaliyotuama, ni hatari sana kwa wamama
wajawazito kwani huiingilia mfumo wa ukuaji wa
mtoto.
10.Furesamide: hii ni dawa ambayo inapatikana
kwenye kikundi cha diuretic.. mara nyingi
hutumika kushusha ongezeko la maji nje ya
mfumo husika wa damu [oedema] na kutibu
presha kubwa ya damu. Sio dawa nzuri kwa
akina mama wajawazito kwani wajawazito hua na
presha ya chini kidogo hivyo huweza kuishusha
chini kabisa[intravascular volume depletion].

Usiache kutembelea kila siku kwenye blog hii kwa makala nyingi na bora za afya... Pia waweza ku subscribe kwa kuingiza email yako hapo chini na utapata makala zetu kwa urahisi zaidi punde tu inapopostiwa....

Sunday, July 2, 2017

SABABU,DALILI NA MADHARA YA SHINIKIZO LA DAMU[PRESSURE]

UGONJWA WA PRESSURE (SHINIKIZO LA DAMU )

Nini maana ya shinikizo la damu?

Ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa muda mrefu. Msukumo wa damu huhitajika mwilini ili kusambaza chakula, oksijeni na kutoa uchafu.

Shinikizo la damu hupimwa kwa kutumia kifaa kinachoitwa Sphygmomanometer

Shinikizo la damu husababishwa na nini?

Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu la damu:

- Uvutaji sigara
- Unene na uzito kupita kiasi
- Unywaji wa pombe
- Upungufu wa madini ya potassium
- Upungufu wa vitamin D
- Umri mkubwa
- Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
- Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin

*Uanishaji wa shinikizo la damu

- Presha ya kawaida <120 <80
- Presha inayoelekea kupanda 120-139 80-89
- Presha hatua ya 1 140-159 90-99
- Presha hatua ya 2 160-179 100-109
- Presha hatua ya 3 ≥180 ≥110

Shinikizo la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi sana duniani na hii ni kutokana na kutokujuwa ni nini hasa husababisha ugonjwa huu mwilini. Shinikizo la damu linaonekana kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata masharti.

Katika makala hii tutaona uhusiano mkubwa uliopo kati ya upungufu wa maji mwilini na ugonjwa huu, mwishoni utakuwa umeelewa sasa ni jinsi gani ilivyo rahisi kabisa kujiepusha na kujiponya ugonjwa huu. Endelea kusoma.

Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku likisababisha mshtuko wa moyo (Heart Attacks), kupooza na kiharusi (Strokes).

Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.

Dalili za shinikizo la damu:

- Maumivu ya kichwa (Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi nyakati za asubuhi),
- Kuchanganyikiwa,
- Kizunguzungu,
- Kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni),
- Kutoweza kuona vizuri au
- Matukio ya kuzirai.
- Uchovu/kujisikia kuchokachoka
- Mapigo ya moyo kwenda haraka
- Kutokuweza kuona vizuri
- Damu kutoka puani
Uonapo dalili hizi unapaswa kuwahi hospitali kupata vipimo.

‘Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi, una kiu, usiitibu kiu na madawa – dr. Batmanghelidj’.

Shinikizo la damu (hasa la juu) ni kiashiria cha mwili kupungukiwa maji kwa kiwango kikubwa, ni wakati ambapo mwili unajaribu kujizoesha na upungufu wa jumla wa maji wakati kunapokuwa hakuna maji ya kutosha kuijaza mishipa ya damu yenye kazi ya kusambaza maji kwenye seli mhimu.

Mishipa ya damu imebuniwa maalumu kuendana na mtiririko uliosawa wa ujazo wake wa damu na mahitaji mbalimbali ya tishu kwa kufunga na kufungua mishipa mbalimbali ya damu ndani ya mwili.

Figo hushtuka upesi kulingana na mtiririko wa damu. Hili linaposhindikana, yaani iwapo mtiririko au ujazo wa damu utapungua, basi Figo huitoa homoni iitwayo ‘renini’ ambayo yenyewe huzarisha kitu kiitwacho ‘angiotensini’ ambayo huwa na matokeo mawili; kwanza huzibana ateri na kupandisha shinikizo la damu, pili huisababisha tezi ya ‘adreno’ kutoa homoni iitwayo ‘aldosteroni’ ambayo huzifanya figo kuishikilia chumvi na hivyo kusababisha kupanda kwa shinikizo la damu.

Asilimia 94 ya damu ni maji. Kwa ujumla kila seli ndani ya miili yetu ina bahari ya maji baridi ndani yake na bahari ya maji chumvi nje yake. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa maji ya bahari hizo mbili.

Chumvi inayashikilia na kuyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli (osmotic retention) na potasiamu inayashikilia maji ndani ya seli.

Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji (yaani haunywi maji ya kutosha kila siku) mwili utaongeza ujazo wa maji chumvi kwenye bahari ya nje ya seli.

Kupitia mfumo maalumu, homoni iitwayo ‘vasopressini’ hutolewa ambayo inaweza kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli na kuyachoma maji hayo baridi (baada ya kuwa yamechujwa) ndani katikati ya bahari ya ndani ya seli kama yanavyohitajika ili kuutunza uwiano sawa wa maji ndani na nje ya seli.

Lakini ili mbinu hii ifanikiwe, mbinu gani, mbinu ya kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli, vasopressini husababisha kapilari na mishipa ya damu kujikaza au kupunguza vipenyo vyake na kukupatia wewe shinikizo la juu la damu (BP) ambalo ni mhimu ili kuyachuja na kuyachoma maji baridi ndani ya seli toka katika bahari ya maji chumvi iliyopo nje ya seli.

Kama mishipa ya damu haitapunguza vipenyo vyake, baadhi ya gesi itaachana na damu ili kuziba nafasi zilizowazi kutokana na kupungua kwa umajimaji mwilini na hatimaye kukusababishia msongamano wa Gesi (Gas locks).

Sifa hii ya vipenyo vya mishipa ya damu kujirekebisha kwa ajili ya mzunguko wa damu, ndiyo mtindo unaotumika zaidi katika kanuni za kihaidroliki wakati ambapo mzunguko wa damu mwilini umejirekebisha kuendana na kiasi cha umajimaji kinachopatikana.

Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji kwa mfano kutokana na kutokunywa maji ya kutosha; asilimia 66 ya kuishiwa maji inajionesha kwa kupungua kwa ujazo wa seli, asilimia 26 inapotea toka ujazo wa umajimaji uliopo sehemu ya nje ya seli na asilimia 8 tu inapotea toka katika ujazo wa damu.

Shinikizo la juu la damu ni kiashirio cha mwili kupungukiwa maji kwa asilimia 8 tu, lakini madhara yanajitokeza sababu ya asilimia 66 ya kupunguwa kwa ujazo wa seli.

Maji na chumvi vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida.

Hii ndiyo sababu shinikizo la damu linapaswa kutibiwa kwa kuongeza unywaji wa maji pekee. Dr.Batmanghelidj anasema; Maji peke yake, ni dawa bora ya kukojosha, pekee ya asili tuwezayo kuiendea.

Kama watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu wangeongeza kiasi cha uchukuaji maji, hawatazihitaji dawa za kukojosha, watazarisha mkojo wa kutosha na hivyo kuiondoa chumvi iliyokuwa imezidi!. Watatakiwa pia kuacha kula vyakula visivyo na chumvi na hivyo kuepukana na mikakamao ya mishipa (cramps) kwenye miguu yao.

* Madhara yanayoweza kuletwa na shinikizo la damu:

Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, kutokulielewa shinikizo la damu kama moja ya ishara za mwili kupungukiwa maji na kulitibu kwa dawa za kukojosha ambazo zinaukausha mwili zaidi, baada ya muda zitasababisha;

- Kuzibika kwa ateri za moyo na ateri ziendazo kwenye ubongo
- Shambulio la moyo (heart attack)
- Mishtuko midogo midogo au mikubwa inayopelekea kuzimia
- Ugonjwa wa kibofu cha mkojo
- Kiharusi
- Kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wanaume
- Kuharibiwa kwa ubongo na matatizo ya akili kama vile kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Daktari mwingine, Dr.David Brownstein katika kitabu chake kiitwacho; “Salt Your Way to Live”, anasema kwamba alifundishwa katika vyuo vya kiganga kuwa chumvi husababisha shinikizo la damu na kuwa kila mmoja lazima ale vyakula vyenye chumvi kidogo. Na hili watu wengi wamekuwa wakiamini hivi.

Wakati akiwatibu wagonjwa wake, anasema; alianza kuona kuwa wale wanaotumia vyakula vyenye chumvi kidogo wanapata matokeo ya chini au wanapata nafuu ndogo sana kutoka katika vyakula hivyo vyenye chumvi kidogo au bila chumvi kabisa na wengi wao walitokewa kuwa na uhaba mkubwa wa madini katika miili yao.

Katika utafiti wake ili kuwasaidia wagonjwa wake, ndipo akaja na jibu la chumvi ya baharini ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ambayo huwa na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake, alianza kuona kitu kigeni kinaanza kutokea. Wagonjwa wake hao wakaanza kuona mashinikizo yao ya damu yanaanza kushuka katika kiwango ambacho wanaweza kuachana kabisa na matumizi ya dawa.

Dr.Batmanghelidj anasema, ikiwa watu watajishughulisha na mazoezi hasa mazoezi ya kutembea kwa miguu, watakunywa maji halisi zaidi na kuongeza chumvi (siyo sodiamu) kidogo ya ziada kwenye vyakula vyao, mashinikizo yao ya damu yatarudi katika hali yake ya kawaida.

Swali la kujiuliza; Ni zaidi ya miongo minne sasa tangu tulipoambiwa kula vyakula vyenye chumvi kidogo ili kuepukana na shinikizo la damu, kwanini sasa Idadi ya watu wanaopatwa na ugonjwa huu inazidi kuongezeka?.

Narudia tena, mwili unapoanza kuishikilia chumvi, hufanya hivyo ili kuhifadhi maji, toka katika bahari chumvi hiyo ya nje ya seli, maji huchujwa na kutumika wakati wa mahitaji ya dharura.

Maji na chumvi kwa pamoja vitalirudisha shinikizo la damu katika hali yake ya kawaida. Kuikimbia chumvi kunasababisha shinikizo la damu (BP) kuwa sehemu ya maisha yetu, tutapata nafuu, lakini baada ya muda mfupi hali hurudi ileile na pengine kuwa watumwa wa kuchagua kula hiki au kile.

Tofauti na zamani ambapo shinikizo la juu la damu lilipokuwa ni ugonjwa wa watu wanene au wenye uzito uliozidi pekee, siku hizi wanene kwa wembamba, watoto kwa wakubwa wanaugua BP.

Featured Post

FAIZA ZA KULA PAPAI

 _*Siri usioijua kuhusu utajiri wa tunda la papai katika kukulinda na magonjwa hatarishi kutokana na faida zake lukuki*_  Hizi ndizo FAIDA 1...