Powered By Blogger

Wednesday, June 14, 2017

FAIDA TISA(9) ZA KULA NANASI

FAIDA ZA KULA NANASI KWA AFYA YAKO

Hapa tuta angalia faida kuu za kula nanasi na Wote tunajua kuwa kula matunda mazuri inasaidia mwili kupata vitamin na madini mbalimbali na kuwa mtu mwenye afya njema, na sasa tunda la nanasi ni tunda moja wapo ambalo ni muhimu sana hasa katika msimu huu wa mananasi.

1: Mmeng’enyo wa chakula.

Nanasi linasaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula kwa kiasi kikubwa sana. Hii inatokana na kuwa nanasi linatoa aina protini katika mwili wako ambayo inarahisisha kazi hii ya kumeng’enya chakula.

2: Nanasi Lina Vitamin na Madini

Tunda la nanasi limejaa madini na protini nyingi ambazo zinafaa kwa mwili wako. Nanasi lina vitamin A Vitamini C calcium, fiber na pia potassium.

3: Kuzuia Kikohozi na Baridi.

Tangu nanasi lina utajiri wa vitamin C linaweza kupigana na virusi amabavyo vinaweza kusababisha kikohozi na ubaridi. Hata kama umeshakuwa na kikohozi nanasi kwa kiasi flan linaweza kukusaidia kupunguza makali. Tunda hili lina madini ya Bromelain ambayo yanauwezo wa kudhoofisha virusi vya kikohozi. Wakati unaumwa kula tunda la nanasi hata wakati unakuwa kwenye dozi ya dawa ambazo umepewa na daktari linaweza kukusaidia sana kuharakisha kupona haraka.

4: Kuimarisha Mifupa.

Je unahisi mifupa yako sio imara? Basi anza kula nanasi. Nanasi pia lina uwezo wa kuimarisha mifupa nakuifanya kuwa yenye nguvu. Hii ni kwa sababu nanasi lina madini ya manganese ambayo mwili wako unahitaji madini haya ili kwa ajili ya kuimarisha mifupa yako. Tena kama ukinywa kikombe kimoja tu cha juice ya nanasi unakua umeongeza asilimia 73% ya madini ya manganese ambayo ni hata zaidi ya mwili unavyoihitaji kitu ambacho ni kizuri kwa afya ya mifupa ya mwili wako. Unakua na mifupa iliyokomaa.

5: Huimarisha Meno yako.

Watu kila mara huwa wanajali sana meno yao, na mara nyingine huwa wanashindwa kuyapa kipaumbele kwa saaana. Kama una matatizo ya meno basi unashauriwa kula nanasi kwa sababu nanasi linasaidia kuimarisha magego ambayo yanashikiria meno. Kula tunda la nanasi linakufanya kuimarisha magego yanayoshikiria meno na pia meno yenyewe yanaimarika.

6: Huzuia Ugonjwa wa Asthma.

Ukila nanasi unajiweka katika hali nzuri ya kuto pata ugonjwa wa asthma. Watu wanaokula nanasi wanakua katika hali nzuri kwa sababu nanasi lina vitamin aina ya Beta Carotene ambayo linausaidia mwili kukabiliana na magonjwa mbali mbali ikiwemo asthma.

7: Blood Pressure.
Unapokula nanasi unaongeza potassium na pia kula matunda mengine yenye madini ya potassium yanaweza kukusaidia kupunguza uwezekano wa kupata blood pressure.

8. Kansa.
Kama kawaida nanasi lina utajili mkubwa wa vitamin C. Hii vitamin C inauwezo wa kuzuia virusi ambavyo vinaweza kukusababishia magonjwa mabali mabli ya kansa.

9. Huimarisha Afya ya Moyo.

Utajiri wa madini ya fiber, potassium na vitamin C ni mojawapo ya faida za tunda hili ambazo pia zina uwezo wa kuimarisha afya ya moyo wako na kuzuia maradhi yanayoweza kuuadhiri moyo wako.

Sasa jamani tuanze kula tunda la nanasi ili tuweze kufaidi madini ya na vitamin zilizojaa katika tunda hili. ili kuepuka magonjwa ya baadaee. 

Endelea ku subscribe blog hii kwa Habari zaidi. >>>>>>>>

2 comments:

FEATURED POSTS

AFYA TIPS