Tuesday, August 22, 2017

SABABU ZA KUISHIWA NA KUKAUKIWA MAZIWA KWA MAMA ANAENYONYESHA

SABABU KUMI ZA KUISHIWA AU KUKAUKIWA MAZIWA KABISA KWA MAMA ANAYENYONYESHA

zifuatazo ni sababu

1.matumizi ya dawa za uzazi wa mpango; wanawake wengi hutumia njia hizi baada ya kujifungua bila shida yeyote lakini kuna baadhi yao njia hizi huingilia mfumo wao wa  kutoa maziwa hasa zikitumika kabla mtoto hajafikisha miezi sita. hii husababishwa na kuongezeka kwa homoni za uzazi yaani progesterone na oestrogen ambazo hushusha homoni ya kutoa maziwa yaani prolactin hormone.kama umekumbwa na hali hii basi acha mara moja njia hiyo na utumie njia zingine kama kondom,kalenda au njia nyingine isiyotumia dawa.

2.matatizo ya kimaumbile; baadhi ya wanawake matiti yao hayakukamilika wakati wamakua yaani yanakua na upungufu wa vitu muhimu vinavyohifadhi maziwa kwenye matiti kitaalamu kama grandular tissues hii hufanya maziwa yatoke kwa shida sana.mama anashauriwa akamue maziwa wakati wa kunyonyesha na mara nyingi mtoto wa pili mpaka watatu wakizaliwa matiti haya yanakua yameshazoea hivyo hayasumbui tena kutoa maziwa.

3.upasuaji wa matiti; kama mama ameshawahi kupasuliwa matiti yake kwa shida yeyote labda majipu, ajari, upasuaji wa kuongeza au kupunguza matiti basi kwa namna moja au nyingine hii inaweza kuharibu mfumo wake wa matiti kupitisha maziwa na kujikuta hatoi maziwa ya kutosha.ukiwa na shida hii utahitaji kutumia maziwa mbadala kwa mtoto.

4.matumizi ya dawa; wakati wa kunyonyesha mama anaweza kuugua na  kutumia dawa fulani fulani ili apone ugonjwa alionao lakini kuna  baadhi ya dawa ni hatari kwani hushusha kiwango cha maziwa. mfano dawa za kama bromocriptine,methergine,pseudoephredine.

5.matatizo ya homoni za uzazi; matatizo ya homoni kua juu sana au kua chini sana yanaweza kusababishwa na magonjwa ya ovari, kisukari na kadhalika. pia magonjwa yeyote ya homoni yanayochelewesha mtu kupata mimba huweza kuzuia maziwa pia. ni vizuri ukaonana na daktari kupima kiwango cha homoni na kupata matibabu.

6.kutonyonyesha usiku; wakati wa usiku homoni inayohusika na kutengeneza maziwa yaani prolactin hutengenezwa kwa kiwango cha juu sana lakini pia ili mtoto alale usiku mzima bila kusumbua lazima anyonye vizuri usiku.kutonyonyesha usiku hupunguza homoni hii na kumfanya mama atoe maziwa kidogo sana siku inayofuata.

7.kutonyonyesha vya kutosha; kawaida mama anatakiwa anyonyeshe angalau mara kumi ndani ya masaa 24, sasa mwili hutengeneza maziwa unapohisi matiti hayana kitu na kama mwili ukihisi matiti yana maziwa muda mwingi basi unajua maziwa hayahitajiki sana na kuanza kupunguza kiasi cha kutoa maziwa.

8.kutokula vizuri;maziwa anayotoa mama yanatengenezwa na chakula anachokula wala sio miujiza fulani hivyo kipindi hiki mama anatakiwa ale mlo kamili yaani matunda, protini ya kutosha, wanga, mboga za majan na maji mengi i na ikiwezekana atumie virutubisho vinavyotengenezwa maalumu kwa ajili ya kuongeza maziwa.

9.matumizi ya vyakula mbadala;  miezi sita baada ya kuzaliwa mtoto anatakiwa anyonye tu bila kupewa kitu chochote, kuna watu hua wanawapa maji wakidai eti watoto walisikia kiu sio kweli.sasa kuanza kumchanganyia maziwa ya ngombe na yale ya dukani kutamfanya anyonye kidogo kwako na mwili utapunguza kiasi cha maziwa yako...hivyo siku ukikosa mbadala utajikuta huna maziwa kabisa.

10.mtoto kushindwa kunyonya; kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba maziwa yakitoka mengi na mwili unatengeneza mengi zaidi na kama mtoto hanyonyi vizuri basi na maziwa hutoka kidogo zaidi.hali hii inaweza kusababishwa na dawa ya usingizi ambayo alipewa mama wakati wa kupasuliwa ambayo huamuathiri mtoto pia, au matatizo ya kuzaliwa nayo kama tongue tie[ulimi kushikwa chini ya mdomo, hii inaweza kurekebishwa na daktari] au mtoto kuugua.

Tuesday, August 15, 2017

FAIDA ZA MASSAGE KIAFYA

HII NDIYO TIBA KWA KUTUMIA MASAJI AMBAYO WENGI HAWAIFAHAMU

Wakati tunakabiliwa na mfadhaiko mkubwa kiakili na kimwili wa muda mrefu wengi wetu huwa tunatafuta msaada.

Hata hivyo moja ya tiba ya matatizo haya ambayo wengi hawaijuwi ni tiba kwa kutumia masaji, tiba ambayo ina uhakika wa uponyaji kwa karibu ya asilimia 100 bila kutumia dawa yoyote na bila madhara yoyote.

Masaji ni njia nzuri sana ya kuondoa stress na kupigana na maradhi mengi mwilini ukitumia nguvu ya mwili wenyewe kujitibu bila dawa yoyote zaidi ya mazoezi maalumu kwa kutumia mikono.

Shuhudia faida na uponyaji kupitia masaji kutoka katika kuongeza kinga ya mwili, kuondoa tatizo la kukosa usingizi, kupona baridi yabisi (stroke), kifafa na magonjwa mengine mengi yahusianayo na mishipa.

Masaji ni tiba inayofanywa kwa kutumia mikono tu huku mtoa masaji akikugusagusa na kukusugua juu ya mwili wako kwa namna maalumu ambayo ndiyo huamsha na kufungua mishipa na kuondoa sumu na stress mbalimbali na hivyo kuongeza kinga ya mwili kupambana na maradhi mbalimbali bila kutumia dawa yoyote.

Ni tiba maarufu kidogo maeneo ya mijini kuliko vijijini.

Pia ni huduma inayopatikana kwenye mahoteli makubwa ya kifahari Dar Es Salaam na Zanzibar wenyewe huita SPA’s ingawa hizo za kwenye mahoteli lengo kubwa huwa ni kwa ajili ya kukufanya u-relax na kupata utulivu baada ya uchovu wa shughuli za kila siku.

Hii masaji ya tiba (physiotherapy message) ni masaji maalumu kwa ajili ya wagonjwa.

Unaweza kujitibu hali hizi 6 zifuatazo kwa kutumia masaji tu:

1. Kuongeza kinga ya mwili

Kufanya masaji hakukufanyi ujisikie ni mtulivu peke yake, bali pia kunaweza kukuongezea kinga yako ya mwili.

Masaji ya dakika 45 kwa siku imethibitika kuongeza uwingi wa seli nyeupe za damu (lymphocytes) ambazo ndizo hupigana dhidi ya vijidudu nyemelezi vya magonjwa mbalimbali mwilini.

Faida nyingine za kiafya ni pamoja na kushuka kwa homoni inayohusika na kupunguza maambukizi mbalimbali homoni ijulikanayo kama ‘cytokines’ vile vile masaji inashusha homoni inayohusika na matendo ya mashari homoni ijulikanayo kama ‘cortisol’.

Kipindi kimoja cha masaji kinatosha kuzalisha matokeo yanayoonekana ya kuongezeka kwa kinga ya mwili.

2. Kuondoa tatizo la kukosa usingizi

Mamia ya watu wanapatwa na tatizo hili la kukosa usingizi jambo linaloharibu ufanisi wa kazi zao kila siku.

Tatizo la kukosa usingizi linaweza kutibika kwa kufanya masaji tu kwakuwa masaji husaidia kupunguza uchovu na kuongeza uwezo wa kupata usingizi mtulivu kwa watu wa rika zote yaani watoto wadogo mpaka wazee ikihusisha wale wenye matatizo ya akili, kansa na magonjwa ya moyo, machache kati ya magonjwa mengi yawezayo kutibika kwa masaji tu.

Tafiti nyingi zinasema masaji inao uwezo wa kuamsha mawimbi ndani ya ubongo yanayohusiana na kutengenezwa kwa usingizi mzito (delta waves) na hii ndiyo sababu kwanini wengine hupitiwa na usingizi mzito mara tu baada ya mazoezi ya masaji.

3. Kuondoa mfadhaiko wa akili  (Stress)

Zaidi ya asilimia 32 ya watu waliojaribu tiba hii wanathibitisha kupungukiwa na kiasi kikubwa cha mfadhaiko wa akili katika miili yao huku tafiti zaidi zikiendelea kutoa ushuhuda wa aina moja.

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Afya cha chuo kikuu cha Harvard umethibitisha kuwa masaji huondoa hamaki na maumivu huku yakiongeza uwezo wa kupata usingizi mzuri na wa uhakika.

Chuo kikuu cha afya cha Boston Uingereza kiliona matokeo yaliyo sawa kati ya wagonjwa 60 wenye kansa ambao walifanya tiba ya masaji dakika 20 kabla ya mionzi kuliwapunguzia kiwango cha hamaki na mfadhaiko wa akili.

Watafiti kutoka Australia wameripoti kwenye jarida la afya liitwalo ‘The Journal of Thoracic and Cardiovascular Surgery’  kuwa masaji hupunguza maumivu, hamaki na mshtuko wa mishipa baada ya upasuwaji wa moyo.

Utafiti mwingine kutoka chuo kikuu cha Toho cha Japan umethibitisha masaji inayohusisha mafuta maalumu ambayo huwa na harufu ya kunukia (ya kuvutia) na ambayo ni dawa husaidia kupunguza mfadhaiko wa kisaikolojia katika wazee wagonjwa wanaotibiwa majumbani.

4. Kuondoa huzuni

Tafiti kutoka chuo cha afya cha Nashville’s Meharry Medical College wagonjwa 43 wa ukimwi walionyesha kuondokewa na hali zao za huzuni baada ya kufanya masaji ya mwili mzima kwa majuma matatu tu.

Profesa maarufu na mtafiti Russell Poland, Ph.D. ambaye ni Profesa wa magonjwa ya akili na sayansi ya akili amesema: “Wakati tunaanza huu utafiti hatukutegemea kuona matokeo mazuri kiasi hiki kwa tiba hii ya masaji. Sote tulibaki na mshangao tu’’.

Faida hizi zilirudiwa pia na chuo kikuu cha Los Angeles Calfornia Marekani ambapo watu 95 waliojitolea kwa utafiti wa tiba hii ya masaji walionyesha kuongezeka homoni ijulikanayo kama 'oxytocin' na kupungua kwa homoni nyingine iitwayo 'adrenocorticotropin'.

Oxytocin inahusika na matendo ya huruma, maono, upendo na ushirikiano wa kijamii. Wakati adrenocorticotropin yenyewe huhusika na kupungua kwa mfadhaiko (stress) moja kwa moja.

5. Kuondoa maumivu mbalimbali mwilini

Watafiti kutoka kitengo cha jinakolojia (uuguzi) cha chuo kikuu cha Sao Paulo Brazil walitafiti wanawake 46 wajawazito waliofanyiwa masaji ya mgongo walipunguza kiasi cha maumivu wakiwa leba kwa zaidi ya asilimiaa 27.

Katika utafiti mwingine uliofanyika hospitali kuu ya Beijing nchini China masaji nzito ilisaidia kuondoa maumivu ya mgongo kwa wagonjwa. Kupungua kwa maumivu haya kuliripotiwa na robo tatu kati ya wagonjwa 110 waliofanyiwa utafiti huo.

Maumivu mengine yaliyoripotiwa kuondoka kwa kutumia tiba ya masaji ni pamoja na maumivu ya kichwa na maumivu ya kwenye mishipa.

6. Kuongeza uwezo wa kujiamini

Watu wengi zaidi kila kukicha wanaendelea kuitafuta huduma hii ya tiba kwa njia ya masaji wakiwa na maradhi mabalimbali katika miili yao. Madaktari wengi nao wameendelea kuwashauri wagonjwa wao kujaribu tiba hii.

Utafiti unaendelea kuwaeleimisha watoa tiba hii jinsi ya kuifanya ili kupata matokeo mazuri katika kutibu matatizo kama maumivu sugu ya misuli, matatizo yanayotokea wakati wa matibabu ya kansa, wakati wa mabadiliko yaletwayo na ujauzito, na maradhi mengine mengi.

Matatizo mengine yanayoweza kutibika kwa kutumia masaji ni pamoja na saratani ya matiti, tatizo la kufunga choo, ukichaa, maumivu, maumivu ya kichwa, maumivu ya mifupa, baridi yabisi (stroke) nk.

Bila shaka mpaka hapo umepata kuzijuwa faida za masaji na magonjwa inayoweza kuyatibu.



Tafadhali SHARE kwa ajili ya uwapendao.

Wednesday, August 9, 2017

FAIDA THELATHINI NA TISA(39) ZA MAFUTA YA NAZI KWA AFYA YAKO

 FAIDA 39 ZITAKAZOKUSHANGAZA ZA MAFUTA YA NAZI KIAFYA

Zaidi ya tafiti 1500 zimethibitisha kuwa mafuta ya nazi ndiyo mafuta bora zaidi chini ya jua. Hili halishangazi sababu karibu kila mtu anajua mafuta ya nazi ni dhahabu kwa afya ya mwili na ngozi kwa ujumla.

Bidhaa nyingi za vipodozi ukizichunguza utagundua huongezwa pia mafuta ya nazi ndani yake. Ili upate faida hasa za mafuta haya ni lazima yawe ni ya asili na hayajachanganywa na kingine au kemikali yoyote na yakiwa hivyo hujulikana kama mafuta bikra ya nazi (Virgin Coconut Oil).

Nyingi ya faida za mafuta ya nazi ni matokeo ya kuwa na asidi mafuta mhimu sana ijulikanayo kama ‘lauric’. Lauric ni asidi mafuta mhimu ambayo ni mdhibiti mzuri dhidi ya bakteria, fangasi, sumu, vijidudu nyemelezi na maambukizi.

Ili kupata faida hizi nyingi za mafuta ya nazi unaweza kuyanywa au kupakaa juu ya ngozi.

Mafuta ya nazi ni moja ya chanzo cha viinilishe mhimu sana mhimu na hivyo kufanya moja ya dawa mbadala mhimu kuwa nayo.

Mafuta ya nazi yanaweza kutumika kuongeza kinga ya mwili, kuzuia matatizo kwenye mfumo wa upumuwaji, kuponya matatizo katika figo, kutibu shinikizo la chini la damu, kupunguza hatari ya kisukari nk

Matumizi ya mara kwa mara ya mafuta ya nazi yanaweza kuongeza umeng’enywaji wa asidi amino, madini, vitamini mhimu na hivyo matumizi yake yanaweza kuboresha muonekano wako kwa ujumla.

Ndiyo maana siyo jambo la kushangaza kuona bidhaa nyingi kama vipodozi, sabuni na zile dawa za nywele ndani yake zikiongezwa mafuta ya nazi pia.

Kuna faida nyingi za kushangaza katika mafuta ya nazi kwa ajili ya afya na urembo ambazo ninapenda kukuonyesha kupitia makala hii.

Faida 39 zitakazokushangaza za mafuta ya Nazi kiafya

1. Huzuia na kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu

Wakati mafuta ya nazi yakiwa yamemeng’enywa na mwili huhamasisha uundwaji wa nguvu mpya za ubongo zijulikanazo kama ‘ketones’.

Ketones zina uwezo wa kusambaza nguvu katika ubongo hata kama insulin itakuwa chini ya kiwango kama matokeo ya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Insulin kazi yake kubwa ni kuishughulikia sukari (glucose) na hivyo kuzipa nguvu seli za ubongo.

Kwa bahati mbaya ubongo wa mtu mwenye ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu hauwezi kujitengenezea insulin yake kwa usahihi na vya kutosha.

Watu wanaosumbuliwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu wanatakiwa waongeze matumizi ya mafuta ya nazi kwenye vyakula vyao kila siku.

Kutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu ni moja ya kazi za mafuta ya nazi ambayo ninapenda kukufahamisha kupitia makala hii.

2. Huzuia uwezekano wa kupata kansa

Mafuta ya nazi yanao uwezo wa kupigana na seli za kansa. Tafiti za karibuni zinasema kitu chochote chenye uwezo wa kuuongezea nguvu ubongo husaidia pia kuzuia kusambaa kwa seli za kansa katika mwili.

Zaidi ni kuwa mafuta haya yana uwezo wa kumdhibiti bakteria ajulikanaye kama “helicobacter pylori” ambaye husababisha vidonda vya tumbo.

3. Yanaongeza kinga ya mwili mara dufu

Kinga imara ya mwili ina umhimu mkubwa katika kupigana na aina mbalimbali za magonjwa. Kuongeza kinga ya mwili ni moja ya faida za mafuta ya nazi sababu ni mafuta ambayo hupigana dhidi ya bakteria, fangasi na virusi mbalimbali.

Unaweza kupakaa moja kwa moja juu ya ngozi au kuyanywa pia kuchanganya kwenye vyakula mbalimbali kwa ajili ya kuongeza kinga yako ya mwili.

4. Yanaongeza nguvu za ubongo

Utafiti mmoja uliofanywa mwaka 2004 unaonyesha mafuta ya nazi yana uwezo wa kuongeza nguvu za ubongo hata kwa watu wenye umri mkubwa na wazee.

Mafuta ya nazi yana asidi mafuta nzuri zenye uwezo wa kusaidia na kuzilinda seli za ubongo na kuziwezesha kufanya kazi kwa ufasaha zaidi.

5. Yanaongeza nguvu na uvumilivu

Mafuta ya nazi yana uwezo wa kukupa nguvu na kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, moja ya kazi mhimu zaidi ya mafuta haya.

Mafuta ya nazi yanajulikana vizuri kwa uwezo wake wa kukuongezea uvumilivu. Hii ndiyo sababu wakimbia mbio wengi hupendelea kutumia mafuta ya nazi.

Changanya kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya nazi na kijiko kidogo kingine cha asali mbichi na unywe pamoja mchanganyiko huu kila siku kutwa mara 1 kabla ya kwenda kwenye mazoezi au kwenye kazi yoyote ngumu.

6. Dawa nzuri kwa matatizo ya mifupa

Ugonjwa wa mifupa husababishwa na vijidudu nyemelezi na mfadhaiko wa mwili wa muda mrefu.

Mafuta ya nazi yana viondoa sumu vyenye nguvu zaidi ambavyo vinaweza kuulinda mwili wako dhidi ya vijidudu nyemelezi.

Zaidi, matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kurahisisha umeng’enywaji wa madini ya kalsiamu tumboni mwako.

Upungufu wa madini ya kalsiamu mwilini husababisha mifupa kuwa hafifu jambo linaloishia kuleta ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).

Kuzuia ugonjwa wa mifupa unahitaji kuongeza mafuta ya nazi kuwa sehemu ya chakula chako. Hii ndiyo faida ya mafuta ya nazi ambayo niliona si vema kama sitakuambia.

7. Husaidia kushusha uzito

Watu wengi wanaamini kwamba ili kupungua uzito basi hutakiwi kabisa kutumia mafuta. Hata hivyo hili si jambo la kweli. Kupunguza uzito ni moja ya kazi nyingine nzuri sana ya mafuta ya nazi.

Matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kusaidia mafuta kuchomwa zaidi mwilini huku kiasi chako cha njaa kikishuka.

Watu wenye vitambi au unene uliozidi wanatakiwa kuongeza mafuta ya nazi kwenye milo yao na miili yao itakaa sawa yenyewe.

8. Huondoa mfadhaiko (Stress)

Mifadhaiko ni jambo lisiloweza kuepukika katika maisha yetu. Kazi ya mfadhaiko au stress ni kukufanya uwe imara zaidi, mpole na unayejiamini zaidi.

Unapofadhaishwa mwili wako huwa unajiongeza na kuwa na shauku ya kufanikiwa zaidi. Hata hivyo mfadhaiko unapodumu kwa muda mrefu unaweza kuleta madhara makubwa kwa mhusika kihisia na hata kimwili pia.

Mfadhaiko wa muda mrefu unaweza kupelekea huzuni mbaya na hatimaye kuathiri muonekano wako.

Watu wenye mifadhaiko (stress) ya muda mrefu huonekana ni wenye umri mkubwa hata kama umri wao bado ni mdogo.

Tafiti za karibuni zimeonyesha uhusiano wa karibu uliopo kati ya matumizi ya mafuta ya nazi na kupungua kwa mfadhaiko wa akili.

Tunaweza kusema kuwa, kitendo hiki cha kuondoa mfadhaiko au stress ni moja ya kazi ya kustajaabisha kabisa ya mafuta ya nazi. Asidi mafuta zilizomo ndani ya mafuta haya ndizo zinazohusika na kazi hii mhimu.

9. Huimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Ili mwili wako ubaki ni wenye afya na kuzuia usipatwe na magonjwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula na wakati huo huo mfumo imara wa uchukuwaji wa viinilishe, madini na vitamini mbalimbali kutoka kwenye chakula unachokula.

Kwa bahati nzuri, kuuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula ni kazi nyingine ambayo mafuta ya nazi yanaweza kukusaidia bila madhara mengine mabaya.

Matumizi ya mafuta ya nazi yatakuwezesha kuongeza uchukuwaji wa viinilishe mhimu kutoka kwenye chakula sababu mafuta haya yana madini ambayo huweza kuyeyuka kwenye mafuta kama kalsiamu na magnesiamu.

Zaidi, mafuta haya yanaweza kusaidia umeng’enywaji wa mafuta mengine magumu ndani ya mwili kama matokeo ya kuimarishwa kwa vimeng’enya vinavyohusiana na mmeng’enyo wa chakula.

10. Jitibu matatizo katika Kongosho na Kibofu cha mkojo

Kama unapata maumivu au matatizo yoyote katika kongosho au kibofu cha mkojo unahitaji kuongeza matumizi ya mafuta ya nazi.

Ukiendelea kutumia mafuta ya nazi kila mara utaweza kujitibu pia tatizo la mawe katika kibofu cha mkojo na kuondoa hali ya kutojisikia vizuri kutokana na magonjwa katika kongosho au kibofu cha mkojo.

11. Yanatengeneza Misuli ya mwili

Faida kubwa ya mafuta ya nazi haiishii katika uwezo wake wa kuchoma mafuta, bali yana kazi nyingine ya kushangaza zaidi nayo ni kutengeneza misuli ya mwili.

Kwenye bidhaa nyingi zinazouzwa zaidi duniani za kutengeneza virutubishi vya kutengeneza misuli ya mwili mafuta ya nazi lazima yawemo.

Kama unataka kuongeza misuli mingi mwilini kirahisi zaidi changanya tui zito la nazi kikombe kimoja (robo lita), ongeza vanilla vijiko vikubwa vitatu, ongeza maji maji ya chungwa vijiko vikuwa viwili na ndizi zilizoiva mbili.

Saga na mashine ya kusagia matunda jikoni (blender) mchanganyiko huu kwa pamoja na ule wote kutwa mara 1 kila siku.

12. Zuia jino kuoza na magonjwa ya kwenye fizi

Kuzuia kuoza kwa jino na magonjwa ya fizi ni moja ya kazi nyingine nzuri ya kushangaza ya mafuta ya nazi ambayo nimependa kukufahamisha kupitia makala hii.

Mafuta ya nazi ni dawa inayoweza kudhibiti bakteria wabaya na hivyo kuzuia kuoza kwa jino na maumivu mengine katika fizi. Ili kuzuia haya unahitaji tu kutumia mafuta yako ya nazi kama dawa yako ya mswaki kila siku.

Unaweza pia kuongeza kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto ili kutengeneza dawa ya kusafisha mdomo (mouthwash).

13. Ongeza ufanisi wa Ini na Figo

Kwa mjibu wa madaktari wengi, kuna uhusiano wa karibu kati ya madhara ya figo na kushindwa kufanya kazi kwa ogani hii mhimu.

Kama tatizo la kufeli kwa figo halitapatiwa ufumbuzi linaweza kupelekea kifo. Figo na Ini ni ogani mhimu zaidi katika mwili ambazo zinatakiwa kupewa uangalizi wa karibu kila mara zisipatwe na madhara yoyote.

Kwa bahati nzuri, mafuta ya nazi yanayo uwezo wa kulinda figo na Ini visipatwe na madhara yoyote mabaya moja ya kazi ya mafuta ya nazi mwilini ulikuwa huijuwi bado.

Wanasayansi wameviona viinilishe katika mafuta ya nazi ambavyo ni mhimu sana kwa afya ya Ini na figo katika mwili wa binadamu.

14. Yanaondoa mawe katika figo na kibofu cha mkojo

Nazi pamoja na mafuta ya nazi huwa na asidi mafuta mhimu sana ambazo huhamasisha uundwaji wa ‘Monooctanoin’ ambayo hufanya kazi ya kuyeyusha mawe katika kibofu cha mkojo na figo.

Wagonjwa ambao hawawezi kumudu gharama za upasuwaji kuondoa mawe katika figo na katika kibofu cha mkojo wanaweza kujitibu hilo kwa kutumia mafuta ya nazi kama dawa mbadala.

Unachohitaji kufanya ni kunywa tu kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi kila siku kutwa mara 1 mpaka utakapokuwa umepona.

15. Yanatibu baridi yabisi

Mafuta ya nazi hudhibiti uvimbe na kuondoa sumu mwilini, kazi hizi mbili zinayafanya kuwa dawa bora ya kutibu ugonjwa wa baridi yabisi.

Unahitaji kijiko kidogo kimoja cha mafuta haya kila siku ili kujitibu na ugonjwa wa baridi yabisi.

16. Husaidia kazi za tezi koromeo (Thyroid gland)

Faida za mafuta ya nazi zinahusu pia kurekebisha kazi za ogani za mwili kama kuweka sawa mapigo ya moyo, kupumua na kuzalisha homoni mhimu.

Tezi koromeo huzalisha homoni mbili ambazo huwa na msaada mkubwa katika kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Ufanisi mzuri wa tezi hii huweza kuhakikisha mapigo ya moyo ni sawa, uzito sawa wa mwili, na usawa ulio sawa wa homoni.

17. Yanatibu kisukari aina ya kwanza

Kutibu kisukari aina ya kwanza ni moja ya kazi nyingine nzuri za mafuta ya nazi sababu mafuta haya yanao uwezo wa kuiweka sawa damu sukari (blood glucose) ndani ya mwili.

Mafuta ya nazi yamethibitika siyo katika kushusha kisukari aina ya kwanza tu bali pia katika kuweka sawa aina mbalimbali za homoni mwilini.

Kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi kwa siku kinatosha kwa kazi hii.

18. Hutibu maambukizi ya fangasi

Mafuta ya nazi ni moja ya dawa nyingine nzuri kwa ajili ya kutibu maambukizi ya fangasi kwa sababu moja kuu kwamba ni mafuta yanayoweza kuua bakteria na virusi mbalimbali.

Hii ni kazi ya mafuta haya ambayo isingekuwa vema kama nisingekujulisha kupitia makala hii. Hii ni matokeo ya kuwa na ‘lauric acid’ na ‘capric acid’.

Tafiti mbalimbali zimeonyesha uhusiano uliopo baina ya matumizi ya mafuta yenye afya na kushuka kwa maambukizi ya fangasi.

Kwa fangasi yoyote juu ya ngozi unaweza kutumia mafuta haya kama mafuta yako ya kupakaa kila siku pia unaweza kunywa kijiko kidogo kimoja kila siku kuongeza kinga zaidi ya mwili.

19. Yanaweka sawa homoni zako.

Maradhi mengi mwilini huja kama sababu ya homoni zako kutokuwa sawa. Ni bahati kufahamu kuwa mafuta ya nazi ni moja ya dawa za asili nzuri katika kuziweka sawa homoni zako.

Hii ni kwa sababu mafuta ya nazi yana mafuta mazuri yajulikanayo kama ‘lauric acid’. Mafuta ya nazi huiweka sawa homoni mhimu sana kwa upande wa uzazi kwa mwanamke homoni ijulikanayo kama ‘estrogen’. Chanzo kingine kizuri cha homoni hii ni pamoja na tunda la parachichi.

20. Yatakufanya usizeeke mapema

Kuzeeka mapema ni jambo lisilopendwa karibu na watu wote. Kuzeeka mapema hakuathiri muonekano wako tu bali huathiri pia afya yako.

Tunapozungumzia juu ya faida za kushangaza zilizomo katika mafuta ya nazi lazima ujuwe kuwa mojawapo ni hili la kukufanya usizeeke mapema.

Viuajivijasumu vilivyomo kwenye mafuta ya nazi hufanya kazi mhimu katika kupunguza vijidudu nyemelezi na matatizo mengine katika ini.

21. Hupunguza maradhi ya ubongo

Kuzuia magonjwa ya ubongo ni faida nyingine ya mafuta ya nazi ambayo unapaswa kuijua.

Asidi mafuta zilizomo kwenye mafuta ya nazi hubadilishwa na kuwa ‘ketones’ ambazo huzuia kutokea tatizo la kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Kupoteza kumbukumbu ni matokeo ya kuongezeka kwa kemikali ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘amyloid beta peptides’.

Kwenye mafuta ya nazi kuna kitu mhimu sana kijulikanacho kama ‘Phenolic compounds’ ambacho hudhibiti ile kemikali ya ‘amyloid beta peptides’ na hivyo kukuondolea tatizo la kupoteza kumbukumbu kirahisi zaidi.

22. Hupunguza njaa

Mafuta ya nazi yanaweza kukupunguzia hitaji lako la kutaka kula chakula kila mara kwa kuwa hufanya kazi ya kupunguza njaa ndani ya mwili.

Kutumia mafuta ya nazi kutakufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu na kama matokeo yake kutakusaidia kupunguza kiasi cha nishati unaingiza ndani ya mwili wako kila siku.

Kuna uhusiano wa karibu kati ya mafuta safi kwa afya na kuwa na njaa ya wastani.

23. Yanapunguza uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa moyo

Tafiti mbalimbali Zimeonyesha kwamba Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto (high-density lipoproteins -HDL) unao uwezo wa kulinda moyo wako.

Hivyo mafuta ya nazi yanaweza kupunguza hatari kwako ya kupatwa na ugonjwa wa moyo moja ya kazi nyingine mhimu sana ya mafuta haya.

Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla.

Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.

24. Yanauongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Tafiti zimeendelea kuonyesha uhusiano uliopo kati ya matumizi ya mafuta ya nazi na kuimarika kwa mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula.

Mafuta ya nazi yanapokuwa yamemeng’enywa ndani ya mwili wako hutumika kama nguvu yako moja kwa moja.

Watu wanaotumia mara kwa mara mafuta ya nazi kwenye vyakula vyao kila siku wanakuwa na mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula jambo ambalo ni mhimu katika kuchoma mafuta na nishati ndani ya mwili.

25. Yanapigana kuondoa vijidudu nyemelezi

Maisha yetu ya kila siku yanapelekea kuundwa kwa vijidudu nyemelezi ndani ya mwili bila sisi kupenda.

Kuzidi kujitokeza kwa vijidudu nyemelezi ndani ya mwili ndiyo kunakopelekea mwili kuwa ni wa kuchokachoka kila mara na ni chanzo cha magonjwa mengine mengi.

Kuendelea kutumia mafuta ya nazi kutasaidia kuimarisha kinga yako ya mwili kwani mafuta ya nazi yana kiasi cha kutosha cha viuajivijasumu (antioxidants) dhidi ya vijidudu mbalimbali nyemelezi.

26. Yanaotesha nywele

Faida za mafuta ya nazi haziishii ndani ya mwili tu, bali yana faida nyingine nyingi yanapotumika nje ya mwili.

Tafiti zimeonyesha kwamba matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kuwa msaada mkubwa katika kuotesha na kukuza nywele.

Tafiti zimeonyesha kwamba matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kuzuia aina yoyote ya upotevu wa nywele.

Kupungua kwa protini kunaweza kuwa ni sababu nyingine ya kupotea kwa nywele zako kama hakutadhibitiwa kwa haraka.

Unachohitaji ni kuyafanya kuwa mafuta yako ya nywele na hutachelewa kuwa na nywele nzuri zinazopendeza. Mafuta ya nazi ni mlinzi mzuri wa nywele zako.

27. Yanaondoa mba kichwani

Unasumbuliwa na mba kichwani? Pakaa mafuta ya nazi na mba utapotea bila kupenda wenyewe.

Mafuta ya nazi ni moja ya dawa mbadala zenye nguvu kutibu tatizo la mba. Dawa nyingi na vipodozi vya kuondoa mba kichwani huongezwa mafuta ya nazi ndani yake.

Tuliona pia pale juu kuwa hutumika kuotesha nywele.

Unahohitaji ni kufanya ni kuamua mafuta ya nazi kuwa ndiyo mafuta yako ya kupakaa kichwani na mba utapotea wenyewe kadri unavyoendelea kuyatumia.

28. Mafuta bora zaidi kwa ngozi yako

Mafuta pekee mazuri kwa ngozi yako ni mafuta ya nazi. Hii ndiyo sababu dawa nyingi na vipodozi vya ngozi ndani yake huwa na mafuta ya nazi pia.

Kama una ngozi kavu au yenye mikunjokunjo basi pakaa mafuta ya nazi na ngozi yako itakuwa nzuri, nyororo, yenye rangi yake ya asili na ya kupendeza sana. Waulize watu wa ukanda wa pwani hili wanalifahamu vizuri sana.

Kama utaamua kutumia mafuta ya nazi kama mafuta yako ya kupakaa magonjwa mengi ya ngozi utayasikia tu kwa jirani.

29. Yanalinda ngozi yako dhidi ya miale ya jua

Viinilishe vya asili kwenye mafuta ya nazi vinawezesha ngozi yako isiathirike na miale ya jua moja kwa moja. Moja ya kazi nyingine ya kushangaza ya mafuta haya.

Mafuta ya nazi ni miwani ya jua ya asili. Kwa mjibu wa utafiti, mafuta ya nazi yanaweza kuzuia mpaka asilimia 20 ya miale ya jua kushindwa kukufikia moja kwa moja kwenye ngozi yako kama utayafanya kuwa ndiyo mafuta yako ya kupakaa.

Tafiti nyingi zimeonyesha miale ya jua kuwa ina athari nyingi ikitua moja kwa moja juu ya ngozi yako ikiwemo kufanya ngozi kuwa na makunyanzi, magonjwa ya ngozi na kansa ya ngozi.

30. Dawa nzuri ya kusugulia mwili (Scrub)

Wengi mnapenda kufanya scrub hasa usoni (facial). Kwa lugha nyepesi ni kitendo cha kusugua ngozi kwa dawa maalumu ili kuondoa uchafu wote na kuifanya ionekane nyororo na yenye kupendeza.

Sasa huhitaji dawa zenye kemikali kwa ajili hiyo wakati mafuta ya nazi yanaweza kukusaidia hilo bila madhara yoyote mabaya.

Fanya hivi changanya nusu kikombe (mln125) cha mafuta ya nazi na sukari kikombe kimoja na ufanye dawa ya kusugua na kusafisha uso wako.

Unaweza pia kutumia nazi yenyewe moja kwa moja kabla hujapata mafuta yake.

Tumezoea kutumia nazi jikoni kwenye mapishi, lakini nazi pia inaweza kutumika kama scrub ya asili ya ngozi yako.

Fuata hatua hizi zifuatazo ili kufanya ngozi ya uso wako iwe laini, nyororo na kufanya uso wako uwe laini, nyororo na wenye mvuto.

Scrub hii unaweza pia kuitumia kwa mwili mzima, lakini hapa nitaelezea namna ya kutumia kwa uso wako.

* Andaa nazi yako kwa kuikuna vizuri na ili upate matokeo mazuri jitahidi kuikuna taratibu ili itoke laini.
*Safisha uso wako kwa maji safi na sabuni ya kawaida isiwe sabuni ya dawa (medicated)
* Kausha uso wako kwa taulo safi.
* Baada ya uso wako kuwa mkavu, ichukue ile nazi yako uliyoikuna tayari, taratibu anza kusugua usoni kwa dakika kama 3 mpaka 5.
*Ukishamaliza hapo, utakaa hivyo bila kuuosha uso wako kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.
* Baada ya muda huo, utaosha uso wako kwa sabuni ya kawaida.
* Kausha uso wako kwa taulo safi, kisha paka losheni yako unayotumia siku zote.

Ili kupata matokeo mazuri fanya hivi kwa muda wa siku 5 mfululizo bila kuacha, yaani mara moja kwa siku.

Amini nakuambia utapata matokeo mazuri mpaka mwenyewe utaifurahia ngozi yako na hata vocha utaninunulia kunipongeza.

31. Yanatibu vidonda vya homa mdomoni

Mafuta ya nazi ni moja ya dawa nzuri kabisa kutibu vidonda vya homa ambavyo hujitokeza mdomoni.

Unahitaji kupakaa tu sehemu yenye tatizo moja kwa moja huku ukinywa kijiko kidogo kimoja kila siku na hutakawia kupona hivyo vidonda.

Hili linawezekana kutokana na sifa ile ile ya mafuta haya katika kupigana dhidi ya bakteria na virusi na vijidudu nyemelezi.

32. Yanaimarisha kucha

Ukitumia mafuta ya nazi utakuwa na kucha nzuri na zenye kupendeza.

Wakati huo huo kunyunyiza mafuta ya nazi kwenye kucha zako kunaua wadudu wowote wanaoweza kuharibu kucha zako.

33. Hufukuza wadudu mbali

Yanaweza kutumika kama dawa ya asili ya kufukuza wadudu (insect repellent) wakiwemo mbu. Unachohitaji ni kuchanganya pamoja na kiasi kidogo cha mafuta ya karafuu au ya mnanaa (mint) na ujipake juu ya ngozi yako na hakuna mdudu yoyote akiwemo mbu atakayekusogelea.

Pakaa mchanganyiko huu mara kadhaa katika siku kwa matokeo mazuri zaidi.

34. Mafuta mazuri kwa ajili ya Lips

Wasichana na wamama wengi ni watumiaji wa bidhaa nyingi za lipstiki zenye kemikali kwa ajili tu ya kulainisha midomo yao ya nje (lips). Kile wengi hawajuwi ni kuwa bidhaa hizi si salama sana kwa afya zao.

Bahati nzuri kwa wewe unayesoma makala hii mafuta ya nazi yanaweza kutumika kama lipstiki yako ya asili isiyo na madhara mabaya hapo baadaye.

Kwahiyo kama una tatizo la midomo kukauka basi uwe unapakaa mafuta ya asili ya nazi kila mara..

35. Ni mafuta mubadala ya kupikia yenye afya

Tofauti na mafuta ya alizeti au hata mafuta ya zeituni, kupika chakula kwa mafuta ya nazi ni zaidi ya afya.

Mafuta haya yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto.

Hii ni kwamba mafuta kama ya zeituni ambayo huweza kuliwa hata yakiwa mabichi lakini yanapochomwa katika moto basi ubora wake hupungua au kwa maneno mengine huzalisha taka sumu kama ilivyo kwa vitu vingi vinapounguzwa lakini hili halitokei kwa mafuta ya nazi!

36. Ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama

Siyo kupika tu na mafuta ya nazi ndiko huleta afya, bali pia ni mafuta mazuri kwa wasiopenda kutumia mafuta yatokanayo na wanyama kama mubadala kwa siagi au vitu vingine mnavyopaka juu ya mikate mnapokula.

Hii nikwa sababu mafuta ya nazi hubaki katika hali yake hata katika joto la kawaida la chumba tofauti na mafuta mengine.

37. Mafuta mazuri kwa ajili ya masaji

Mafuta ya nazi ni mafuta mazuri kwa ajili ya masaji na kukupatia hali ya utulivu unaouhitaji kupitia masaji.

Unaweza kuchanganya na mafuta mengine kama ya karafuu na kupata mchanganyiko wa mafuta maalumu kwa ajili ya masaji na ukiyatumia utaweza ku-relax kwa uzuri kabisa huku yakituliza mishipa, misuli, ubongo na mwili wako kwa ujumla.

38. Hutumika kulainisha uke mkavu

Mafuta ya nazi yana matumizi mengi sana mwilini zaidi ya 100, kuna wanawake wana tatizo la kuwa na uke mkavu muda wote hata wakisisimuliwa vipi bado huwa wakavu.

Kuondokana na tatizo hilo pakaa mafuta ya nazi katika uke wako na utaona faida yake nyingine ikiwemo ya kutibu, fangasi na bakteria tena bila madhara yeyote mabaya.

39. Husaidia katika ugonjwa wa aleji

Tukisema tuelezee faida zote za mafuta ya nazi kwa hakika hatutaweza.

Moja ya faida zake zinazoshangaza wengi ni uwezo wa kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji. Kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na uone kama utapiga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.





Hakikisha unapata mafuta ya nazi ambayo ni ya asili kwa asilimia 100, ikiwa utanunua dukani kuna uwezekano mkubwa yakawa yamechanganywa na kemikali zingine au haidrogeni kitu kinachoyapunguzia thamani yake ile ya asili.

Kama unapikia kwenye chakula najuwa wengi mnapenda wali wa nazi au hata tui lake likiwekwa kwenye samaki au hata mboga yoyote lazima utajing’ata ulimi, basi nakushauri usichanganye na mafuta mengine kwenye hicho chakula.

Yanauzwa gharama? Unaweza kutengeneza wewe mwenyewe nyumbani, fuata hatua hizi zifuatazo:

1. Nunua nazi idadi utakayo
2. Pasua nazi na ukune na mbuzi
3. Chukua nazi uliyopata isage na maji kiasi kidogo kwenye blenda na ukamue upate tui Zito jingi
4. Chukua hilo tui weka kwenye chombo kisafi kikubwa au hata kwenye sufuria, funika na kitambaa (nguo yoyote Safi) na uache hivyo ipumzike kwa masaa 24
5. Kesho yake utaona maji yamebaki Chini na juu kuna layer kubwa ya tui lililoganda, chukua tui hilo la juu lililoganda na uweke kwenye sufuria nzito, weka kwenye moto kama dakika 6 hivi tayari umepata mafuta ya nazi.

Hakikisha yasiunguwe, chuja endelea kutumia mafuta yako.

Tafadhali SHARE kwa ajili ya uwapendao



Tuesday, August 8, 2017

FAIDA ZA JUISI YA UBUYU

 MAAJABU YA JUISI YA UBUYU

Mungu ameumba miti na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi.

Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.

Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa.

1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.

2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya kalsiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!

3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini

4. Ina virutubisho vya kulinda mwili

5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili wa binadamu huwa na vitamin B2.
6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
7. Huongeza nuru ya macho
8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
9.  Unga wa ubuyu una magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

Unywe kiasi gani? Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.

Ili upate faida za juisi ya ubuyu, zinazoelezwa hapa, lazima upate ule ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.

Namna ya kuandaa hii juisi: Chukuwa unga wa ubuyu vijiko vikubwa vitatu, weka kwenye kikombe, ongeza maji robo lita na ukoroge vizuri, unaweza kuongeza sukari au asali kidogo kupata radha, tikisa na unywe.


Saturday, August 5, 2017

FAIDA ZA ASALI NA MDALASINI

KAMA ULIPITWA NA MAKALA YA FAIDA ZA ASALI NA MDALASINI BASI SOMA HAPA


1. Asali ikichanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.

2. Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini.

3. Asali inatajwa pia kuwa dawa ya jino, inaponya pia ngozi iliyoharibika, ni dawa asilia ya shinikizo la juu la damu na kiungo muhimu katika utengenezaji wa asilimia kubwa ya madawa mmimiko na asilimia kubwa ya vipodozi na mafuta ya kupaka.

4. Ugonjwa wa mafua(wengine huita ugonjwa wa mapenzi) ambao huwakera na kuwanyima watu wengi raha unaweza kupungua na kupotea kabisa ikiwa utatumia kijiko kimoja cha chai cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko cha chai cha mdalasini. Mchanganyiko huo pia ni mahususi katika kusaidia kupunguza na kuondoa chafya na kuvimba kwa koo.

5. Asali na mdalasini hutumika katika mwongozo wa tiba ya upungufu wa nguvu za kiume. Yaani huongeza hamu ya tendo la ndoa

6. Asali na mdalasini husaidia katika kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ukiwa katika kadhia hiyo, unashauriwa kuongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali kwenye chai ama maji.

7. Asali na mdalasini husaidia kupunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.

8. Ulaji wa asali pamoja na mdalasini husaidia kuondoa mchafuko wa tumbo uletwao na gesi.

9. Matumizi ya mara kwa mara ya asali na mdalasini wakati wa kifungua kinywa husaidia kuzuia uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo pamoja na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu.

10. Kula mkate uliopakwa asali kijiko kimoja cha mezani kila siku  ni muhimu pia kiafya kwani hupunguza uwezekano wa kutokea kwa tatizo la kuziba kwa mishipa ya damu.

11. Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu yanaweza kutoweka kwa kutumia mara kwa mara asali iliyochanganywa na mdalasini.

12.Matumizi ya mara kwa mara ya asali na mdalasini husaidia kuimarika na kuongezeka kwa kinga ya mwili kutokana na asali  kuwa na hazina kubwa ya virutubisho na madini.

13. Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo, huondoa kiungulia.

14. Unywaji wa kila siku wa kikombe baridi cha chai iliyowekewa asali na mdalasini huimarisha afya bora na madhubuti kwa mtumiaji.

15. Asali ni tiba rafiki na asilia kwa watu wenye shida ya chunusi. Ili kutibu tatizo hilo changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja mdalasini na pakaa kwenye chunusi. Uwezo wa asali wa kuua bakteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili pekee.

16. Asali husaidia kuirudisha ngozi iliyoharibiwa na wadudu kama dondola na washawasha na hata ngozi iliyopata madhara kutokana na kuungua moto. Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati muwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi uvimbe unapotoweka.

17. Kwa mujibu wa tafiti za hivi karibuni zilizofanyika nchini Australia na Japan asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa anayetumia madawa ya kutibu saratani kwa kutumia kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi.

18. Upo ushahidi mpya kwamba sukari asilia zilizopo kwenye asali, zina uwezo wa kuongeza nishati mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu. Wataalamu wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji kisha nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi na kisha kunywa tena alasiri wakati nishati (nguvu) inapoanza kushuka.

19. Asali ina uwezo mkubwa wa kupunguza na kuponya miguu iliyopasuka kwenye kisigino. Chua asali na mdalasini vuguvugu katika miguu au nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu na kazi au baada ya mazoezi marefu. Rudia kila siku asubuhi halafu, osha nyayo zako kwenye maji baridi na vaa viatu.

20. Kusukutua maji ya vuguvugu yaliyowekwa asali na mdalasini kila asubuhi husaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni (halitosis) kutokana na uwezo wa asali kuua bakteria.

KUMBUKA: HIZO FAIDA UTAZIPATA ENDAPO UTATUMIA ASALI MBICHI PEKEE NA SIYO ASALI ILIYOCHEMSHWA




Wednesday, August 2, 2017

FAIDA KUMI NA TATU(13) ZA KULA TIKITI MAJI

 LIJARIBU TUNDA HILI UJIONEE HAYA MACHACHE...

Tunda hili lina faida nyingi pamoja na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuzi, Wanga,Calcium, Phosphorus, Chuma,Vitamin A,B6,C. Potasium, Magnesium, Carotene, anthocyanins na Virutubisho vingine vingi.

Tunda linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu.

Faida 13 za tikiti maji kiafya

• Asilimia 92 yake ni maji
• Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho
• Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili,
• Huponya majeraha,
• Hukinga uharibifu wa seli
• Huboresha afya ya meno na fizi
• Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema
• Hubadilisha protin kuwa nishati
• Chanzo cha madini ya potasiamu
• Husaidia kushusha na kuponya shinikizo la damu
• Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini
• Huondoa sumu mwilini
• Huongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanaume

NB: Tikiti halifai kutumika katika program ya kupunguza uzito/kitambi kutokana na kuwa na sukari nyingi japo ni sukari ya asili, lakini sisi tuna-discouraged sukari zote kwa tatizo la uzito.



Featured Post

FAIZA ZA KULA PAPAI

 _*Siri usioijua kuhusu utajiri wa tunda la papai katika kukulinda na magonjwa hatarishi kutokana na faida zake lukuki*_  Hizi ndizo FAIDA 1...