Powered By Blogger

Tuesday, August 15, 2017

FAIDA ZA MASSAGE KIAFYA

HII NDIYO TIBA KWA KUTUMIA MASAJI AMBAYO WENGI HAWAIFAHAMU

Wakati tunakabiliwa na mfadhaiko mkubwa kiakili na kimwili wa muda mrefu wengi wetu huwa tunatafuta msaada.

Hata hivyo moja ya tiba ya matatizo haya ambayo wengi hawaijuwi ni tiba kwa kutumia masaji, tiba ambayo ina uhakika wa uponyaji kwa karibu ya asilimia 100 bila kutumia dawa yoyote na bila madhara yoyote.

Masaji ni njia nzuri sana ya kuondoa stress na kupigana na maradhi mengi mwilini ukitumia nguvu ya mwili wenyewe kujitibu bila dawa yoyote zaidi ya mazoezi maalumu kwa kutumia mikono.

Shuhudia faida na uponyaji kupitia masaji kutoka katika kuongeza kinga ya mwili, kuondoa tatizo la kukosa usingizi, kupona baridi yabisi (stroke), kifafa na magonjwa mengine mengi yahusianayo na mishipa.

Masaji ni tiba inayofanywa kwa kutumia mikono tu huku mtoa masaji akikugusagusa na kukusugua juu ya mwili wako kwa namna maalumu ambayo ndiyo huamsha na kufungua mishipa na kuondoa sumu na stress mbalimbali na hivyo kuongeza kinga ya mwili kupambana na maradhi mbalimbali bila kutumia dawa yoyote.

Ni tiba maarufu kidogo maeneo ya mijini kuliko vijijini.

Pia ni huduma inayopatikana kwenye mahoteli makubwa ya kifahari Dar Es Salaam na Zanzibar wenyewe huita SPA’s ingawa hizo za kwenye mahoteli lengo kubwa huwa ni kwa ajili ya kukufanya u-relax na kupata utulivu baada ya uchovu wa shughuli za kila siku.

Hii masaji ya tiba (physiotherapy message) ni masaji maalumu kwa ajili ya wagonjwa.

Unaweza kujitibu hali hizi 6 zifuatazo kwa kutumia masaji tu:

1. Kuongeza kinga ya mwili

Kufanya masaji hakukufanyi ujisikie ni mtulivu peke yake, bali pia kunaweza kukuongezea kinga yako ya mwili.

Masaji ya dakika 45 kwa siku imethibitika kuongeza uwingi wa seli nyeupe za damu (lymphocytes) ambazo ndizo hupigana dhidi ya vijidudu nyemelezi vya magonjwa mbalimbali mwilini.

Faida nyingine za kiafya ni pamoja na kushuka kwa homoni inayohusika na kupunguza maambukizi mbalimbali homoni ijulikanayo kama ‘cytokines’ vile vile masaji inashusha homoni inayohusika na matendo ya mashari homoni ijulikanayo kama ‘cortisol’.

Kipindi kimoja cha masaji kinatosha kuzalisha matokeo yanayoonekana ya kuongezeka kwa kinga ya mwili.

2. Kuondoa tatizo la kukosa usingizi

Mamia ya watu wanapatwa na tatizo hili la kukosa usingizi jambo linaloharibu ufanisi wa kazi zao kila siku.

Tatizo la kukosa usingizi linaweza kutibika kwa kufanya masaji tu kwakuwa masaji husaidia kupunguza uchovu na kuongeza uwezo wa kupata usingizi mtulivu kwa watu wa rika zote yaani watoto wadogo mpaka wazee ikihusisha wale wenye matatizo ya akili, kansa na magonjwa ya moyo, machache kati ya magonjwa mengi yawezayo kutibika kwa masaji tu.

Tafiti nyingi zinasema masaji inao uwezo wa kuamsha mawimbi ndani ya ubongo yanayohusiana na kutengenezwa kwa usingizi mzito (delta waves) na hii ndiyo sababu kwanini wengine hupitiwa na usingizi mzito mara tu baada ya mazoezi ya masaji.

3. Kuondoa mfadhaiko wa akili  (Stress)

Zaidi ya asilimia 32 ya watu waliojaribu tiba hii wanathibitisha kupungukiwa na kiasi kikubwa cha mfadhaiko wa akili katika miili yao huku tafiti zaidi zikiendelea kutoa ushuhuda wa aina moja.

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Afya cha chuo kikuu cha Harvard umethibitisha kuwa masaji huondoa hamaki na maumivu huku yakiongeza uwezo wa kupata usingizi mzuri na wa uhakika.

Chuo kikuu cha afya cha Boston Uingereza kiliona matokeo yaliyo sawa kati ya wagonjwa 60 wenye kansa ambao walifanya tiba ya masaji dakika 20 kabla ya mionzi kuliwapunguzia kiwango cha hamaki na mfadhaiko wa akili.

Watafiti kutoka Australia wameripoti kwenye jarida la afya liitwalo ‘The Journal of Thoracic and Cardiovascular Surgery’  kuwa masaji hupunguza maumivu, hamaki na mshtuko wa mishipa baada ya upasuwaji wa moyo.

Utafiti mwingine kutoka chuo kikuu cha Toho cha Japan umethibitisha masaji inayohusisha mafuta maalumu ambayo huwa na harufu ya kunukia (ya kuvutia) na ambayo ni dawa husaidia kupunguza mfadhaiko wa kisaikolojia katika wazee wagonjwa wanaotibiwa majumbani.

4. Kuondoa huzuni

Tafiti kutoka chuo cha afya cha Nashville’s Meharry Medical College wagonjwa 43 wa ukimwi walionyesha kuondokewa na hali zao za huzuni baada ya kufanya masaji ya mwili mzima kwa majuma matatu tu.

Profesa maarufu na mtafiti Russell Poland, Ph.D. ambaye ni Profesa wa magonjwa ya akili na sayansi ya akili amesema: “Wakati tunaanza huu utafiti hatukutegemea kuona matokeo mazuri kiasi hiki kwa tiba hii ya masaji. Sote tulibaki na mshangao tu’’.

Faida hizi zilirudiwa pia na chuo kikuu cha Los Angeles Calfornia Marekani ambapo watu 95 waliojitolea kwa utafiti wa tiba hii ya masaji walionyesha kuongezeka homoni ijulikanayo kama 'oxytocin' na kupungua kwa homoni nyingine iitwayo 'adrenocorticotropin'.

Oxytocin inahusika na matendo ya huruma, maono, upendo na ushirikiano wa kijamii. Wakati adrenocorticotropin yenyewe huhusika na kupungua kwa mfadhaiko (stress) moja kwa moja.

5. Kuondoa maumivu mbalimbali mwilini

Watafiti kutoka kitengo cha jinakolojia (uuguzi) cha chuo kikuu cha Sao Paulo Brazil walitafiti wanawake 46 wajawazito waliofanyiwa masaji ya mgongo walipunguza kiasi cha maumivu wakiwa leba kwa zaidi ya asilimiaa 27.

Katika utafiti mwingine uliofanyika hospitali kuu ya Beijing nchini China masaji nzito ilisaidia kuondoa maumivu ya mgongo kwa wagonjwa. Kupungua kwa maumivu haya kuliripotiwa na robo tatu kati ya wagonjwa 110 waliofanyiwa utafiti huo.

Maumivu mengine yaliyoripotiwa kuondoka kwa kutumia tiba ya masaji ni pamoja na maumivu ya kichwa na maumivu ya kwenye mishipa.

6. Kuongeza uwezo wa kujiamini

Watu wengi zaidi kila kukicha wanaendelea kuitafuta huduma hii ya tiba kwa njia ya masaji wakiwa na maradhi mabalimbali katika miili yao. Madaktari wengi nao wameendelea kuwashauri wagonjwa wao kujaribu tiba hii.

Utafiti unaendelea kuwaeleimisha watoa tiba hii jinsi ya kuifanya ili kupata matokeo mazuri katika kutibu matatizo kama maumivu sugu ya misuli, matatizo yanayotokea wakati wa matibabu ya kansa, wakati wa mabadiliko yaletwayo na ujauzito, na maradhi mengine mengi.

Matatizo mengine yanayoweza kutibika kwa kutumia masaji ni pamoja na saratani ya matiti, tatizo la kufunga choo, ukichaa, maumivu, maumivu ya kichwa, maumivu ya mifupa, baridi yabisi (stroke) nk.

Bila shaka mpaka hapo umepata kuzijuwa faida za masaji na magonjwa inayoweza kuyatibu.



Tafadhali SHARE kwa ajili ya uwapendao.

No comments:

Post a Comment

FEATURED POSTS

AFYA TIPS