Powered By Blogger

Saturday, August 5, 2017

FAIDA ZA ASALI NA MDALASINI

KAMA ULIPITWA NA MAKALA YA FAIDA ZA ASALI NA MDALASINI BASI SOMA HAPA


1. Asali ikichanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.

2. Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini.

3. Asali inatajwa pia kuwa dawa ya jino, inaponya pia ngozi iliyoharibika, ni dawa asilia ya shinikizo la juu la damu na kiungo muhimu katika utengenezaji wa asilimia kubwa ya madawa mmimiko na asilimia kubwa ya vipodozi na mafuta ya kupaka.

4. Ugonjwa wa mafua(wengine huita ugonjwa wa mapenzi) ambao huwakera na kuwanyima watu wengi raha unaweza kupungua na kupotea kabisa ikiwa utatumia kijiko kimoja cha chai cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko cha chai cha mdalasini. Mchanganyiko huo pia ni mahususi katika kusaidia kupunguza na kuondoa chafya na kuvimba kwa koo.

5. Asali na mdalasini hutumika katika mwongozo wa tiba ya upungufu wa nguvu za kiume. Yaani huongeza hamu ya tendo la ndoa

6. Asali na mdalasini husaidia katika kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ukiwa katika kadhia hiyo, unashauriwa kuongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali kwenye chai ama maji.

7. Asali na mdalasini husaidia kupunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.

8. Ulaji wa asali pamoja na mdalasini husaidia kuondoa mchafuko wa tumbo uletwao na gesi.

9. Matumizi ya mara kwa mara ya asali na mdalasini wakati wa kifungua kinywa husaidia kuzuia uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo pamoja na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu.

10. Kula mkate uliopakwa asali kijiko kimoja cha mezani kila siku  ni muhimu pia kiafya kwani hupunguza uwezekano wa kutokea kwa tatizo la kuziba kwa mishipa ya damu.

11. Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu yanaweza kutoweka kwa kutumia mara kwa mara asali iliyochanganywa na mdalasini.

12.Matumizi ya mara kwa mara ya asali na mdalasini husaidia kuimarika na kuongezeka kwa kinga ya mwili kutokana na asali  kuwa na hazina kubwa ya virutubisho na madini.

13. Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo, huondoa kiungulia.

14. Unywaji wa kila siku wa kikombe baridi cha chai iliyowekewa asali na mdalasini huimarisha afya bora na madhubuti kwa mtumiaji.

15. Asali ni tiba rafiki na asilia kwa watu wenye shida ya chunusi. Ili kutibu tatizo hilo changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja mdalasini na pakaa kwenye chunusi. Uwezo wa asali wa kuua bakteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili pekee.

16. Asali husaidia kuirudisha ngozi iliyoharibiwa na wadudu kama dondola na washawasha na hata ngozi iliyopata madhara kutokana na kuungua moto. Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati muwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi uvimbe unapotoweka.

17. Kwa mujibu wa tafiti za hivi karibuni zilizofanyika nchini Australia na Japan asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa anayetumia madawa ya kutibu saratani kwa kutumia kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi.

18. Upo ushahidi mpya kwamba sukari asilia zilizopo kwenye asali, zina uwezo wa kuongeza nishati mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu. Wataalamu wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji kisha nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi na kisha kunywa tena alasiri wakati nishati (nguvu) inapoanza kushuka.

19. Asali ina uwezo mkubwa wa kupunguza na kuponya miguu iliyopasuka kwenye kisigino. Chua asali na mdalasini vuguvugu katika miguu au nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu na kazi au baada ya mazoezi marefu. Rudia kila siku asubuhi halafu, osha nyayo zako kwenye maji baridi na vaa viatu.

20. Kusukutua maji ya vuguvugu yaliyowekwa asali na mdalasini kila asubuhi husaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni (halitosis) kutokana na uwezo wa asali kuua bakteria.

KUMBUKA: HIZO FAIDA UTAZIPATA ENDAPO UTATUMIA ASALI MBICHI PEKEE NA SIYO ASALI ILIYOCHEMSHWA




No comments:

Post a Comment

FEATURED POSTS

AFYA TIPS