Saturday, June 24, 2017

TATIZO LA KUNUKA MDOMO NA JINSI YA KUJILINDA

TATIZO KA KUNUKA MDOMO

Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla.
Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni hupunguza mtu kuwa lovable kwani hata unapoongea wengi watakwepa kuongea direct na wewe kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka mdomoni.
Kile unakula kina affect hewa unayotoa iwe mdomoni au sehemu nyingine. Na baadhi ya vyakula vina matokeo mabaya sana kwa hurufu unayotoa mdomoni.

Harufu mbaya mdomoni si ugonjwa wa kuambukiza haina haja kuogopa ukikutana na mtu mwenye harufu mbaya mdomoni kwamba atakuambukiza.

Pia tatizo kubwa ni kwamba watu wenye harufu mbaya mdomoni hawajijui kwamba wana harufu mbaya.
Asilimia 85 – 90% ya tatizo la harufu mbaya mdomoni asili yake ni kinywa chenyewe. Pia kiwango cha harufu hutofautiana kutokana na muda (mchana, usiku na asubuhi).
Harufu nyingi mbaya mdomoni hutokana na vyakula vyenye asilia ya protein.
Kuna zaidi ya aina 600 ya bacteria wanaoishi kwenye kinywa cha Binadamu (sehemu ya juu ya ulimi, fizi na kuzunguka meno).

NINI HUSABABISHA KUWA NA HARUFU MBAYA MDOMONI

Kutokuwa makini na usafi wa kinywa kama vile kupiga mswaki vizuri kunakoacha mabaki ya chakula ambayo huoza na kusababisha harufu mbaya mdomoni.
(Wengi hupiga mswaki haraka haraka na kuacha mabaki ya chakula)
Maambukizi ya magonjwa kama vile fizi kutoka damu, mfumo wa upumuaji na kisukari.
Kinywa kuwa kikavu kutokana na medications
Kuvuta sigara, kunywa kahawa

JINSI YA KUTAMBUA KWAMBA UNA HARUFU MBAYA MDOMONI

Wanasayansi wamekiri kwamba ni ngumu sana mtu kujijua mwenyewe kama ana harufu mbaya kwa sababu ya mazoea (habituation).
Ni rahisi sana kutambua harufu kutoka kwenye kinywa cha mtu mwingine.
Unaweza kutambua kama una harufu mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu unayemuamini.
Pia unaweza kujua harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa, wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa.
Pia unaweza kutumia kijiti cha kuchokonolea meno na kukinusa.
Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama Halimeter, Gas Chromatography na BANA Test.

JINSI YA KUJILINDA NA HARUFU MBAYA MDOMONI (TIBA)

Kula vyakula vyenye afya na pia kula vyakula ambavyo wakati unakula vinaweza kusafisha kinywa vizuri.
Kusafisha meno mara mbili kwa siku asubuhi na baada ya mlo wa usiku, unashauriwa kutumia tongue cleaner kusafisha ulimi.
Tumia chewing gum ambazo husaidia kuongeza kiasi cha mate kwenye kimywa kilichokauka. Baadhi ya gums zina viungo vinavyoondoa harufu mbaya mdomoni na zingine husafisha kinywa na bacteria wanaosababisha harufu mbaya.
Tumia dawa ya kusukutua mdomoni (mouthwash) kabla ya kulala usiku.
Kuwa makini na afya ya kichwa chako kama vile kupiga mswaki vizuri, kuondoa mabaki ya vyakula kwenye meno na kumuona daktari kila unapoona una Matatizo ya meno au kinywa.
Kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku angalau glass mbili za maji.
Mwone daktari wako ukiona una tatizo la harufu mbaya mdomoni.

Tuesday, June 20, 2017

UJUE UGONJWA WA KISUKARI NA JINSI YA KUJIKINGA

UJUE UGONJWA WA KISUKARI (Diabetes)
Kisukari ni ugonjwa unaotokana na mtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati.
Ugonjwa wa Kisukari hutokea pale ambapo tezi ya kongosho inaposhindwa kutengeneza kichocheo (Homoni) aina ya insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka kwa sukari (Hyperglycemia) au kushuka kwa kiwango cha sukari (Hypoglycemia). Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa na kuwa na kiwango kidogo cha insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili

KISUKARI NI NINI HASWA?
Sukari mwilini hutokana na vyakula pamoja na vinywaji tunavyotumia kila siku na hutumika kuupa mwili nguvu. Glukosi ni aina ya sukari ambayo huzipa chembe za mwili nishati. Hata hivyo ili glukosi iingie ndani ya chembe hizo inahitaji insulini. Insulini ni kemikali (Homoni) ambayo hutokezwa na kongosho (Pancrease).

NINI CHANZO HASA CHA KISUKARI?

Ili kuelewa vyema ugonjwa wa kisukari ni muhimu kwanza kuelewa namna chakula kinavyovunjwa vunjwa na kutumiwa na mwili ili kuzalisha nguvu. Wakati chakula kinapoyeyushwa matukio kadhaa hutokea. Moja ni sukari inayoitwa glucosi ambayo ni chanzo cha nishati/nguvu mwilini huingia katika damu. Tukio la pili ni kiungo kinachoitwa kongosho (Pancrease) kutengeneza kichocheo cha insulini. Kazi ya insulini ni kuondoa glucosi katika damu na kuingiza katika misuli, seli za mafuta na ini, ambako hutumika kama nishati.
Watu wenye kisukari huwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kuliko inavyotakiwa kwa sababu miili yao haiwezi kupeleka sukari kwenye seli za mafuta, ini na misuli ili ihifadhiwe kwa ajili ya kuzalisha nguvu. Hii ni kutokana na moja ya sababu zifuatazo, huenda kongosho zao haziwezi kutengeneza insulini ya kutosha au seli za mwili wao haziathiriwi na insini kama inavyotakiwa au sababu zote hizo mbili.
DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
Kama wewe ni mnene kupita kiasi, hufanyi mazoezi kwa ukawaida au una watu wa ukoo walio na kisukari, huenda tayari una kiwango cha juu cha sukari kwenye damu. Ongezeko la sukari kwenye damu mbali na kuwa kisababishi cha kisukari, hali hiyo inahusianishwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa akili uitwao 'DEMENTIA'.

Kula sukari nyingi sio sababu ya ugonjwa wa kisukari. Lakini lazima tuseme kwamba kula sukari nyingi si nzuri kwa afya yako kwani utaongeza uzito wa kuweza kuathiri uwezo wa mwili wako kujikinga na maradhi tofauti. Ugonjwa wa kisukari umeitwa kwa kufaa "ugonjwa unaoathiri kiini cha nishati ya mwili". Mwili unaposhindwa kutumia glukosi, mifumo mbalimbali ya mwili inaweza kuacha kufanya kazi au hata kusababisha kifo
Ugonjwa wa Kisukari kitaalamu hujulikana kama 'DIABETES MELLITUS'. Jina 'Diabetes Mellitus' linatokana na neno la Kigiriki linalomaanisha 'kunyonya' na neno la Kilatini linalomaanisha 'tamu kama asali'. Maneno hayo yanafafanua vizuri sana ugonjwa huo, kwani maji hupita mwilini mwa mtu aliye na ugonjwa wa kisukari kana kwamba yananyonywa na mdomo na kupitia kwenye njia ya mkojo kisha kutoka nje ya mwili. Isitoshe mkojo huwa na ladha tamu kwa kuwa una sukari.
Nyingine ni ngozi kuwa kavu na kuwasha, mgonjwa kupoteza uzito bila sababu, kuwa na ukungu machoni, kuchoka kusiko kwa kawaida, hisia kupungua katika vidole na viganja
mikononi na miguuni na kuwa na ukungu katika fizi, ngozi na kibofu cha mkojo.
NI NANI ANAWEZA KUWA NA UGONJWA WA KISUKARI?
Watu walio katika makundi yafuatayo wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kisukari:
 Wenye uzito uliozidi
 Wenye historia ya kuwa na wagonjwa wa kisukari katika familia zao,
  Wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi,
 Watu wasiojishughirisha au wasiofanya mazoezi,
  Wenye shinikizo la damu,
  Wenye msongo wa mawazo na
  Wenye matumizi makubwa ya pombe na sigara
 Watu hawa wanashauriwa kupima sukari yao kila mwaka wakiwa na umri wa miaka 45 na kuendelea.
Kuna hatari kubwa ya kuugua ugonjwa huo ikiwa mtu ana mafuta mengi katika tumbo na kiuno chake kuliko katika mapaja yake. Mafuta katika kongosho na ini huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu.
Wavutaji wa sigara wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi kwani zoea hilo hudhuru moyo na mfumo wa mzunguko wa damu na kubana mishipa ya damu. Kitabu kimoja kinasema kwamba asilimia 95 ya watu wanaougua kisukari ambao hulazimika kukatwa viungo ni wavutaji wa sigara.

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
  Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati
  Kwenda haja ndogo mara kwa mara. Watoto kukojoa kitandani
  Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.
  Kupungua uzito au kukonda licha ya kula vizuri.
  Kusikia njaa kila wakati na kula sana.
  Wanawake kuwashwa ukeni.
  Kutoona vizuri.
  Kupungua nguvu za kiume au hamu ya kujamiiana kwa wanawake.
  Ganzi, kuchomwachomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole
  Miguu kuoza na hata kupata gangrini.
  Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ganzi katika miguu.
  Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.
  Majipu mwilini.

Wenye dalili hizi wanashauriwa kupima sukari ili kubaini kama wana kisukari.
Watu wenye kisukari wanapaswa kubadili jinsi wanavyokula na kuishi.Ufuatao ni ushauri wa kuwasaidia kufanya mabadiliko:
• Anza na mabadiliko madogo madogo. Kwa mfano, badala ya kuacha utumiaji wa vinywaji vilivyokolezwa sukari mara moja, jaribu kupunguza matumizi ya vinywaji hivyo taratibu. Kupunguza taratibu kiasi cha sukari unayokula au kuongeza kiasi cha mazoezi ni rahisi kutekeleza na kuna uwezekano mkubwa utazoea na kuendelea na utaratibu huo.
• Amua mwenyewe unataka kubadili nini. Weka lengo kama vile kutembea zaidi, kupunguza uvutaji au kutovuta kabisa, au kuweza kucheza na wajukuu zako.
• Tafuta msaada. Familia, marafiki, au watu wengine wenye kisukari wanaweza kukusaidia kufanya mabadiliko.
• Tafuta msaada kwa matatizo ya kisaikolojia. Ni jambo la kawaida kwa watu wenye kisukari kuogopa maisha ya baadaye, kuhuzunika juu ya kuugua mara kwa mara, au kuwa na hasira juu ya mabadiliko yanayohitajika. Hisia za uchungu, huzuni, au kukosa matumaini vinaweza kumzuia mtu mwenye kisukari kufanya mabadiliko ambayo yanahitajika au ambayo anataka kufanya.
• Tafuta sababu zako za kutaka kuwa na afya bora zaidi. Unataka kufanya nini na unataka kujisikia vizuri namna gani? Kwa mfano, fikiria familia yako na kwa nini unataka kuendelea kuishi ukiwa mwenye afya ya kukuwezesha kuwasaidia wanafamilia kwa muda mrefu zaidi.
• Ugonjwa wa kisukari ni tatizo ambalo siku hizi husababishwa na mfumo wa maisha tunayoishi hasa vijana, tafiti zilizowahi kufanywa zinaonesha kuwa vijana wapo kwenye hatari kubwa ya kupata kisukari kwa sababu ya mfumo usio sahihi wa maisha wanayoishi vijana.
• Kutokufanya mazoezi, kukosa muda wa kupumzika na kutokula mlo sahihi,unywaji wa pombe na uvutaji sigara wa kupitiliza, hizi ni sababu chache zinazochangia vijana kuishi katika mfumo wa maisha hatarishi wa kupata maradhi ya kisukari.
Baadhi ya dawa za mitishamba zinaweza kusaidia kucontrol sukari mwilini
Waulize wataalam wa tiba za asili dawa gani za mitishamba zinapatikana katika eneo lako kwa ajili ya kupunguza sukari kwenye damu na kuwa kawaida, njia bora zaidi za kuzitumia, na kama ni salama kuzitumia sambamba na insulini na dawa zingine.
Duniani kote, wataalam wa tiba za asili wamegundua vyakula na dawa za mitishamba ambazo zinaweza kusaidia kupunguza sukari kwenye damu. Ifuatayo ni mifano kadhaa:
• Bitter melon , Mdalasin, Binzari ya manjano, Majani ya mlonge, Uwatu (Fenugreek), Forosadi (Mulberry) , Tangawizi , Nopal (cactus, Bitter leaf , Siki
SHARE UJUMBE HUU KWA NDGU NA MARAFIKI KWA MSAADA WA ELIMU JUU YA UGONJWA HUU

SARATANI YA TEZI DUME(VISABABISHI,DALILI PAMOJA NA JINSI YA KUIEPUKA)

HABARI ZENU WADAU WA MAKALA ZANGU..?

LEO NATAKA NIIZUNGUMZIE CHANGAMOTO YA SARATANI YA TEZI DUME.

SARATANI ya TEZI DUME inashika NAFASI YA TATU kwa kusababisha VIFO vinavyotokana na KANSA kwa WANAUME duniani.

UGONJWA huu ni chanzo kikuu cha VIFO vinavyosababishwa na SARATANI kwa WANAUME wenye UMRI wa kuanzia MIAKA 45 na kuendelea, hata hivyo, SARATANI ya TEZI DUME kwa sasa inawapata sana WANAUME kuanzia MIAKA 25.

Kwa ufahamisho tu ni kwamba NENO SARATANI ni JINA la UGONJWA ambalo hutokea wakati CHEMBE HAI au SELI katika sehemu fulani ya MWILI zinapoanza KUKUA bila kufuata UTARATIBU wa MFUMO WA MWILI na kutengeneza VIJIUVIMBE vidogo vidogo.
Kwa kawaida SELI huwa ZINAJIGAWA, KUPEVUKA na baadaye ZINAKUFA.

UTOKEAJI wa SARATANI ni pale ambapo SELI zilizotakiwa KUFA HAZIFI, zinaendelea KUISHI wakati HUOHUO zile MPYA zinazidi KUZALIWA.

UKWELI ni kwamba WANAUME wote WANAZALIWA na TEZI DUME lakini baada ya BALEHE, TEZI DUME huongezeka UKUBWA mara MBILI.
Na ikifika MIAKA 30 TEZI DUME huanza KUKUA haraka zaidi.Hii ni kwa sababu UKUAJI wa TEZI DUME huenda SAMBAMBA na UMRI.

Kuna VIHATARISHI vingi vinavyochangia MWANAUME kupata SARATANI ya TEZI dume.

Vifuatavyo ni baadhi yake:-

-UMRI. Nafasi ya kupata SARATANI ya TEZI DUME huongezeka sana hasa ukifikia UMRI wa karibu MIAKA 50 na kuendelea.

-NASABA ni kihatarishi kingine ambapo WANAUME wenye HISTORIA ya tatizo hili kwenye FAMILIA ZAO,wale ambao MMOJA WA NDUGU ZAO wamewahi kuugua UGONJWA huu, huwa katika HATARI ya kupata SARATANI hiyo kutokana na KURITHI JENI za UGONJWA huo.

-SUALA jingine ni LISHE ambapo WANAUME wanaopenda KULA NYAMA(red meat) na WALAJI wa CHAKULA chenye kiasi KIKUBWA cha MAFUTA hasa ya WANYAMA, huwa katika HATARI KUBWA ya kupata SARATANI ya TEZI DUME.

-Pia WATAALAM wanatumbia kuwa,WANAUME wasiopenda kufanya MAZOEZI,WANENE na WENYE UPUNGUFU wa VIRUTUBISHO vya VITAMIN E pia wako kwenye HATARI ZAIDI ya kupata SARATANI ya KIBOFU cha MKOJO.

-WANAUME wengine walio katika HATARI KUBWA ya kupata SARATANI ya TEZI DUME ni pamoja na wale wenye ASILI ya AFRIKA(Weusi), ikilinganishwa na WAZUNGU.

-WAKULIMA wanaotumia aina fulani ya MBOLEA za KEMIKALI, wanaofanya KAZI katika VIWANDA vya kutengeneza MATAIRI na WACHIMBAJI MADINI, hususani aina ya cadmium

DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME

Katika HATUA zake za AWALI, dalili za saratani ya TEZI DUME hazitofautiani na zile za KUVIMBA kwa TEZI DUME au BPH. Dalili hizo ni pamoja na:-

1.Kupata SHIDA wakati wa kuanza KUKOJOA.

2.Kutiririka kwa MKOJO baada ya KUMALIZA kukojoa.

3.Kukojoa MKOJO wenye mtiririko DHAIFU.

4.Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za USIKU.

5.KUJIKAKAMUA wakati wa kukojoa na KUSHINDWA kumaliza MKOJO wote.

6.Kutoa MKOJO uliochanganyika na DAMU.

KITAALAM imethibitika kuwa endapo MWANAUME HUYU hasa mwenye MIAKA kuanzia 30 atapata VIRUTUBISHO maalum vya VITAMINI na MADINI anaweza KUEPUKA CHANGAMOTO HII.

WANAUME waliopo HATARINI zaidi ni kuanzia MIAKA 45 na kuendelea. Kwani katika kila WANAUME 6 inakadiriwa kuwa MMOJA atakuwa na SARATANI HII.

Monday, June 19, 2017

ZIFAHAMU AINA KUMI NA MBILI(12) ZA MAUMIVU YA KICHWA NA TIBA ZAKE

AINA KUMI NA MBILI ZA KUUMWA NA KICHWA

Kuumwa na kichwa kumegawanyka sehemu kuu nyingi sana japo kuwa 1% yake ni hashirio la matatizo ya kiafya ambayo yameadvance. Kama vile concussion of brain,meningitis,encephaliti, na stroke. Kuumwa na kichwa pia inawezatokana na matatizo ya taya, meno au hata kula vitu vya baridi zaidi. Vyakula vyenye nitrite au monosodium glutamate.
Sehemu ambazo huuma ni kama ifuatavyo.mfumo wa fahamu ambao upo kwenye fuvu la kichwa.
Baadhi ya neva za fahamu zizlizoko usoni
Misuli ya kichwani
Mishipa inayopatikana kwenye fuvu la kichwana chini ya ubongo kuna mifumo ya fahamu yenye hisia. Kumbuka fuvu na tishuu za ubongo kwa zenyewe haziumi kwani hazna mifumo ya fahamu ambayo inahisia.
Mambo haya 12 nayo yanahusika sana.

1:Nervous tension headaches;

Ni maumivu ya kichwa endelevu upande mmoja au pande zote za misuli ya shingo na upande wa juu wa mgongo,kuumwa na kichwa pamoja na kusinzia. Tumia vitamin b2 na c , punguza au acha matumizi ya sukari,kahawa,chakula chenye kukusababishia mzio,misongo ya mawazo na ufanye mazoezi yakutosha.

2: Cluster headaches

Kichwa kuuma haswa upande mmoja wa kichwa kwa maumivu makali, machozi humtoka mtu na makamasi kwa mbali. Kitu cha kwanza ni kutumia chakula chenye protein ya kutosha, epukana na chakula chenye mzio kwako.

3: Hangover headaches;

Hii ni hali ya kichwa kuuma kwa sababu ya matumizi makubwa ya vinywaji vikali haswa pombe. Weka barafu chini ya kichwa yaani maeneo ya kichogoni au shingoni,kunywa maji mengi na juice ya matunda freshi na uache pombe.

4: Exertion headaches;

Hutokea pale ambapo mwili utatumika sana na haswa kwenye ngono. Weka barafu linalouma, kula mlo kamili na usifanye mazoezi.

5: Caffein headaches;

Hali hii hutokea pale ambapo umeacha matumizi makubwa sana ya kahawa kwa ghafla. Kunywa kiasi kidogo cha kahawa kuondoa maumivu na upunguze matumizi kidogokodogo mpaka utakapo acha kabisa.

6: Sinus headaches;

Maumivu haya huanzia upande wa kulia na kushoto wa pua na kupanda mpaka kichwani. Kula vitamini C kwa wingi na umuone mtaalamu wa afya maana saa zingine hii utkana na maambukizi.

7: Bilious headaches;

Kichwa na macho huuma haswa kipanda uso na husababishwa na kula sana, kula vibaya, kutofanya mazoezi na kukosa choo. Fanya mazoezi na kunywa maji yakutosha na kasha fanya enema.

8: Hunger headaches;

Maumivu ya kichwa ambaya husababishwa na kutokula kwa muda. Kula chochote ilimradi kiwe ni protein au carbohydrates .

9: Eyes ram headaches

Haya ni maumivu yanayotokea kwenye macho na wengi hudhani labda wameangalia vibaya japo saa zingine inaweza kuwa sababu. lakini chanzo chake haswa ni ubongo kufanya kazi kupita kiasi. Badili mtindo wa maisha na kama ni mtumiaji wa miwani ni vyema ukamuana mtaalamu aangalie kama lensi zimepotea nuru au la.

10: Menstrual headaches;

Hali hii hutokea kwa kina mama kipindi cha yai kupevuka. Hutokana na mabadiliko ya hormone, muone mtaalamu wa afya.

11: Arthritis headaches;

Haya ni maumivu ya kichwa yanayosikika mpaka shingoni na saa zingine mpaka mgongoni ambayo husababisha maumivu haswa unapozidisha mwendo au shughuli. Kitu kikubwa ni kutibu ugonjwa unaosababisha hali hiyo.

12: Hypertension headaches;

Ni maumivu ya kichwa chote, mwendo mkubwa pia huongeza maumivu. Hali hii husababishwa na shinikizo la damu. Tibu au pambana kushusha shinikizo la damu na halii itaisha bila shaka.

@Swali lolote comment hapo chini nawe utajibiwa haraka kwa blog yetu

Saturday, June 17, 2017

TATIZO LA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME NA CHANZO CHAKE

...
LIFAHAMU TATIZO LA #UKOSEFU WA NGUVU ZA #KIUME NA CHANZO CHAKE.

Leo katika zama hizi za sayansi na teknolojia tatizo la kupungua nguvu za kiume limekuwa kubwa sana, siyo Tanzania tu, bali duniani kote. Jambo muhimu analopaswa mwanaume yeyote kufahamu ni kwamba, kupungua nguvu za kiume siyo ugonjwa, ni dalili ya ugonjwa. Hii ina maana kuna dosari au udhaifu wa kiutendaji ndani ya mwili wake. 

Kuna sababu nyingi mno zinazosababisha mwanaume apungue nguvu za kiume. Mtu aweza kujiuliza kwa nini kuwe na sababu nyingi namna hiyo?

Kwani nguvu za kiume ni nini?

Nguvu za kiume ni jina la jumla lenye vipengele vingi ndani yake ikiwa ni pamoja na hamu ya mapenzi; kusimama kwa uume barabara; kuchelewa kufika kileleni kiasi cha kufurahia tendo la ndoa; uwezo wa kurudia tendo la ndoa; pumzi, wepesi na uchangamfu wa mwili katika kutenda tendo  lenyewe.

Ni viungo gani vinavyohusika na nguvu za kiume?

Nguvu za kiume ni tukio pana sana lenye kuhusisha viungo na vitu vingi ndani ya mwili. Kuna zaidi ya viungo na vitu 50 ndani ya mwili wa mwanaume vinavyohusika na nguvu za kiume ambapo viungo hivi pia hufanya kazi zingine za mwili. Baadhi ya viungo hivyo ni ubongo, moyo, mishipa ya neva mishipa ya ateri, mirija iliyo ndani ya uume iitwayo corpora cavernosa.

Viungo vingine ni neva maalumu za parasympathetic, tezidume (prostate gland), ini, figo, homoni ya testestorone, kemikali za  acetylcholine, serotonin, na dopamine, uti wa mgongo, eneo la chini ya mgongo (kiuno), eneo la nyonga.

Viungo vingine ni misuli maalumu iitwayo pelvic floor, tezi pituitari (pituitary gland), utando maalumu wa uumeni uitwao tunica albuginea, misuli iitwayopubococcygeus [PC muscles], kemikali ya nitric oxide, kemikali ya prolactin n.k.
Nadhani unaona jinsi ilivyo vitu vingi.

Nini maana ya kupungua nguvu za kiume?

Unapopungua nguvu za kiume ina maana ndani ya mwili wako kuna baadhi ya vitu katika vitu nilivyovitaja hapo juu havifanyi kazi vizuri jinsi ipasavyo na inavyotakiwa. Yawezekana ni figo ndilo halifanyi kazi vizuri, au ini, au tezi dume, au neva ya parasympathetic, au moyo una tatizo au mishipa ya ateri, au misuli ya pelvic au homoni fulani iko juu sana au iko chini sana (hormonal imbalance), orodha ni ndefu sana.

Kitendo cha baadhi ya viungo hivyo kutofanya kazi vizuri basi hapo hutokea upungufu katika nguvu za kiume. Upungufu huo unaweza kuwa ni:

1. Kukosa hamu ya mapenzi; au

2. Uume kusimama kwa uregevu; au

3. Kuwahi kufika kileleni; au

4. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa); au

5. Kushindwa kurudia tendo la ndoa; au

6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo; au

7. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji; au

8. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu;

Ili uelewe vizuri zaidi labda niseme kwamba, nguvu za kiume ni kama kiwanda; na ni zaidi ya kiwanda. Ndani ya kiwanda kuna umeme, maji, madawa, watu (wafanyakazi wa kila taaluma na fani), mashine, mitambo n.k.

Ikitokea kitu kimojawapo kukosekana, mathalani umeme, au wafanyakazi wakagoma, au kukakosekana madawa muhimu au maji na kadhaa wa kadha, basi bidhaa inayotarajiwa kupatikana sokoni, kwa hakika haitapatikana.

Vivyo hivyo nguvu za kiume, mathalani, ikitokea tezi dume kutofanya kazi vyema, basi hapo mwanaume hatoona nguvu za kiume, zitapungua au zitaisha kabisa!

Kwa hiyo upungufu wa nguvu za kiume ni upungufu au kasoro za kiutendaji wa viungo ndani ya mwili wa mwanaume. Mwanaume yoyote anapaswa kutambua jambo hili.

Lakini nini kinachopelekea viungo hivyo vishindwe kufanya kazi vizuri?

Kuna maradhi kadhaa, vyakula tunavyokula, tabia na mtindo wa maisha vinavyoweza kupelekea viungo hivyo kutofanya kazi vizuri. Baadhi ya maradhi hayo na tabia hizo ni kujichua/punyeto (masturbation) kwa muda mrefu; kisukari; presha ya kupanda; presha ya kushuka; uvutaji wa sigara; unywaji wa pombe; madawa ya kulevya; kufanya kazi kupita kiwango na kukosa muda wa kupumuzika; matatizo ya kukosa usingizi na kuchelewa kulala usiku.

Uume wako unatakiwa usimame kwenda juu siyo usimame kwenda mbele tu au kurudi chini. Na ukielekea juu uwe umenyooka kama rula usijikunje kama ndizi maana ukijikunja hilo ni tatizo la kitu kinachoitwa plaque kuganda kwenye uume. See? Ndo maana tunaelimishana rafiki. Tatizo la nguvu za kiume ni pana sana.

Hata hivyo kuna vitu unaweza kufanya ili kurejesha nguvu zako za kiume.

Usilee tatizo. Madhara ni makubwa mno likiendelea kwa muda mrefu!

Mawasiliano haya hapa.

#WhatsApp +255620204770

TATIZO LA KUTOPATA CHOO(CONSTIPATION)

#CONSTIPATION/TATIZO LA KUTOPATA CHOO.

#KAMA UNAPATA CHOO MARA 1 KWA SIKU NA UNAKULA MARA 3,UPO KWENYE HATARI YA KUPATA MAGONJWA YAFUATAYO....….…..

~Kansa ya Utumbo.
~Uzito uliozidi.
~Bawasiri(Vinyama sehemu ya haja kubwa).
~Kifo.
~Maumivu ya Kiuno,Mgongo,Mabega,Kichwa,Misuli.
~Kukosa usingizi(Insomnia)
~Kukosa hamu ya kula(Loss of appetite).
~Tumbo kuja gesi.
~Vidonda vya tumbo(Ulcers).
~Upungufu wa nguvu za kiume.
~Kushindwa kubeba mimba  au kuzaa.
~Kupasuka kwa utumbo.
~Ileocecal valve incompetence.
~Kutoa harufu mbaya mdomoni na unapojamba.

Soma zaidi hapa.............
Kati ya changamoto ya kiafya niliyokua nayo,ni kutopata choo na kupata choo kigumu kama cha mbuzi,na nilidhani ni kawaida kutopata choo kwa muda wa siku 3 hadi week,kumbe ni tatizo kubwa linaloweza kusababisha 90% ya magonjwa yasiyoambukizwa na hatimae vifo.

#WATU wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba.

#CHANZO CHA TATIZO
Tatizo la kutopata choo linasababishwa na mfumo mbovu wa mmeng'enyo wa chakula.

Kwenye utumbo mdogo ambao una urefu wa takribani mara 10 mpaka 13 ya urefu wa mtu husika,kuna Villars, hivi ni kama vidole vinavyokua vinachezacheza ili kumeng'enya chakula,ila kutokana na sumu tunazoingiza mwilini kila siku kutoka kwenye vinywaji,chakula,dawa na hewa,pamoja na mafuta tunayokula kwenye vyakula,zinaenda kujipachika katikati ya Villars (vidole) na hivyo kusababisha vidole visimame(blocked) hivyo chakula hakimeng'enywi na kusababisha chakula unachokula kupitiliza moja kwa moja kwenye utumbo mkubwa,na hapo ndio tatizo linapoanzia.
Na tatizo hili ndio hupelekea kupata tatizo la bawasiri.

#JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI????!!

~Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na Inje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe.

~ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles.

~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50

#AINA ZA BAWASIRI

~Kuna Aina mbili za bawasiri

(A) BAWASIRI YA NDANI

~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili

~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa

(B)BAWASIRI YA NNJE

~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS

#CHANZO CHA TATIZO

~chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni

°Kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
°Kuharisha kwa muda mrefu.
°Tatizo la kutopata choo.
°Matatizo ya umri.
°Shughuri ya kukaa kwa muda mrefu sana.
°Uzito kupita kiasi.
°Matumizi ya vyoo vya kukaa kwa muda mrefu.
°Vyakula vyenye mafuta kwa wingi.
°Vinywaji vikali kama pombe,kahawa,viroba.
°Kutokula vyakula vya nyuzi nyuzi.
°Kutokunywa maji ya kutosha.
°Vyakula vya ngano,wanga na vilivyokobolewa.
°Kutofanya shughuli yoyote baada ya kula.
°Kulala kabla ya masaa 4 baada ya kula usiku.

#DALILI ZA KUTOPATA CHOO NA BAWASIRI.

√ Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa.
√ kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia.
√ kutokea uvimbe/kinyama katika eneo la tundu la haja kubwa.
√kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana.
√ Kinyesi cha makundi makundi kama cha mbuzi.
√ Kuhisi moto wakati wa kujisaidia.
√ Kutopata choo kwa siku 2 na kuendelea.
√ Tumbo kujaa gesi na kujisaidia hewa.
√ Kuhisi maumivu ukikaa.
√ Kusinzia baada tu ya kula
√ Tumbo kuunguruma.
√ Kujamba kila wakati.
√ Kukosa hamu ya kula.
√ Mkojo wenye rangi(ambao sio mweupe kama maji)

#MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI NA KUTOKUPATA CHOO.

~matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula,kama kula matunda,mboga za majani,maji kwa wingi, hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia.

#MADHARA YA TATIZO LA KUTOPATA CHOO NA BAWASIRI.

-kupata upungufu wa damu (anemia).
-Kupata tatizo la kutokuweza kuhimili choo.
-hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake.
-kuathirika kisaikolojia
- kukosa moral ya kufanya Kazi kutokana na maumivu makali.
- Kupasuka kwa utumbo na kusababisha kifo.
- Kitambi na uzito uliopindukia.
- Kansa ya Utumbo.
- Kukosa uwezo wa kubeba mimba.
- Na mengine yoote niliyoyataja mwanzo wa post.

Na Kwa ushauri zaidi juu ya nini ufanye kama una tatizo hilo,na kwa lengo la kujikinga,usikose makala ijayo

Friday, June 16, 2017

UGONJWA WA KIDOLE TUMBO(APPENDICITIS) NA TIBA YAKE

TAMBUA UGONJWA WA KIDOLE TUMBO
(APPENDICITIS) NA TIBA YAKE

Kidole tumbo au Apendeksi hupatikana katika utumbo mkubwa, urefu wake ni kama kidole cha mwisho cha mkono, huwa hakina kazi yoyote mwilini. Sehemu hii hupitisha myeyuko wa chakula na endapo katika chakula hicho kuna michanga au vitu vidogovidogo vigumu, hujikita humo na kushindwa kutoka.

Kidole tumbo pia kinapatikana upande wa kulia wa tumbo kutoka usawa wa kitovu na nyonga ya kulia.
Taka ngumu hizo zikishajikita kwenye kidole  tumbo na kushindwa kutoka ndipo kinapoanza kuvimba, hali hii kitaalam huitwa ‘Inflammation’. Hapa kidole tumbo kinavimba na kuwa na maumivu na pia hupata maambukizi ya bakteria.

DALILI ZA UGONJWA

Mgonjwa huanza kuhisi maumivu ya tumbo  kuanzia usawa wa kitovu ambayo huwa makali na kuacha kisha kusambaa taratibu kuelekea upande wa kulia.

Baada ya muda mgonjwa huanza kutapika  kisha kupata homa. Dalili hizi huwa haziji pamoja, huanza moja na kufuata nyingine lakini mgonjwa akiwahi kupata tiba dalili nyingine haziendelei. Baada ya hapo mgonjwa hupata homa.

Dalili za ugonjwa zinatofautiana kufuatana na aina ya ugonjwa huu ambapo kawaida umegawanyika katika hali ya ukali ‘Acute’ na hali ya usugu ‘chronic’. Maumivu makali yanayoambatana na homa na kutapika tunaita ni ‘Acute’

Maumivu ya ugonjwa huu ukifikia hatua mbaya husambaa hadi katika uti wa mgongo usawa wa kitovu au ‘Belly button’.

Pamoja na kwamba maumivu huanzia usawa wa kitovu, lakini dalili za awali kabisa huanzia juu ya kitovu ambayo huja na kupotea na mgonjwa anaweza kujihisi ana ugonjwa wa vidonda vya tumbo, baadaye ndipo hushuka chini taratibu na kusambaa.

Dalili hizi ni tofauti na watoto ambao hulalamika tumbo linauma sehemu zote kukiwa hakuna eneo maalam na baadaye maumivu huwa makali sana kwa tumbo lote hata akiguswa linauma sana.

Hali ya tumbo kuuma huambatana na kujaa gesi kwa wote yaani wanaume, wanawake na watoto.

CHANZO CHA TATIZO

Kama tulivyoona hapo awali chanzo cha tatizo, maumivu makali ‘Acute’ hapa hutokana na vile vitu vigumu vilivyoingia katika kidole tumbo kushindwa kutoka hivyo huziba kwa juu na zile taka ngumu huganda humo na kidole tumbo kuzidi kuvimba.

Hali ya usugu wa maumivu hutokana na taka ngumu hizo kukaa humo kwa muda fulani na baadaye hutoka huku ukiacha hali ya kidole tumbo kuwa na uvimbe.

Hali ya uvimbe ikikaa muda mrefu husababisha mzunguko wa damu kuzuiliwa sehemu hiyo hivyo kidole tumbo huvimba zaidi na husababisha kuta za Apendeksi kuharibika ‘Necrtotic’ na kukusanya majimaji kama usaha.

Hali hii husababisha tatizo liitwalo ‘Peritonitis’ yaani tumbo lote huathirika na kuuma. Mgonjwa akichelewa kupata tiba, usaha huu husambaa katika mfumo wa damu na kusababisha kifo.

UCHUNGUZI

Huzingatia historia ya mgonjwa, dalili na ishara zitajitokeza, vipimo vya damu vitafanyika, vipimo vingine ni vya Ultrasound na CT Scan ya tumbo vitasaidia kujua tatizo kwa undani zaidi.

Zipo pia njia mbalimbali za uchunguzi ambazo daktari anaweza kuzitumia mfano ‘Rovsing’s sign’ na  sitokovkty’s sign na nyinginezo.
Matibabu

Tatizo hili katika hatua za awali mgonjwa anaweza kutibiwa kwa dawa lakini tatizo linapoendelea inabidi afanyiwe upasuaji kuondoa Apendeksi.

Tatizo likiwa kubwa, upasuaji wa dharura hufanyika. Ni vema uwahi hospitali kwa uchunguzi na tiba.

Featured Post

FAIZA ZA KULA PAPAI

 _*Siri usioijua kuhusu utajiri wa tunda la papai katika kukulinda na magonjwa hatarishi kutokana na faida zake lukuki*_  Hizi ndizo FAIDA 1...