Wednesday, June 14, 2017

FAIDA TISA(9) ZA KULA NANASI

FAIDA ZA KULA NANASI KWA AFYA YAKO

Hapa tuta angalia faida kuu za kula nanasi na Wote tunajua kuwa kula matunda mazuri inasaidia mwili kupata vitamin na madini mbalimbali na kuwa mtu mwenye afya njema, na sasa tunda la nanasi ni tunda moja wapo ambalo ni muhimu sana hasa katika msimu huu wa mananasi.

1: Mmeng’enyo wa chakula.

Nanasi linasaidia kurahisisha mmeng’enyo wa chakula kwa kiasi kikubwa sana. Hii inatokana na kuwa nanasi linatoa aina protini katika mwili wako ambayo inarahisisha kazi hii ya kumeng’enya chakula.

2: Nanasi Lina Vitamin na Madini

Tunda la nanasi limejaa madini na protini nyingi ambazo zinafaa kwa mwili wako. Nanasi lina vitamin A Vitamini C calcium, fiber na pia potassium.

3: Kuzuia Kikohozi na Baridi.

Tangu nanasi lina utajiri wa vitamin C linaweza kupigana na virusi amabavyo vinaweza kusababisha kikohozi na ubaridi. Hata kama umeshakuwa na kikohozi nanasi kwa kiasi flan linaweza kukusaidia kupunguza makali. Tunda hili lina madini ya Bromelain ambayo yanauwezo wa kudhoofisha virusi vya kikohozi. Wakati unaumwa kula tunda la nanasi hata wakati unakuwa kwenye dozi ya dawa ambazo umepewa na daktari linaweza kukusaidia sana kuharakisha kupona haraka.

4: Kuimarisha Mifupa.

Je unahisi mifupa yako sio imara? Basi anza kula nanasi. Nanasi pia lina uwezo wa kuimarisha mifupa nakuifanya kuwa yenye nguvu. Hii ni kwa sababu nanasi lina madini ya manganese ambayo mwili wako unahitaji madini haya ili kwa ajili ya kuimarisha mifupa yako. Tena kama ukinywa kikombe kimoja tu cha juice ya nanasi unakua umeongeza asilimia 73% ya madini ya manganese ambayo ni hata zaidi ya mwili unavyoihitaji kitu ambacho ni kizuri kwa afya ya mifupa ya mwili wako. Unakua na mifupa iliyokomaa.

5: Huimarisha Meno yako.

Watu kila mara huwa wanajali sana meno yao, na mara nyingine huwa wanashindwa kuyapa kipaumbele kwa saaana. Kama una matatizo ya meno basi unashauriwa kula nanasi kwa sababu nanasi linasaidia kuimarisha magego ambayo yanashikiria meno. Kula tunda la nanasi linakufanya kuimarisha magego yanayoshikiria meno na pia meno yenyewe yanaimarika.

6: Huzuia Ugonjwa wa Asthma.

Ukila nanasi unajiweka katika hali nzuri ya kuto pata ugonjwa wa asthma. Watu wanaokula nanasi wanakua katika hali nzuri kwa sababu nanasi lina vitamin aina ya Beta Carotene ambayo linausaidia mwili kukabiliana na magonjwa mbali mbali ikiwemo asthma.

7: Blood Pressure.
Unapokula nanasi unaongeza potassium na pia kula matunda mengine yenye madini ya potassium yanaweza kukusaidia kupunguza uwezekano wa kupata blood pressure.

8. Kansa.
Kama kawaida nanasi lina utajili mkubwa wa vitamin C. Hii vitamin C inauwezo wa kuzuia virusi ambavyo vinaweza kukusababishia magonjwa mabali mabli ya kansa.

9. Huimarisha Afya ya Moyo.

Utajiri wa madini ya fiber, potassium na vitamin C ni mojawapo ya faida za tunda hili ambazo pia zina uwezo wa kuimarisha afya ya moyo wako na kuzuia maradhi yanayoweza kuuadhiri moyo wako.

Sasa jamani tuanze kula tunda la nanasi ili tuweze kufaidi madini ya na vitamin zilizojaa katika tunda hili. ili kuepuka magonjwa ya baadaee. 

Endelea ku subscribe blog hii kwa Habari zaidi. >>>>>>>>

FAHAMU MWANAMKE ANAVOPATA MIMBA

FAHAMU JINSI MWANAMKEE ANAVYO PATA MIMBA

Wengi hasa wanawake wamekuwa wakiuliza maswali mengi sana kuhusuana na jinsi ya mwanamke kupata mimba au kuzuia kutopata mimba.
Naamini maelezo yafuatayo ukisoma kwa makini unaweza kupata ufahamu na kujibiwa maswali yako yote ambayo yamekuwa yanakutatiza.
Pia ni vizuri kuzingatia na kutochanganya Kalenda ya menstrual cycle tunayoongelea hapa na ile 'kalenda ya mwaka' inayohusu tarehe za miezi 12 ya mwaka ambayo huwa tunaitundika ukutani huko nyumbani na maofisini kwetu!

Wanawake wamegawanyika katika makundi makubwa 4 linapokuja suala la siku za hedhi

Mzunguko mfupi yaani siku 22
Mzunguko wa kati yaani siku 28
Mzunguko mrefu yaani siku 35
Na mzunguko abnormal siku 15

Kama mwanamke ana menstruation cycle ya siku 22 inabidi afanye kama ifuatavo:

Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstruation cycle kama hapa chini:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd.

Kisha ahesabu kuanzia ile 22nd day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 8th day ya kalenda yake.
Hivyo 8th day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstration cycle ya siku 22.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!

Kama mwanamke ana menstruation cycle ya siku 28 inabidi afanye kama ifuatavo:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstration cycle kama hapa chini:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 28th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 14th day.
Inamaana kwamba 14th day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstruation cycle ya siku 28.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!
Kama mwanamke ana menstruation cycle ya siku 35 inabidi afanye kama ifuatavo:
Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstruation cycle kama hapa chini:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th, 16th, 17th, 18th, 19th, 20th, 21st, 22nd, 23rd, 24th, 25th, 26th, 27th, 28th, 29th, 30th, 31st, 32nd, 33rd, 34th, 35th.

Kisha ahesabu kuanzia ile 35th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 21st day.
Inamaana kwamba 21st day ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstruation cycle ya siku 35.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed!
Kama mwanamke ana abnormal menstruation cycle ya siku 15

BASI KUNAUWEZEKANO WA KUTOPATA MIMBA KABISA KAMA INAVYOONEKANA HAPA CHINI:

Kwanza itabidi atengeneze kalenda yake mwenyewe ya siku zake zote za menstruation cycle kama kawaida:
1st, 2nd, 3rd, 4th, 5th, 6th, 7th, 8th, 9th, 10th, 11th, 12th, 13th, 14th, 15th.
Kisha ahesabu kuanzia ile 15th day kurudi nyuma mpaka afikishe siku 15.
Ataona kuwa siku ya kumi na tano inaangukia kwenye 1st day.
Inamaana kwamba, the 1st day of her bleeding ndiyo siku ya mimba kwa mwanamke yeyote ambaye ana menstruation cycle ya siku 15.
Akumbuke kwamba 1st day ndiyo siku anayoanza ku-bleed, na ndiyo hiyo hiyo siku ambayo mwanamke wa kundi hili anaweza kupata mimba!
Hii inamaana kwamba, siku ambayo linaharibika lile yai la upande mmoja ndiyo siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linapevuka tayari kwa kurutubishwa.
Mwanamke wa aina hii anaweza kupata mimba tu kama atakutana na mwanaume siku ile anayoanza kubleed, kwani siku ambayo yai moja linaanza kuharibika ndio siku hiyo hiyo ambayo yai la upande wa pili linakuwa tayari kurutubishwa
Na wanawake wa kundi hili la nne ukiwauliza vizuri watakiri kwamba hawajawahi kuona au ku-feel ule ute mweupe ambao wenzao huwa wanaupata siku ile yai linapokuwa tayari kwa kurutubishwa, kwani ute wa wanawake wa kundi hili la nne huwa unachanganyikana na damu kwa vile unatoka siku ile ile wanapoanza ku-bleed.Pia wanawake wa kundi hili huwa wanatokwa na kiasi kidogo sana cha damu na bleed hukatika ndani ya siku moja au mbili tu!

Endelea kuwa pamoja nami na unaweza share na wenzako walitambue hili...

Tuesday, June 13, 2017

JINSI YA KUONDOA CHUNUSI KWA NJIA YA ASILI

JINSI YA KUONDOA CHUNSI KWA NJIA YA ASILI

Magadi Soda:
Magadi soda ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Changanya kiasi kidogo cha magadi soda na maji ya kutosha kuunda kidonge kidogo na kisha weka au kandika kidonge icho sehemu ilio athirika na chunusi. Kwa muda wa dakika 15-20 au mpaka ikauke, na kisha suuza kwa maji yasiwe ya moto. Unaweza kurudia rudia mara kadhaa kwa siku mpaka utakapo ona athari ya chunusi imepotea.

Matango:
Unaweza kutumia Tango kwa kuondoa chunusi na hata kuondoa mabaka mabaka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuonekana yenye afya na yenye kuvutia.
mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Kata tango na kasha liponde ponde (unaweza kutumia blenda) kisha paka au kandika usoni. Wacha ikae kwa muda wa dakika 15-20  kisha suuza kwa maji baridi. Unaweza kurudia kwa siku mara mbili mpaka mara tatu kwa siku.

Kitunguu Thaumu:
Unaweza kutumia kitunguu thaumu. Kuondoa chunusi. Matumizi ya Kitunguu thaumu, uleta matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na hata kuuwa bacteria sababu ina kemikali (antiseptiki) inayozuia kukua kwa bakteria kwenye jeraha au ngozi iliyo athirika kwa chunusi au hata kwenye kidonda. Na pia ina viwango vya juu wa salfa (ni zuri kwa ajili kukausha mafuta kwenye ngozi ya mwili). Twanga kitungu thaumu, au unaweza kukata nusu na kubandika sehemu iliyo na chunusi shikilia kwa dakika 5-10, na kisha safisha na maji baridi. Waweza kufanya ivyo asubuhi na jioni.

Mnana (Peppermint):
Unaweza kutumia majani ya Mnanaa kuondoa chunusi usoni.
Majani ya manna utumika hata kwa wale wenye matatizo ya Mba kwenye kichwa. Twanga majani machache au saga kisha weka sehemu iliyo athirika. Wacha mpaka pakauke na kisha safisha kwa maji baridi. Unaweza kufanya hivyo mara kadhaa kwa siku.

Matumizi ya Limao:
Kata limao na kisha kwa kutumia kijiti chenye pamba kiloweke kwa maji ya limao, sugua sehemu yenye chunusi, kisha wacha pakauke, unaweza kurudia rudi kila baada ya masaa kadhaa. Usitumie maji ya limao ya kwenye chupa, kwa sababu yameweka vihifadhi kemikali zingine kiasi cha kuondoa ubora wa kemikali halisi za kwenye limao. Tumia limao alisi.

Kutumia Asali:
Matumizi ya asali ni ya asili na ufanya ngozi, iwe na afya na nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na kusinyaa kwa ngozi.
Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iwache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.

Kutumia Papai:
Unaweza kushangaa, lakini matumizi ya papai yameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili.
Ponda ponda kiasi kidogo cha papai na kisha iwache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya kawaida. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.

Dawa Ya Meno:
Unaweza kushangaa, lakini ushangazwi na matokeo mazuri ya meno yako kusafishika kwa dawa ya meno.
Kemikali zinazotumika kuuwa Bakteria wa kwenye meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine. Tumia dawa ya meno isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze kufanyakazi vizuri.

Namna nyingine ni kuchanganya dawa ya meno na unga wa mahindi au nganoiuliosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na kuiwacha ikauke kwa dakika tano mpaka 10.
Safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.

Matumizi ya Poda:
Unaweza kutumia baby powder kwa kupaka nyakati za usiku wakati wa kwenda kulala na na kuiwacha mpaka asubuhi.

Matumizi ya Mvuke:
Unaweza kutumia mvuke (Steam/vapour) kuondoa mafuta yaliozidi kwenye ngozi ya uso wako. Kwa kujifukisha. Kwa wale ambao hawana mashine wanaweza kujaza sufuria au bakuli kwa maji ya moto na kujifunika kwa taulo uku ukielekeza uso wao kwenye sufuria au bakuli lenye maji yanayotoa mvuke k wa dakika 5-10. Unaweza kufanya hivi pamoja na njia mojawapo nilizo zitaja hapo juu.

Tahadhari:
Njia hizi za Asili, uchukuwa muda kidogo mpaka kuona matokeo ya kuridhisha.
Njia zote hizi kama hazijaleta matokeo mazuri, tafadhali muone daktari wa ngozi au nenda hospitali ilio karibu kwa uchunguzi zaidi wa ngozi yako.

JINSI YA KUJIKINGA NA HOMA YA INI(HEPATITIS B)

HABARI ZENU WADAU WA MAKALA ZANGU?

Leo nimeona nikushirikishe kuhusu UGONJWA WA HOMA YA INI

HOMA YA INI ni UGONJWA unaoambukizwa kwa njia ya VIRUSI ambavyo vikishaingia MWILINI hushambulia INI kabla ya kugeuka kuwa MARADHI SUGU.VIRUSI ivyo vinaitwa HBV - HEPATITIS B VIRUSES.

VIRUSI hivi husambazwa kwa njia ya DAMU au MAJIMAJI mengine ya MWILINI mfano MATE au JASHO.

UGONJWA huu kama haujatibiwa hutengeneza UVIMBE katika INI na kusababisha KANSA ya INI na baadaye KIFO.

JINSI UNAVYOAMBUKIZWA.
Katika maeneo hatari zaidi DUNIANI,virusi vya HEPATITIS B ( HBV ) kwa kawaida husambazwa kutoka kwa MAMA kwenda kwa MTOTO wakati wa kuzaliwa au kutoka kwa MTU mmoja hadi mwingine hususani nyakati za UTOTONI.

Kama ilivyo kwa UKIMWI virusi vya HOMA ya INI navyo huambukizwa kwa njia ya KUJAMIIANA ,MATE,JASHO, na mwingiliano wowote wa DAMU.

NJIA KUU ZA MAAMBUKIZI :-
- Kujamiiana bila kinga.
- Kunyonyana NDIMI ( Denda )
- MAMA mwenye Ugonjwa kumwambikiza MTOTO wakati wa kujifungua.
- Kuchangia DAMU isiyo salama.
- Kuchangia vitu vya ncha kali kama SINDANO ,WEMBE n.k
- Kuchangia MISWAKI .
- Kuchangia TAULO na mwenye Ugonjwa huo.
- Kubadilishana nguo au kukumbatiana wakati mkiwa mnavuja JASHO .

Tafiti zinaonesha kuwa VIRUSI hivi ni HATARI kuliko hata vya UKIMWI kwa sababu vinaweza kuishi NJE ya MWILI wa BINADAMU  ( yaani nje ya mfumo wa damu ) kwa siku SABA.
VIRUSI vya UKIMWI  ( VVU ) havina UWEZO wa kuishi NJE ya mfumo wa DAMU hata kwa DAKIKA moja.

Kutokana na USUGU wa HBV maana yake ni kwamba kama kirusi kipo kwenye NGOZI,kitaendelea kuwa HAI kwa siku SABA na katika kipindi hicho MTU anaweza kuambukizwa kwa njia ya DAMU au JASHO. Kwa wastani kirusi cha HBV kikishaingia MWILINI hupevuka ndani ya SIKU 75.Hata hivyo upo uwezekano wa kupevuka kati ya SIKU 30 hadi SIKU 180.Ndani ya SIKU 30 mpaka SIKU 60, MTU mwenye HBV anaweza kugundulika ikiwa atapimwa.

MTU mwenye HOMA ya INI ana wastani mdogo wa KUISHI kuliko mwenye UKIMWI.

DALILI ZA UGONJWA HUU.
WATU wengi hawaonyeshi DALILI yoyote.
Kwa maana hiyo MTU anaweza kuishi na HBV na kusababisha MAAMBUKIZI kwa WENGINE bila kugundulika.
Hata hivyo WATU wengine husumbuliwa na HOMA KALI na DALILI ambazo hudumu kwa wiki kadhaa. DALILI hizo ni:-
- Uchovu
- Kichefuchefu
- Mwili kuwa dhaifu
- Homa kali
- Kupoteza hamu ya kula
- Kupungua uzito
- Maumivu makali ya tumbo upande wa INI.
- Macho na ngozi kuwa ya njano.
- Mkojo mweusi.
Kwa WAGONJWA wengine, VIRUSI vya HEPATITIS B hukua hadi kusababisha INI kuharibika kabisa ( Cirrhosis of the liver ) au SARATANI ya INI  ( liver cancer  ).

KINGA.
- Chanjo
- Kutumia kinga wakati wa Kujamiiana.
- Kuacha Kuchangia vitu vya ncha kali.
- Kutochangia miswaki.
- Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu.
- Kutochangia damu isiyo salama.

Monday, June 12, 2017

JINSI YA KUPUNGUZA NA KUONDOA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

JINSI YA KUONDOA AU KUPUNGUZA MAFUTA TUMBONI KWA WANAWAKE

Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana na kitambi kwa upande wa wanaume. Hivyo ingekuwa ni wanaume tungesema ni kitambi ambalo nalo ni tatizo kubwa miongoni mwa wanaume wengi nyakati za sasa.

Kinachowasumbuwa wanawake siyo kitambi tunasema ni mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na tumbo kwa ujumla kufikia hali kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni mafuta tu mengi.

Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, hivyo kwenye post hii pamoja na mengine tutaona pia visababishi vya tatizo lenyewe, dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote.

Nini kinasababisha tumbo kwa kina mama:

*Vyakula feki (Junk food)
*Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi
*Kutokunywa maji ya kutosha kila siku
*Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala
*Kukaa masaa mengi kwenye kiti
*Kutokujishughulisha na mazoezi
*Mfadhaiko (stress)
*Kula wali kila siku
*Ugali wa sembe
*Kula vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (chipsi, maandazi, nk)

Vyakula 25 vinavyoondoa mafuta kwenye tumbo kwa wanawake

1. ASALI NA LIMAU

Chukua asali kijiko kikubwa kimoja cha chakula na majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili, changanya hivi viwili ndani ya glasi moja (robo lita) ya maji ya uvuguvugu na unywe yote mara tu ukiamka asubuhi.

Tumia kwa wiki 3 hivi mpaka mwezi mmoja na hutachelewa kuona tofauti.

2. MAJI YA UVUGUVUGU

Kunywa maji ya uvuguvugu kama lita 1 hivi wakati tumbo likiwa tupu hasa asubuhi ukiamka tu. Hii inasaidia kusafisha mwili na kuondoa mafuta yasiyohitajika.

3. NYANYA

Kula nyanya ambazo hazijapikwa pia inasaidia kupunguza tumbo kwa kina mama, hivyo kula kachumbali ya kutosha kila siku ya nyanya peke yake na utaona mabadiliko.

4. TANGAWIZI

Chemsha chai ya tangawizi, ipua na usubiri ipowe kidogo, ongeza asali mbichi kidogo na pilipili manga kidogo ya unga. Pata kikombe kimoja cha chai hii kila siku asubuhi mapema ukiamka tu. Asali inasaidia kuyeyusha mafuta wakati pilipili itauongezea nguvu mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.

5. SIKI YA TUFAA

Siki ya tufaa (apple cider vinegar) inasaidia kupunguza njaa na kukufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu. Kunywa kijiko kikubwa kimoja cha siki ya tufaa mara 1 kwa siku kila siku wakati unakula chakula cha usiku. Kazi nyingine ya hii siki ni kuweka sawa damu sukari mwilini hivyo ni nzuri pia kwa wenye kisukari.

6. MAJANI YA BIZARI

Majani ya bizari husaidia kuondoa sumu na takatka nyingine mwilini kitu ambacho moja kwa moja hupelekea mlundikano mdogo wa mafuta katika tumbo. Kunywa chai ya majani ya bizari kila siku asubuhi, ukikosa majani unaweza kutumia hata unga wake.

8. ILIKI

Iliki hufanya kazi ya kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na ni dawa nzuri sana ya kuondoa sumu na takataka nyingine mwilini. Iliki pia hutumika katika kupunguza uzito. Tengeneza chai yenye iliki kila siku ndani yake, pia ni kiungo karibu kwa vyakula vingi hivyo hakikisha unaiweka katika kila chakula unachopika kwa matokeo mazuri zaidi.

9. MDALASINI

Mdalasini hufanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini. Chukua kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na uweke ndani ya glasi 1 ya maji ya moto na uache kwa dakika 5 hivi. Ongeza kijiko kidogo kimoja cha asali mbichi ndani yake na ukoroge vizuri, kisha unywe huo mchanganyiko wote asubuhi ukiamka tu.

10. JUISI YA LIMAU

Kunywa maji ya limau au juisi ya limau kila mara kutakusaidia kuondoa mafuta tumboni kwa haraka sana. Ongeza majimaji ya limau vijiko vikubwa viwili ndani ya glasi 1 ya maji na uongeze punje 1 ya chumvi ya mawe, koroga vizuri na unywe asubuhi ukiamka tu kila siku.

11. KITUNGUU SWAUMU

Ili kupunguza mafuta tumboni katakata vipande vidogo vidogo (chop) punje 3 mpaka 4 za kitunguu swaumu na unywe na maji vikombe viwili asubuhi tu na kisha shushia na glasi moja ya maji yenye limau kidogo kwa mbali. Hii ndiyo njia nzuri kabisa ya asili ya kuondoa mafuta tumboni kwa haraka zaidi.

12. TIKITI MAJI

Tikiti maji lina asilimia 82 za maji kitu kinachofanya tumbo lako kutokuwa na njaa ya kuhitaji chakula. Tikiti maji lina vitamini C ambayo ni mhimu kwa afya bora. Kula tikiti kila siku.

13. MAHARAGE

Kula maharage kila mara kunasaidia kupunguza mafuta katika tumbo. Maharage yana kiasi kingi cha nyuzinyuzi (faiba) kitu kinachosaidia tumbo lako kutojisikia njaa na hivyo itakuwezesha kula chakula kiasi kidogo. Kadri unavyokula chakula kichache ndivyo unavyokuwa mbali na uwezekano wa kuzalisha mafuta mengi tumboni.

Basi kula maharage kila siku.

14. TANGO

Tango lina asilimia 96 za maji na asilimia zinazobaki ni nishati. Tumia kachumbali yenye tango ndani yake kila siku au kula tu tango moja kila siku ili kupunguza mafuta tumboni kwa haraka.

15. PARACHICHI

Parachichi ni tunda lingine zuri sana kwa ajili ya kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini. Parachichi ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (faiba). Parachichi huikimbiza mbali njaa na wewe. Parachichi lina mafuta lakini ni mafuta mazuri (monounsaturated fatty acids) ambayo yenyewe husaidia kuchoma mafuta na hivyo kuondoa mafuta mabaya tumboni kirahisi zaidi.

Kula parachichi 1 kila siku.

16. TUFAA

Kula tufaa maarufu sana kama 'apple' (epo) kunaweza kusaidia kupigana na magonjwa mengi sana mwilini na inaweza pia kusaidia kuondoa mafuta kwenye tumbo lako. Tufaa hukufanya ujisikie umeshiba sana kwa masaa mengi sababu lina potasiamu na vitamini nyingi sana ndani yake.

Hivyo kula tunda hili 1 kila siku asubuhi kupunguza shauku yako ya kutaka kula zaidi ndani ya hiyo siku nzima.

17. MAFUTA YA SAMAKI

Mafuta ya samaki ni mbadala mzuri kabisa katika kuchoma mafuta ya tumboni. Mafuta ya samaki yenyewe hulenga kuyachoma moja kwa moja mafuta yanayozidi tumboni. Ukiweza unaweza kuamua yawe ndiyo mafuta yako ya kupikia, pia unaweza kunywa mafuta haya kijiko kikubwa kimoja kila siku unapoenda kulala.

18. SIAGI YA KARANGA

Siagi ya karanga hupunguza njaa na kuongeza nguvu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Siagi ya karanga ina kiinilishe kijulikanacho kama 'niacin' ambacho chenyewe huzuia mafuta kujilundika tumboni. Hivyo kwenye mkate wako asubuhi ningekushauri utumie hii siagi ya karanga badala ya mafuta mengine ambayo si salama, pia unaweza kutumia hii siagi ya karanga kama mafuta yako ya kuunga katika mboga nyingi unazopika hata katika wali unaweza kutumia kama mafuta yako mbadala.

19. MAYAI

Mayai yana vitamini nyingi sana ndani yake (mayai ya kienyeji lakini) na yana madini pia kama kalsiamu, zinki, chuma, omega -3 nk. Viinilishe vyote hivyo katika mayai husaidia kuchoma mafuta yanayozidi tumboni. Hivyo kula mayai asubuhi kila siku ili kuondoa na kupunguza mafuta mwilini. Mayai pia ni moja ya vyakula vinavyomfanya mtu ajisikie kushiba kwa muda mrefu bila kuhitaji kula kula tena.

20. CHAI YA KIJANI

Chai ya kijani maarufu kama 'Green tea' hufanya kazi ya kuondoa sumu mwilini jambo linalosaidia pia kuchoma mafuta yaliyozidi mwilini. Kunywa chai hii ya kijani kila siku kutafanya ngozi yako kukua vivyo hivyo kufanya tumbo lako kukaa sawa bila kuwa na mafuta mengi.

21. MTINDI

Ingawa mtindi unaweza kupelekea kuongeza uzito zaidi, hata hivyo mtindi mtupu kabisa ule ambao haujaongezwa kingine chochote ndani yake unaweza kukusaidia kupunguza mafuta tumboni. Matumizi yake kwa siku yasizidi kikombe kimoja (robo lita). Pia mtindi ni moja ya vyakula vinavyoweza kukufanya ujisikie umeshiba na hivyo kukuondolea njaa ya kutaka kula.

22. JUISI YA KOTIMIRI

Juisi ya kotimiri (Parsley juice) huondoa sumu na takataka nyingine zozote mwilini, pia huchoma mafuta na nishati. Kotimiri ni dawa nzuri kwa matatizo mbalimbali ya figo pia kwa kuchoma mafuta mwilini.

Pata kikombe kimoja cha juisi hii kila siku unapoenda kulala.

23. NDIZI

Kama lilivyo tufaa, ndizi pia zina kiasi kingi cha potasiamu na vitamini za aina mbalimbali ndani yake. Ukipenda kula ndizi kila mara zinachofanya mwilini mwako ni kuondoa ile hamu ya kutaka kula vyakula feki (fast food). Zaidi sana ndizi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na hivyo kupelekea mafuta ya tumboni kuyeyuka kirahisi zaidi. Kula ndizi kila siku ukiweza ukiamka tu kula ndizi zilizoiva 3 mpaka 5 kila siku.

24. MAJI YA KUNYWA

Kunywa maji ya kutosha kila siku kunasaidia pia kupunguza uzito. Kunywa maji lita 2 mpaka 3 kila siku iendayo kwa Mungu. Kunywa maji kidogo kidogo kutwa nzima. Hili halitafanya kazi ya kusafisha mwili tu bali pia litafanya ngozi yako kung'aa na kukuwa. Nywele zako pia zitaonekana ni zenye afya na mwili mzima utakuwa ni wenye kuvutia.

Kitu cha kwanza ukiamka tu ni kunywa maji glasi 2 na uendelee hivyo hivyo glasi moja moja kila baada ya lisaa limoja au mawili kutwa nzima. Maji ni uhai, bila kunywa maji kila siku ni sawa na kwenda dukani bila hela mfukoni.

Asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 ya ubongo wako ni maji, asilimia 27 ya mifupa yako ni maji, asilimia 75 ya mwili wako ni maji. Sehemu kubwa ya dunia hii imefunikwa na maji na sehemu yenye ardhi ni kipande kidogo sana. Haijalishi unaishi kwenye baridi au kwenye joto hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku, huhitaji kusikia kiu au hamu ndipo unywe maji, hapana maji ni lazima uyanywe tu hata iweje.

25. MAZOEZI YA KUTEMBEA

Shida kubwa kwa kina mama wengi wa kiTanzania ni kuwa hawajishughulishi na mazoezi. Hapa Tanzania mazoezi inaonekana ni jambo la wanaume tu. Mazoezi ni jambo la lazima kwa mtu yeyote iwe unaumwa au huumwi.

Ili kuchoma mafuta mwilini kwa haraka zaidi tembea kwa miguu mwendo kasi kidogo lisaa limoja kila siku. Kumbuka nimesema lisaa limoja yaani dakika 60 bila kupumzika (none stop) kila siku. Kutembea kwa miguu lisaa limoja huamsha mwilini kimeng'enya kijulikanacho kama 'lipase' ambacho chenyewe huamka tu ikiwa utatembea bila kusimama kwa dakika 60 na kikishaamshwa (when it is activated) huendelea kuchoma mafuta mwilini kwa masaa 12 mfulululizo.

Usiseme nikitoka sehemu fulani kwenda sehemu fulani nitakuwa nimetembea vya kutosha, hapana, unahitaji uwe na saa mkononi kuhakikisha kweli dakika 60 zimeisha ukiendelea kutembea bila kusimama. Kama utaweza kukimbia kidogo kidogo (jogging) basi utachoma mafuta ya tumbo kwa haraka zaidi.

Ufanye zoezi hili kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili mfululizo na mafuta kwenye tumbo lako yatapotea yenyewe bila kupenda.


Tafadhari SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.

Faida na Madhara ya kula pilipili manga

Pilipili manga ni mbegu ndogondogo zenye umbo la mviringo zenye rangi nyeusi.mbegu hizi hutoa ladha ya muwasho mfano kama pilipili na kutumika sana majumbani hasa upande wa jikoni, wapo wanaotumia kiungo hiki kikiwa kizima au kimesagwa inategemea na mtumiaji anavyopendelea. Wanawake wengi wa pwani hutumika pilipili manga katika vyakula ili kunogesha na kukipa ladha iliyo nzuri chakula, kitoweo hata kinywaji. Pia wapo wanaotumia pilipili manga kuramba endapo watahisi kifua kinawabana. Licha ya kuwa pilipili manga si dawa ya kifua ila kwa mazoea tumeipa nafasi pilipili manga kuwa ina uwezo wa kutibu kifua kama ifanyavyo tangawizi. Faida ya matumizi ya pilipili manga kwa wanawake. Pilipili manga ina faida kubwa kwa mwanamke ambaye ameshajifungua, hivyo ni vema uji anaokunywa uwekwe unga wa pilipili manga kwani humsaidia kutoa uchafu utakaokuwa upo kwenye kizazi ambao umebakia. Humuondolea maumivu ya mwili pamoja na tumbo, humsaidia kutoshika mimba katika kipindi hicho ambacho analea mtoto wake mchanga. Wapo baadhi ya watu wakila chakula au mchuzi rosti wa biriani ambayo inakuwa haijachanganywa na kiungo hiki hupata ugonjwa wa kuharisha au kupata maumivu makali ya tumbo. Lakini endapo utaweka pilipili manga kiasi kidogo basi mtu huyo hatoweza kuharisha wala kuumwa na tumbo hivyo kwa upande mwingine kiungo hiki huisaidia kutibu tumbo kwa mlaji. Katika matumizi ya watu wengi inashauriwa itumike pilipili manga ambayo ni nzima ili mtu ambaye inamdhuru akiwa anakula chakula ni lazima ataona vitumba vya pilipili manga na kuviondoa. Madhara ya matumizi ya pilipili manga; Kwa mwanamke anayehitaji kupata mtoto haruhusiwi kutunmia kiungo hicho kwa wingi kwani kinaweza kumsababishia kushindwa kushika ujauzito na hivyo kuhangaika kwa muda mrefu licha ya kutumia dawa za kila aina. Mwanamke yeyote ambaye anahitaji kupata mtoto anatakiwa ajichunge sana na vyakula anavyokula kwani viko vyakula vingine vina uwezo wa kumsababishia kushindwa kushika ujauzito kwa urahisi. Usitumie pilipili manga kutibu kifua. Kiungo hiki kinapoliwa na mgonjwa wa kifua humsababishia kukohoa mara mbili zaidi ya hapo awali. Kutokana na muwasho, kiungo hiki kuingia moja kwa moja kwenye mapafu na kusababisha mkwanguo ambao unaweza kuleta madhara ya mgonjwa kukohoa damu. Wapo wanaotumia maji ya limao na pilipili manga pindi wanapokohoa. Ni vema waache mara moja. hii ni hatari sana. Pia kiungo cha pilipili manga husababisha ugonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa ambao hupenda kunywa uji uliotiwa pilipili manga kwa wingi wakitumia kama ndio kifungua kinywa. Elewa kuwa utumbo ni laini sana hivyo ni vizuri kujijali hasa katika matumizi ya vyakula vyenye pilipili chache na nyingi kabla ya kula chakula chochote. Hukatazwi kunywa uji wenye pilipili manga ila unatakiwa kuweka kiasi kidogo sana cha kiungo hicho ili kukuepusha na madhara ya vidonda vya tumbo. Angalizo: Wanawake waliokuwa ndani ya ndoa punguzeni matumizi ya pilipili manga na hatimaye ongezeni matumizi ya mdalasini. Mdalasini unaweza kutumiwa kwa jinsi zote ukiwa mapande mapande au umesagwa na kuwa unga. Unga wa mdalasini huchanganywa na asali kisha watumiaji wale kijiko kimoja cha chakula asubuhi, mchana na jioni. Hii itamsaidia sana katika suala la kupata mtoto, watu waliogundua matumizi ya pilipili manga katika kipindi cha kujifungua hawakuwa wajinga kwani kiungo hiki kilikuwa kinatumika enzi na enzi za babu na bibi zetu.

Saturday, June 10, 2017

FAIDA NNE ZA KUNYWA MAJI YA NAZI

1. HUWA NA VIRUTUBISHO KAMA VILE

  • -CARBS: 9 GRAMS.

  • -FIBER: 3 GRAMS.

  • -PROTEIN: 2 GRAMS.

  • -VITAMIN C: 10% OF THE RDI.

  • -MAGNESIUM: 15% OF THE RDI.

  • -MANGANESE: 17% OF THE RDI.

  • -POTASSIUM: 17% OF THE RDI.

  • -SODIUM: 11% OF THE RDI.

  • -CALCIUM: 6% OF THE RDI.

2. HUWEZA KUPUNGUZA SUKARI NDANI YA MWILI

MAJI YA NAZI HUWEZA KUINGIA NDANI YA MWILI NA KUPUNGUZA SUKARI KWENYE DAMU NA HIVYO MWILI KUKUA VIZURI.

3. HUPUNGUZA HUARIBIFU WA FIGO KWA KIASI FULANI

4. HUPUNGUZA MAGONJWA YA MOYO

Featured Post

FAIZA ZA KULA PAPAI

 _*Siri usioijua kuhusu utajiri wa tunda la papai katika kukulinda na magonjwa hatarishi kutokana na faida zake lukuki*_  Hizi ndizo FAIDA 1...