HABARI ZENU WADAU WA MAKALA ZANGU?
Leo nimeona nikushirikishe kuhusu UGONJWA WA HOMA YA INI
HOMA YA INI ni UGONJWA unaoambukizwa kwa njia ya VIRUSI ambavyo vikishaingia MWILINI hushambulia INI kabla ya kugeuka kuwa MARADHI SUGU.VIRUSI ivyo vinaitwa HBV - HEPATITIS B VIRUSES.
VIRUSI hivi husambazwa kwa njia ya DAMU au MAJIMAJI mengine ya MWILINI mfano MATE au JASHO.
UGONJWA huu kama haujatibiwa hutengeneza UVIMBE katika INI na kusababisha KANSA ya INI na baadaye KIFO.
JINSI UNAVYOAMBUKIZWA.
Katika maeneo hatari zaidi DUNIANI,virusi vya HEPATITIS B ( HBV ) kwa kawaida husambazwa kutoka kwa MAMA kwenda kwa MTOTO wakati wa kuzaliwa au kutoka kwa MTU mmoja hadi mwingine hususani nyakati za UTOTONI.
Kama ilivyo kwa UKIMWI virusi vya HOMA ya INI navyo huambukizwa kwa njia ya KUJAMIIANA ,MATE,JASHO, na mwingiliano wowote wa DAMU.
NJIA KUU ZA MAAMBUKIZI :-
- Kujamiiana bila kinga.
- Kunyonyana NDIMI ( Denda )
- MAMA mwenye Ugonjwa kumwambikiza MTOTO wakati wa kujifungua.
- Kuchangia DAMU isiyo salama.
- Kuchangia vitu vya ncha kali kama SINDANO ,WEMBE n.k
- Kuchangia MISWAKI .
- Kuchangia TAULO na mwenye Ugonjwa huo.
- Kubadilishana nguo au kukumbatiana wakati mkiwa mnavuja JASHO .
Tafiti zinaonesha kuwa VIRUSI hivi ni HATARI kuliko hata vya UKIMWI kwa sababu vinaweza kuishi NJE ya MWILI wa BINADAMU ( yaani nje ya mfumo wa damu ) kwa siku SABA.
VIRUSI vya UKIMWI ( VVU ) havina UWEZO wa kuishi NJE ya mfumo wa DAMU hata kwa DAKIKA moja.
Kutokana na USUGU wa HBV maana yake ni kwamba kama kirusi kipo kwenye NGOZI,kitaendelea kuwa HAI kwa siku SABA na katika kipindi hicho MTU anaweza kuambukizwa kwa njia ya DAMU au JASHO. Kwa wastani kirusi cha HBV kikishaingia MWILINI hupevuka ndani ya SIKU 75.Hata hivyo upo uwezekano wa kupevuka kati ya SIKU 30 hadi SIKU 180.Ndani ya SIKU 30 mpaka SIKU 60, MTU mwenye HBV anaweza kugundulika ikiwa atapimwa.
MTU mwenye HOMA ya INI ana wastani mdogo wa KUISHI kuliko mwenye UKIMWI.
DALILI ZA UGONJWA HUU.
WATU wengi hawaonyeshi DALILI yoyote.
Kwa maana hiyo MTU anaweza kuishi na HBV na kusababisha MAAMBUKIZI kwa WENGINE bila kugundulika.
Hata hivyo WATU wengine husumbuliwa na HOMA KALI na DALILI ambazo hudumu kwa wiki kadhaa. DALILI hizo ni:-
- Uchovu
- Kichefuchefu
- Mwili kuwa dhaifu
- Homa kali
- Kupoteza hamu ya kula
- Kupungua uzito
- Maumivu makali ya tumbo upande wa INI.
- Macho na ngozi kuwa ya njano.
- Mkojo mweusi.
Kwa WAGONJWA wengine, VIRUSI vya HEPATITIS B hukua hadi kusababisha INI kuharibika kabisa ( Cirrhosis of the liver ) au SARATANI ya INI ( liver cancer ).
KINGA.
- Chanjo
- Kutumia kinga wakati wa Kujamiiana.
- Kuacha Kuchangia vitu vya ncha kali.
- Kutochangia miswaki.
- Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu.
- Kutochangia damu isiyo salama.
No comments:
Post a Comment