Sunday, October 22, 2017

FAIDA ZA ZABIBU KIAFYA

 FAIDA ZA ZABIBU KIAFYA
#AfyaMwili

Zabibu ni matunda matamu yanayopendwa yakiwa na faida nyingi kiafya kwa mwili. Kuna zabibu za rangi ya kijani, nyekundu na kama nyeusi. Unaweza kula zabibu kama matunda, zabibu zilizokaushwa (raisin) au kama juisi ya zabibu. Zabibu hutumika sana kutengeneza mvinyo (wine) sehemu mbalimbali duniani.

Faida za zabibu kiafya hujumuisha kusaaidia kuondoa kukosa choo, mmeng’enyo wa chakula kwenda vizuri, kupunguza uchovu na kuzuia mtoto wa jicho.
Virutubisho Vilivyopo Ndani ya Zabibu

Kwa kila gramu 100 za zabibu zina wastani wa virutubishi vifuatavyo;

    Nishati kilokaro 69
    Wanga gramu 18.1
    Sukari gramu 15.48
    Kambakamba gramu 0.9
    Mafuta gramu 0.16
    Protini gramu 0.72

Vitamini

    Vitamini B1, B2, B3, B5, B6, B9
    Vitamini C
    Vitamin E
    Vitamin K

Madini

    Kalsiamu miligramu 10 mg
    Chuma miligramu 0.36
    Magneziamu miligramu 7mg
    Manganizi miligramu 0.071
    Sodiamu miligramu 2mg
    Potasiamu miligramu 191
    Fosforasi miligramu 20

Faida za Zabibu Kiafya


Zinatumika Kutibu Pumu

Zabibu zinasaidia kuongeza unyevunyevu kwenye njia ya hewa na hivyo kupunguza utokeaji wa pumu.
Huimarisha Mifupa

Madini ya shaba, chuma na manganizi yanapatikana kwa wingi kwenye zabibu, na madini haya ni sehemu ya kujenga mifupa imara na yenye afya. Kula zabibu mara kwa mara inasaidia kupunguza kutokea kwa mifupa kulainika kutokana na umri kuwa mkubwa. Pamoja na kuimarisha mifupa, madini haya husaidia mwili kufanya kazi vizuri.
Hulinda Dhidi ya Magonjwa ya Moyo

Zabibu huongeza nitric oxide kwenye damu ambayo huzuia damu kuganda, husaidia kuzuia mafuta kulundikana kwenye mishipa ya damu na ina kampaundi za flavonoids aina za resveratrol na quercetin ambazo husaidia kutoa sumu mwilini. Haya yote husaidia kupunguza hatari ya magonjwa moyo na shinikizo la damu.
Kusafisha Figo

*Zabibu zina viondoa sumu (antioxidants) ambazo husaidia kuondoa sumu (free radicals) kutoka kwenye figo, pia hupunguza tindikali ya uriki (uric acid) kwa kuongeza kiasi cha mokojo unaotengenezwa na figo.
Kupunguza Lehemu (cholesterol)

*Zabibu zina uwezo wa kupunguza lehemu(cholestrol) kwenye damu. Zina kampaundi kama pterostilbene ambazo zinadhaniwa kupunguza mafuta ya lehemu kwenye damu. Pia aina ya kampaundi iliyo kwenye ngozi ya zabibu ziitwazo saponins hupunguza unywonyaji wa lehemu kutoka kwenye utumbo.
Kupunguza Hatari ya Kupata Saratani

Kama tulivyoona hapo juu kampaundi zinazopatikana ndani ya zabibu kama resveratrol ambazo husaidia kuondoa sumu zinazoweza kuleta saratani mwilini. Baadhi ya kampaundi nyingine huzuia seli za saratani kukua na kuzaliana; kuimarisha mfumo wa kinga wa mwili.

Zabibu zilizokaushwa zina faida nyingi pia kama kuzuia choo kigumu, homa na kuongeza damu.
Hakikisha unaosha zabibu kwa maji safi ya moto kabla ya kuzila.
#AfyaMwili

Share makala hii iwafikie wengi

Whatsapp:0717064639
Email:afyamwili@gmail.com

Friday, October 13, 2017

IFAHAMU KANSA YA MLANGO WA KIZAZ KUANZIA VISABABISHI,DALILI NA JINSI YA KUJIKINGA

 KANSA(SARATANI) YA SHINGO YA KIZAZI.

Shingo ya kizazi(CERVIX) ni sehemu ya mfuko wa kizazi kuelekea kwenye njia ya uke.Sehemu hii ina kazi nyingi ikiwemo:1.Kupitisha mbegu za kiume kuelekea ktk mirija ya uzazi ili kupevusha yai.2.Kupitisha damu ya hedhi.3.Ndio mlango anaopita mtoto wakati wa kuzaliwa kutoka ktk mfuko wa uzazi hatimaye ukeni.
Kama zilivyosehemu zingine za mwili,sehemu nayo inaweza kupata maradhi ikiwemo kansa.
Ugonjwa huu uwaathiri wanawake wengi wa rika zote waliokatika umri wa kuzaa.Miaka ya nyuma kabla ya maambukizi ya Ukimwi kugundulika Kansa ya Shingo ya Kizazi ilikuwa ikiwapata zaidi wanawake wenye umri wa miaka 45 na kuendelea.Lakini miaka ya hivi karibuni mwanamke yeyote aliye katika umri wa kuzaa anaweza kupata tatizo hili.
SABABU YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.
Ugonjwa una sababishwa na virusi viitwavyo Human papiloma.Ambapo mtu anaweza kupatwa na hawa virusi wakati wa kujamiana na mtu mwenye maambukizi.
DALILI.
1.Kutokwa na majimaji au uchafu usio wa kawaida ukeni.
2.Kutokwa na damu ukeni hali ya kuwa siyo hedhi au umri wa kupata hedhi umekoma lakini anaona damu inatoka.
3.Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana.
4.Kutokwa na damu baada ya kujamiiana.
5.Kuwa na maumivu makali ya tumbo hasa chini kitovu au kwenye nyonga.
TABIA HATARISHI AU WALIOHATARINI
Je, ni tabia zipi hatarishi zinazoweza kupelekea kupata ugonjwa huu
1.Kuanza ngono mapema katika umri mdogo chini ya miaka 18
2.Uvutaji wa sigara
3.Kuwa na wapenzi wengi au kujamiiana na mtu mwenye wapenzi wengi
4.Matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula au kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi
5.Kutokula mboga za majani na matunda
6.Kuzaa mara kwa mara
7.Wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
TIBA.
Kansa ya shingo ya kizazi inatibika iwapo itagundulika mapema ikiwa katika hatua za mwanzo.
Saratani ya shingo ya kizazi inapogundulika katika hatua za mwisho, uwezekano wa kutibika unakuwa ni mdogo na gharama za matibabu zinakuwa kubwa!
Utagunduaje mapema kama una saratani ya shingo ya kizazi?
Kufanya uchunguzi wa shingo ya kizazi angalau mara 1 kwa mwaka
KUMBUKA KANSA HII NDIYO KANSA INAYONGOZA KUSABABISHA VIFO NCHINI.
WAHI HOSPITALI MAPEMA UNAPOHISI DALILI ZA UGONJWA HUU ILI UPATE MATIBABU.
Email:afyamwili@gmail.com
Whatsapp:0717064639



Featured Post

FAIZA ZA KULA PAPAI

 _*Siri usioijua kuhusu utajiri wa tunda la papai katika kukulinda na magonjwa hatarishi kutokana na faida zake lukuki*_  Hizi ndizo FAIDA 1...