Tuesday, November 12, 2024

AINA ZA KISUKARI

 AINA ZA KISUKARI


Kuna aina kuu mbili za kisukari

1. Kisukari kinachotegemea insulin(type 1 diabete)

2. Kisukari kisichotegemea insulin(type 2 diabete)


1. Kisukari kinachotegemea insulin:

Hii ni aina ya ugonjwa wa kisukari ambapo mwili hushindwa kutengeneza au hua una uhaba wa kichocheo aina ya insulin ambacho huwezesha mwili kutumia sukari. Lakini pia aina hii ya ugonjwa wa kisukari huchangiwa na ukosefu/upungufu wa madini aina ya potassiam.

Aina hii ya kisukari inaweza kudhibitiwa kwa utumiaji wa sindano za insulin pamoja na ulaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha potassiam.


2. Kisukari kisichotegemea insulin:

Hii ni aina ya ugonjwa wa kisukari ambapo kongosho huzalisha kichocheo aina ya insulin, lakini kichocheo hicho, hushindwa kuruhusu milango ya chembe hai za mwili(seli) kufunguka na kuruhusu sukari kuingia ili kwenda kuzalisha nguvu. Hali hii hutokana na athari mbali mbali za mazingira na ulaji mbovu.

Aina hii ya kisukari inaweza kudhibitiwa kwa kurekebisha aina za ulaji.


DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI

Zifuatazo ni miongoni mwa dalili za ugonjwa wa kisukari kiujumla.

- Kuhisi kiu sana/kunywa maji mengi.

- Kukojoa mara kwa mara.

- Kuhisi njaa mara kwa mara.

- Uchovu bila ya kufanya kazi.

- Kukosa nguvu.

- Kupungua uzito kusiko kwa kawaida.

- Kizunguzungu.

- Wanawake kuwashwa ukeni.

- Kupungua kwa nuru ya macho.

- Kupungua kwa nguvu za kiume.

- Ganzi sehemu za miguu na vidole.

- Kufanya majipu mwilini.


MADHARA YA UGONJWA WA KISUKARI

Ugonjwa wa kisukari hupelekea athari mbali mbali zikiwemo:-

- Kupungua kwa nuru ya macho na hata upofu.

- Figo hushindwa kufanya kazi zake vizuri.

- Kutopona kwa vidonda hasa sehemu za miguu na hata kukatwa kidole na mguu.

- Maradhi ya moyo.

- Kupoteza kwa hisia kwa mikono na miguu.

- Kupata kiharusi.

- Kupoteza nguvu za kiume.


ZINGATIO.

Ugonjwa wa kisukari unakingika na kudhibitika ikiwa tu, tutabadili mfumo mzima wa ulaji/virutubisho lishe na kubadili mienendo ya maisha.


Kwa makala za afya Usiache kufatilia page yetu 


Tuandikie ktk email yetu afyamwili@gmail.com 


Au waweza kutupata Whatsapp 0628873628


Karibuni

Saturday, October 26, 2024

FAIZA ZA KULA PAPAI


 _*Siri usioijua kuhusu utajiri wa tunda la papai katika kukulinda na magonjwa hatarishi kutokana na faida zake lukuki*_


 Hizi ndizo FAIDA 10 za kiafya za kula papai

1️⃣ Papai ni katika matunda yanayojenga afya sana kwenye mwili wa binadamu. Papai lina *vitamin C na vitamini A* kwa wingi pia kuna *potassium na folate.* Pia tafiti zinaonesha kuwa *antioxidant aina ya lycopene* iliyomo kwenye papai *husaidia katika kuzuia kupata saratani.* 


2. Tunda hili pia lina *vitamin B, vitamin E na vitamin K.* Pia lina *madini ya calsium (kashiam) potassium, mgnessium na copper.* Pia punje za papai ni *dawa kwa baadhi ya matatizo ya ini na figo.* Pia kwenye papai kuna *protelytic enzymes hii husaidia katika kuuwa bakteria na minyoo pamoja na wadudu wengine hatari ndani ya tumbo (mfumo wa kumeng’enya chakula).* 


3️⃣ Papai linatambulika kwa kuwa na *uwezo wa kuulinda mwili na maradhi ya uzee kama macho, misuli na kuzeeka kwa haraka.* Ndani ya papai kuna *Zeaxanthin hii ni anti oxidant ambayo inakazi ya kuchuja miale hatari ya jua.* Pa inaaminika kuwa *antioxidant hizi husaidia katika afya ya macho na husaidia katika kudhibiti kudhoofu kwa misuli.* 


4️⃣ Vilevile papai huaminika kusaidia kupunguza *hatari ya kuwa na ugonjwa wa pumu.* Hupunguza hatari ya kuugua pumu. Ndani ya papai kuna virutubisho vingi, lakini uwepo wa *beta-carotene ndani ya papai husaidia kwa wagonjwa wenye pumu.* 


5️⃣Ulaji wa antioxidanti zilizopo kwenye papai mfano *beta-carotene* *husaidia katika kupunguza athari za kupata maradhi ya saratani kwa vijana* . Ulaji wa tunda hili husaidia katika *kudhibiti upatikanaji wa saratani ya kwenye via vya uzazi hasa saratani ya korodani.* 

6. Pia papa Lina kiwango kikubwa Cha fibres (nyuzi na kambakamba) zinazosaidia kurahisisha mmeng'enyo wa chakula na kufanya mtumiaji kutopata choo kigumu (Constipation)

 *Hitimisho:* 

Nimalizie kwa kusema kuwa matunda ni dawa. Ni vyema kujitahidi kula matunda na mboga za majani mara kwa mara. Pia viungio vya mboga kama vitunguu, tangawizi, bamia na karoti viungio hivi ni muhimu sana.

Monday, November 13, 2017

MBINU KUMI ZA KUONGEZA WINGI WA MBEGU ZA KIUME(SPERM COUNT) NA FAHAMU VISABABISHI VINAVYOPELEKEA TATIZO HILI


 MBINU 10 ZA KUONGEZA WINGI WA MBEGU ZA KIUME (sperm count)

Mwanaume mwenye uwezo wa kuzalisha anahitaji kuwa na mbegu zisizopungua milioni 20, chochote chini ya hapa kinaweza kuwa sababu ya kutokutungisha ujauzito.

Ikitokea umegundulika kuwa na mbegu chache, ni nyepesi sana na hazina nguvu za kukimbia vya kutosha basi makala hii itakupa maelezo juu ya mbinu 10 zinazoweza kukusaidia kuongeza uwingi wa mbegu zako bila gharama yoyote.

Visababishi vya mbegu kuwa chache:

Kuna vitu vingi vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume, kwa bahati nzuri vingi ya vitu hivyo tunao uwezo wa kuvidhibiti kwa kupunguza matumizi yake.

Vitu hivyo ni pamoja na:

• Vifaa vya kieletroniki – Tafiti zimeonyesha vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa wingi na ubora wa mbegu kwa wanaume wengi miaka ya sasa kwani mionzi yake hupelekea joto lisilohitajika katika mifuko ya mbegu za kiume.

Vifaa hivi ni pamoja na simu na Kompyuta.

Unashauriwa kutokuweka simu ndani ya mfuko wako wa suruali kwa kipindi kirefu na kutokuweka kompyuta mpakato (laptop) kwenye mapaja yako wakati wote ukiitumia.

Ni mhimu pia kutokutumia masaa mengi kutwa nzima ukiwa kwenye kompyuta.

• Vifaa vya Intaneti visivyotumia waya – Siku hizi tofauti na zamani, kuna teknolojia mpya imeingia ya kuunganisha intaneti kwa kutumia vifaa visivyotumia waya (wireless internet) au kwa lugha nyepesi hujulikana kama Wi-Fi.

Vifaa hivi vinapunguza wingi wa mbegu, uwezo wa mbegu kukimbia na kuharibu muundo asili wa mbegu kwa ujumla (DNA fragmentation).

Wanaume wenye tatizo la uzazi wanashauriwa kutotumia aina hii ya vifaa vya kuunganishia intaneti kwenye kompyuta zao na vile vile kutokuweka simu kwenye mifuko yao ya mbele ya suruali.

• Uvutaji wa Sigara – Uvutaji sigara, bangi na bidhaa nyingine za tumbaku huharibu ubora wa mbegu za kiume.

Hilo halihitaji majadiliano. Habari njema ni kuwa madhara yaliyosababishwa na uvutaji sigara yanaweza kurekebishika ikiwa tu utaamua kuacha kuvuta.

Huhitaji dawa kuacha kuvuta sigara, unahitaji kuamua tu kwamba sasa basi na hakuna lisilowezekana kwa mtu mwenye maamuzi na mwenye ndoto za maisha mazuri ya kiafya.

Vingine vya kuviacha ni pamoja na bangi na madawa mengine yote ya kulevya.

• Viuavijasumu na homoni katika vyakula – Viuavijasumu (pesticides) vinavyotumika katika mazao mbalimbali mashambani miaka ya sasa ni sababu mojawapo ya tatizo la homoni kutokuwa sawa kwa wanaume wengi.

Kwenye bidhaa nyingi za maziwa za viwandani sasa huongezwa homoni kama vile homoni ya estrogeni ambazo hazihitajiki katika mwili wako.

Vyote hivi vina madhara katika afya ya mwanaume.

• Vyakula vyenye soya – Vyakula vyenye soya ndani yake hasa vile vya viwandani kama vile maziwa ya soya, burger za soya nk si vizuri kwa afya ya uzazi ya mwanaume.

Vinasemwa moja kwa moja kuathiri ubora wa homoni ya testosterone homoni mhimu sana kwa afya ya uzazi wa mwanaume
.
• Unywaji pombe – Katika moja ya utafiti kwa wanaume wenye mbegu zenye ubora wa chini, matumizi ya kupitiliza ya unywaji pombe yalionyesha kuhusika na kupungua kwa mbegu za kawaida yaani mbegu nzuri zinazofaa kwa ajili ya uzazi.

• Matumizi ya vifaa vya plastiki – Wakati kifaa cha plastiki kinapowekewa chakula cha moto hutoa kitu kijulikanacho kama ‘xenohormones’ ambacho huigiza kama ni ‘estrogen’ ndani ya mwili na hivyo kupelekea matatizo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume.

• Joto kupita kiasi (Hyperthermia) – Mifuko ya mbegu za uzazi ya mwanaume inahitaji joto la chini kidogo ya lile joto la mwili kwa ujumla ili mbegu zibaki na afya.

Inasemekana kuwa hii ndiyo moja ya sababu viungo vya uzazi vya mwanaume vipo karibu nje kabisa ya mwili wake.

Joto linajulikana wazi kuharibu ubora wa mbegu na hivyo itakuwa vizuri kuepuka mazingira ambayo yanaweza kusabbaisha joto la moja kwa moja kwenye viungo vya uzazi vya mwanaume ikiwemo kuepuka kuvaa nguo za ndani zinazobana sana.

• Mfadhaiko (Stress) – Mfadhaiko au stress inaweza kuleta majanga makubwa katika homoni na kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa mbegu za kiume.

Stress inahusika sana na tatizo la ugumba kwa wanaume wengi, na moja ya sababu ya stress hii ni ile hamu yenyewe ya kuwa na mtoto inapokujia kila mara kichwani.

Vile vile kuna presha kutoka kwa wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwamba kwanini huzai.

Hivi vyote ukiviweka kichwani na kuviwaza kila mara ni rahisi kwako kupatwa na tatizo la kupungua kwa mbegu na uzazi kwa ujumla.

Kuwa na amani, mwamini Mungu kwamba siku yako ipo, just relax kila kitu kina muda wake.

• Aina ya chakula unachokula – Chanzo kingine cha kuwa na mbegu chache au zisizokuwa na afya ni kutokula chakula sahihi na cha kutosha kila siku.

Kwa afya bora kabisa ya uzazi mwanaume anahitaji vyakula vyenye madini ya zinki (zinc) kwa wingi, selenium, Vitamin E, folic acids, Vitamini B12, Vitamini C na vyakula mbalimbali vinavyoondoa sumu mwilini (antioxidants).

• Kujichua (punyeto) – Hili ni janga kubwa miongoni mwa wanaume wengi wengi karibu kote duniani. Tabia hii ukiianza huwa ni vigumu kuiacha na ni rahisi sana kugeuka kuwa teja wa punyeto.

Madhara makubwa ya kujichua ni pamoja na kupungua kwa kasi kwa uwingi wa mbegu kwa mwanaume pia nguvu zake kwa ujumla na hivyo kutokuwa na uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito.

Vingine ni pamoja na kuendesha baiskeli masaa mengi, kukosa muda wa mazoezi ya viungo na kutoshiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu.

MBINU 10 ZA KUONGEZA WINGI WA MBEGU ZA KIUME (sperm count)

1. Kula lishe bora

Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula vingi vya kisasa havina uwezo wa kuongeza uwingi wa mbegu.

Kama utarekebisha tu aina ya chakula unachokula kunaweza kupelekea kutibu tatizo lako.

Punguza matumizi ya sukari na vyakula vya ngano. Ongeza zaidi matunda, mboga za majani na mafuta yenye afya. 

Hii inaweza kusaidia kutibu tatizo lako la kuwa na mbegu chache kwa haraka sana.

Endelea kusoma zaidi hii makala hapa chini.

2. Acha kutumia vinywaji au vyakula vyenye kaffeina

Kama una tatizo la kuwa na mbegu chache ni vizuri ukaacha kutumia vinywaji au vyakula vyote vyenye kaffeina kwanza.

Navyo ni pamoja na chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi zote, malta, redbull, chokoleti nk.

Hivi vitu vyenye kaffeina ni sababu ya kupungua kwa uwingi wa mbegu za kiume.

3. Tumia kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu ni maajabu ya Mungu mwenyewe. Kitunguu swaumu kina Selenium na pia kinaondoa sumu mwilini vitu viwili mhimu kwa ajili ya kuongeza spidi ya mbegu.

Kitunguu swaumu kina kitu kingine kiitwacho ‘Allicin’ ambacho huongeza msukumo wa damu kwenda kwenye uume.

Ongeza kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika.

Pia unaweza kutafuna punje 2 au 3 kila unapoenda kulala au unaweza kukatakata hizo punje 3 vipande vidogo vido (chop) kisha unywe na maji.

Usizidishe zaidi ya punje 3 kwa siku.

4. Kula ndizi

Ndizi hazifanani tu na uume kama unavyoweza kuwaza bali pia ni chakula kizuri kwa ajili ya afya ya uume wako. Ndizi zina kimeng’enya kimoja adimu sana kijulikanacho kama ‘Bromeliad’ ambacho husaidia kuziweka sawa homoni zinazohusiana na tendo la ndoa.

Ndizi pia zina Magnesiamu, Vitamini B1 na Vitamini C, vitu ambavyo ni mhimu sana kwa ajili ya kutengeneza mbegu za kiume.

5. Kula mbegu za maboga

Mbegu za maboga zina kiasi kingi ccha madini ya Zinki ambayo ni mhimu katika kuundwa au kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya testosterone.

Pia zina vitamini B, C, D, E,  na K ambazo zote ni vitamini mhimu katika kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa na nguvu kwa ujumla.

Pia mbegu za maboga zina kalsiamu, potasiaumu, niacin na phosphorous.

6. Kula zaidi mboga za majani

Mama alikuwa sahihi kumbe ingawa nilikuwa nachukia nikikuta mboga majani badala ya nyama nikirudi kutoka shule.

Mboga za majani zinapunguza homoni ya ‘estrogen’ na hivyo kufanya homoni ya ‘testosterone’ ipatikane kwa wingi na kiurahisi zaidi na hivyo mbegu zako ziweze kuongezeka bila vipangamizi vyovyote. 

7. Kunywa maji mengi kila siku

Hili ni suluhisho rahisi lisilohitaji gharama wala ugomvi wowote kukuelewesha. Mwenyewe unajua kuwa maji ni uhai na kuwa asilimia 75 ya mwili wako ni maji, sasa kama huna tabia ya kunywa maji ya kutosha kila siku sijuwi unategemea miujiza kutoka wapi.

Huhitaji kusikia kiu au mpaka upate hamu ya kunywa maji bali hili ni jambo la lazima kwamba huwezi kukaa bila kunywa maji halafu ubaki na afya bora.

Mbegu zako zimetengenezwa kwa maji, zipo kwenye hali ya kimiminika.

Kutokunywa maji ya kutosha kila siku kuna uhusiano wa moja kwa moja na kupungua kwa uwingi wa mbegu.

Kama utatekeleza mengine yote niliyoelekeza hapo juu halafu ukasahau kunywa maji hesabu umeshachemka tayari.

Kutegemea na uzito wako unaweza kuhitaji maji lita 2 mpaka 3 kila siku.

8. Tumia vyakula vyenye folic asidi kwa wingi

Katika utafiti mmoja wanaume walioongeza utumiaji wa folic asidi na zink waliongeza uwingi wa mbegu zao kwa zaidi ya asilimia 74 kwa muda wiki 2 tu.

Vyakula hivi ni pamoja na tunda la parachichi na karoti.

Hivyo isipite siku bila kula parachichi 1 kutafuna karoti moja kama una tatizo la mbegu chache.

Vingine ni pamoja na mbegu za maboga, ufuta, alizeti, maharage, chungwa, papai, bamia nk

9. Mayai

Mayai yanachukuliwa kama mbadala wa uhakika zaidi katika kuongeza uwingi wa mbegu pamoja na kuongeza spidi au kasi yake. Yana vitamini E nyingi na protini ya kutosha vitu viwili mhimu katika kuongeza mbegu.

Mayai yanafanya kazi nyingine mhimu nayo ni kuzilinda seli za mbegu za kiume kutoshambuliwa na vijidudu nyemelezi kirahisi ambavyo vinaweza kuwa sababu ya kupungua kwa mbegu zako.

Viinilishe vilivyomo kwenye mayai vinafanya kazi ya ziada ya kuzifanya mbegu zenye afya zaidi na zenye nguvu zaidi jambo ambalo ni mhimu kwa ajili ya uzazi kwa upande wa mwanaume.

Kumbuka ni mayai ya kuku wa kienyeji tu yanayofaa kwa kazi hii. Kila siku kula mayai mawili mpaka matatu kama una tatizo hili la kuwa na mbegu chache.

10. Spinach

Folic asidi ni kitu mhimu katika kuongezeka kwa mbegu za kiume. Spinachi na mboga nyingine za majani zenye rangi ya kijani ni mhimu kwa ajili hii sababu ya vitamini na kuweka sawa usawa wa ‘folate’ kwenye mfumo wako wa mwili.

Kama folate ipo chini kuna uwezekano ukawa unatengeneza mbegu zisizo na umbile linalotakiwa kwa uzazi na hiyo hupelekea shida na matatizo mengine ya uzazi upande wa mwanamke (birth defects) kama ujauzito kutoka mara tu mimba inapotungwa.



Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine.





Tuandikie ujumbe ufupi afyamwili@gmail.com au waweza kuwasiliana nasi kupitia whatsapp number 0717064639 

Sunday, October 22, 2017

FAIDA ZA ZABIBU KIAFYA

 FAIDA ZA ZABIBU KIAFYA
#AfyaMwili

Zabibu ni matunda matamu yanayopendwa yakiwa na faida nyingi kiafya kwa mwili. Kuna zabibu za rangi ya kijani, nyekundu na kama nyeusi. Unaweza kula zabibu kama matunda, zabibu zilizokaushwa (raisin) au kama juisi ya zabibu. Zabibu hutumika sana kutengeneza mvinyo (wine) sehemu mbalimbali duniani.

Faida za zabibu kiafya hujumuisha kusaaidia kuondoa kukosa choo, mmeng’enyo wa chakula kwenda vizuri, kupunguza uchovu na kuzuia mtoto wa jicho.
Virutubisho Vilivyopo Ndani ya Zabibu

Kwa kila gramu 100 za zabibu zina wastani wa virutubishi vifuatavyo;

    Nishati kilokaro 69
    Wanga gramu 18.1
    Sukari gramu 15.48
    Kambakamba gramu 0.9
    Mafuta gramu 0.16
    Protini gramu 0.72

Vitamini

    Vitamini B1, B2, B3, B5, B6, B9
    Vitamini C
    Vitamin E
    Vitamin K

Madini

    Kalsiamu miligramu 10 mg
    Chuma miligramu 0.36
    Magneziamu miligramu 7mg
    Manganizi miligramu 0.071
    Sodiamu miligramu 2mg
    Potasiamu miligramu 191
    Fosforasi miligramu 20

Faida za Zabibu Kiafya


Zinatumika Kutibu Pumu

Zabibu zinasaidia kuongeza unyevunyevu kwenye njia ya hewa na hivyo kupunguza utokeaji wa pumu.
Huimarisha Mifupa

Madini ya shaba, chuma na manganizi yanapatikana kwa wingi kwenye zabibu, na madini haya ni sehemu ya kujenga mifupa imara na yenye afya. Kula zabibu mara kwa mara inasaidia kupunguza kutokea kwa mifupa kulainika kutokana na umri kuwa mkubwa. Pamoja na kuimarisha mifupa, madini haya husaidia mwili kufanya kazi vizuri.
Hulinda Dhidi ya Magonjwa ya Moyo

Zabibu huongeza nitric oxide kwenye damu ambayo huzuia damu kuganda, husaidia kuzuia mafuta kulundikana kwenye mishipa ya damu na ina kampaundi za flavonoids aina za resveratrol na quercetin ambazo husaidia kutoa sumu mwilini. Haya yote husaidia kupunguza hatari ya magonjwa moyo na shinikizo la damu.
Kusafisha Figo

*Zabibu zina viondoa sumu (antioxidants) ambazo husaidia kuondoa sumu (free radicals) kutoka kwenye figo, pia hupunguza tindikali ya uriki (uric acid) kwa kuongeza kiasi cha mokojo unaotengenezwa na figo.
Kupunguza Lehemu (cholesterol)

*Zabibu zina uwezo wa kupunguza lehemu(cholestrol) kwenye damu. Zina kampaundi kama pterostilbene ambazo zinadhaniwa kupunguza mafuta ya lehemu kwenye damu. Pia aina ya kampaundi iliyo kwenye ngozi ya zabibu ziitwazo saponins hupunguza unywonyaji wa lehemu kutoka kwenye utumbo.
Kupunguza Hatari ya Kupata Saratani

Kama tulivyoona hapo juu kampaundi zinazopatikana ndani ya zabibu kama resveratrol ambazo husaidia kuondoa sumu zinazoweza kuleta saratani mwilini. Baadhi ya kampaundi nyingine huzuia seli za saratani kukua na kuzaliana; kuimarisha mfumo wa kinga wa mwili.

Zabibu zilizokaushwa zina faida nyingi pia kama kuzuia choo kigumu, homa na kuongeza damu.
Hakikisha unaosha zabibu kwa maji safi ya moto kabla ya kuzila.
#AfyaMwili

Share makala hii iwafikie wengi

Whatsapp:0717064639
Email:afyamwili@gmail.com

Friday, October 13, 2017

IFAHAMU KANSA YA MLANGO WA KIZAZ KUANZIA VISABABISHI,DALILI NA JINSI YA KUJIKINGA

 KANSA(SARATANI) YA SHINGO YA KIZAZI.

Shingo ya kizazi(CERVIX) ni sehemu ya mfuko wa kizazi kuelekea kwenye njia ya uke.Sehemu hii ina kazi nyingi ikiwemo:1.Kupitisha mbegu za kiume kuelekea ktk mirija ya uzazi ili kupevusha yai.2.Kupitisha damu ya hedhi.3.Ndio mlango anaopita mtoto wakati wa kuzaliwa kutoka ktk mfuko wa uzazi hatimaye ukeni.
Kama zilivyosehemu zingine za mwili,sehemu nayo inaweza kupata maradhi ikiwemo kansa.
Ugonjwa huu uwaathiri wanawake wengi wa rika zote waliokatika umri wa kuzaa.Miaka ya nyuma kabla ya maambukizi ya Ukimwi kugundulika Kansa ya Shingo ya Kizazi ilikuwa ikiwapata zaidi wanawake wenye umri wa miaka 45 na kuendelea.Lakini miaka ya hivi karibuni mwanamke yeyote aliye katika umri wa kuzaa anaweza kupata tatizo hili.
SABABU YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.
Ugonjwa una sababishwa na virusi viitwavyo Human papiloma.Ambapo mtu anaweza kupatwa na hawa virusi wakati wa kujamiana na mtu mwenye maambukizi.
DALILI.
1.Kutokwa na majimaji au uchafu usio wa kawaida ukeni.
2.Kutokwa na damu ukeni hali ya kuwa siyo hedhi au umri wa kupata hedhi umekoma lakini anaona damu inatoka.
3.Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana.
4.Kutokwa na damu baada ya kujamiiana.
5.Kuwa na maumivu makali ya tumbo hasa chini kitovu au kwenye nyonga.
TABIA HATARISHI AU WALIOHATARINI
Je, ni tabia zipi hatarishi zinazoweza kupelekea kupata ugonjwa huu
1.Kuanza ngono mapema katika umri mdogo chini ya miaka 18
2.Uvutaji wa sigara
3.Kuwa na wapenzi wengi au kujamiiana na mtu mwenye wapenzi wengi
4.Matumizi ya mafuta mengi kwenye chakula au kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi
5.Kutokula mboga za majani na matunda
6.Kuzaa mara kwa mara
7.Wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
TIBA.
Kansa ya shingo ya kizazi inatibika iwapo itagundulika mapema ikiwa katika hatua za mwanzo.
Saratani ya shingo ya kizazi inapogundulika katika hatua za mwisho, uwezekano wa kutibika unakuwa ni mdogo na gharama za matibabu zinakuwa kubwa!
Utagunduaje mapema kama una saratani ya shingo ya kizazi?
Kufanya uchunguzi wa shingo ya kizazi angalau mara 1 kwa mwaka
KUMBUKA KANSA HII NDIYO KANSA INAYONGOZA KUSABABISHA VIFO NCHINI.
WAHI HOSPITALI MAPEMA UNAPOHISI DALILI ZA UGONJWA HUU ILI UPATE MATIBABU.
Email:afyamwili@gmail.com
Whatsapp:0717064639



Tuesday, September 19, 2017

FAIDA KUMI ZA TANGO

 
FAIDA ZA TANGO
1.    Tango ni chanzo kizuri cha vitamin B.
2.    Tango huupa mwili maji na vitamin. Asilimia 95 ya tango ni maji hivyo huupa mwili maji na kuusaidia kuondoa sumu mwilini kwani pia lina vitamin karibu zote ambazo mwili huhitaji kila siku.

3.    Tango pia hutumika kwenye matunzo ya ngozi/urembo ambapo huwekwa usoni na kuondoa vimbe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea kwani tango lina virutubisho vya kuondoa vimbe hizi na pia lina silicon na sulfur ambazo husaidia ukuwaji wa nywele.

4.    Tango lina virutubisho kama lariciresinol, pinoresinol na secoisalariciresinol ambavyo kulingana na tafiti mbali mbali za magonjwa ya kansa husaidia kupunguza aina mbali mbali za kansa kama kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa wanawake, kansa ya kizazi kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume.

5.    Tango husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani.

6.    Tango huondoa hangover kwa watumiaji wa pombe kwani lina vitamin B ambazo husaidia kupunguza ukali wa maumivu ya kichwa pale unapoamka asubuhi ila unatakiwa kula kabla ya kulala ili uamke ukiwa vizuri.

7.    Tango husaidia kupungua uzito na mmeng’enyo uende vizuri. Kutokana na kiasi kidogo cha sukari kilichopo kwenye tango na kiasi kikubwa cha maji, tango ni tunda sahihi kukusaidia upungue uzito. Kiasi cha maji kilichopo kwenye tango na Kamba Kamba zake huusaidia mwili kuondoa sumu katika mfumo wa chakula na kusaidia mmeng’enyo wa chakula. Unapokula tango kila siku pia hukusaidia wewe mwenye choo kigumu au usiyepata choo kabisa kwa muda mrefu kuondokana na tatizo hilo.

8.    Tango husaidia wagonjwa wa kisukari, hupunguza mafuta mafuta kwenye mishipa ya damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu aina zote mbili (Low and high blood pressure). Tango lina hormone ambayo huhitajika kwenye chembechembe za kongosho (pancreatic cells) ilikuweza kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye mwili hivyo kuwasaidia wagonjwa wa kisukari. Pia watafiti wamegundua kuwa kuna kirutubisho kiitwacho sterol kwenye tango ambacho husaidia kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu. Tango lina kiwango kikubwa cha potassium, magnesium na Kamba Kamba ambazo husaidia sana kudhibiti shinikizo la damu aina zote yani high blood pressure na low blood pressure.

9.    Husaidia afya ya viungo, huondoa gout na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis). Tango ni chanzo kizuri cha silica ambayo inafahamika kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha viunganishi vya viungo (connective tissue). Pia tango lina Vitamin A, B1, B6, C & D, Folate, Calcium, Magnesium na potassium ambavyo hufanya tango linapochanganywa na juice ya karoti huweza kutibu gout na baridi ya yabisi (arthritis) kwa kupunguza kiwango cha tindikali kwenye mkoo (Uric acid).

10.    Kutokana na maji na virutubisho vilivyopo kwenye tango, tunda hili husaidia kupunguza homa pale inapopanda.

 Nadhani tutakuwa tumeelimika kwa kufahamu umhimu wa tunda aina ya tango ikiwa tunda hili halivutii kula kwa kuwa halina radha nzuri sana pia halina harufu inayosikia kuwa hili ni Tango  kwa kukazia tango lina asilimia kubwa ya maji.

Zingatia Madini ya Potassium yanayopatikana katika matango ndicho chakula cha moyo kwa sababu huwezesha moyo kupiga mapigo katika hali ya kawaida. Ulaji wa matunda na vyakula vyenye kiwango kikubwa cha potassium kama tango ni muhimu sana hasa kwa mtu mwenye tatizo la moyo, shinikizo la chini la damu.

Sunday, September 3, 2017

SABABU ZINAZOPELEKEA WANAWAKE KUKOSA HEDHI

HIZI NDIZO SABABU ZA WANAWAKE KUKOSA HEDHI.

Wengi wanafahamu kwamba mwanamke akipata mimba hawezi kuziona siku zake za hedhi bila kujua kuwa ziko sababu nyingine zinazoweza kusababisha jambo hilo.
Kwa kawaida kitendo cha mwanamke kuacha kupata hedhi kitaalam huitwa Menopause anapofikisha umri wa miaka 42 - 55 na kuendelea.
Leo nitazieleza sababu nje ya utaratibu huo wa kimaumbile unaoweza kumfanya mwanamke asipate hedhi na moja kubwa ni tabia ya maisha yake ya kila siku, yaani vyakula anavyokula (life style).

MAAMBUKIZI YA WADUDU.
Maambukizi ya magonjwa tofauti yaweza sababisha mwanamke asipate kuona siku zake. Magonjwa yale yana vuruga mfumo wa utoaji wa hormone katika mwili wa mwanamke. eg PID (pelvic inflamatory disease, gono etc

SIGARA
Tatizo moja kubwa ambalo huwakumba wanawake wanaovuta sigara ni kukosa hedhi au kuharakisha kutopata hedhi miaka miwili kabla ya wakati au umri wa miili yao kufanya hivyo.

UNENE
Wanawake wengine hukumbwa na tatizo hilo kutokana na kuongezeka uzito. Imethibitika kuwa uzito ukiwa mkubwa kwa wanawake unasababisha kuingia katika hatua za kuacha kupata hedhi kwa kuchelewa kwa mwaka mmoja zaidi ikilinganishwa na wanawake ambao hawana uzito mkubwa. Kitaalam hali hiyo inatokana na uingilianaji wa mafuta (kwa watu wanene au walio na uzito uliopitiliza) na homoni za kujamiiana yaani Sex homones.
Kama una tatizo la uzito mkubwa wasiliana nasi whatsapp 0622925000 tutakupatia mwongozo wa kupunguza uzito au dawa ya kupunguza mafuta mabaya mwilini kwa haraka.

ULEVI
Wanawake walevi wa pombe yaani wanaokunywa pombe kila siku nao wapo kwenye hatari ya kukumbwa na tatizo hili. Lakini walio katika hatari zaidi ni wale wenye umri kati ya miaka 25 na 49, hawa wanaweza kufunga hedhi kama wataendelea na tabia hiyo ya unywaji wa pombe kila siku.

KUTOKULA NYAMA Wengine ni wanawake ambao wanafanya mazoezi mazito mara kwa mara na wenye umri kati ya miaka 39 na 49 au wasiokula nyama au vyakula vinavyotokana na nyama (vegetarian) nao wamo katika hatari ya kukosa kuona siku zao za hedhi. Wengi wa wanawake wanaopatwa na tatizo hili hukumbwa pia na tatizo la kuchelewa kuacha kupata hedhi kama inavyotakiwa wakiwa katika umri unaotakiwa na hali hiyo huwahatarisha kwani wanaweza kukumbwa na hatari ya kupata saratani ya matiti.
Menopause kama tulivyoeleza hapo juu, ni hatua ya kuacha kupata hedhi ambayo hutokea wakati mwanamke akiwa na umri wa miaka 42-55 na huambatana na usitishwaji wa kutolewa kwa mayai ya uzazi, kupungua kwa kiwango cha homoni za kujamiiana, hivyo kusababisha kupungua kwa hamu ya kujamiiana kwa mwanamke. Hali hiyo husababisha tupu za mwanamke kuwa kavu, nywele kuwa nyembamba, matatizo wakati wa kulala, matiti kusinyaa na kupata hedhi bila mpangilio kabla ya kuacha kupata hedhi kabisa.

USHAURI
Mwanamke yeyote ambaye ataona dalili au kutopata hedhi yake muda muafaka ni vyema akaenda kumuona daktari ili afanyiwe uchunguzi na kama ataonekana ana tatizo la kiafya litapatiwa ufumbuzi.

Whatsapp:0717064639
Email:afyamwili@gmail.com

Featured Post

FAIZA ZA KULA PAPAI

 _*Siri usioijua kuhusu utajiri wa tunda la papai katika kukulinda na magonjwa hatarishi kutokana na faida zake lukuki*_  Hizi ndizo FAIDA 1...