Friday, June 30, 2017

CHANZO CHA MIMBA KUHARIBIKA NA DALILI ZAKE

HABARI ZENU WADAU!!

LEO NATAKA NIZUNGUMZIE
CHANZO CHA KUHARIBIKA KWA MIMBA MARA KWA MARA

KUHARIBIKA kwa MIMBA ni TATIZO linalowapata WANAWAKE wengi.

Si TATIZO linalowapata WANAWAKE MASIKINI TU ,hata MATAJIRI linawakumba.

MIMBA hutoka ikifikisha WIKI 36 hadi WIKI 38 wakati MTOTO anakuwa karibu KUZALIWA.

WENGI wenye MATATIZO haya wamekuwa wakitafuta MATIBABU hospitalini, kwenye MAOMBI maalum na hata kwa WAGANGA wa KIENYEJI .

SABABU za MIMBA kuharibika mara kwa mara KITAALAM hazijulikani ila kuna VYANZO vinavyojulikana kusaidia MIMBA kutoka.

Mbali na MIMBA zinazotolewa KIHARAMU, sababu za MIMBA zinazotoka bila kulazimishwa zinatajwa kuwa ni MAUMBILE ya KURITHI kwa maana ya kuwa na VINASABA ambavyo si vya KAWAIDA na kwa hiyo KIUMBE kinakuwa katika HALI ambayo KWA ASILI MIMBA haiwezi KUKUA na kama itakua na MTOTO kuzaliwa basi MTOTO huyo atakuwa na MATATIZO ya AJABU ya KIMAUMBILE na AKILI. Ni kwa SABABU hiyo MIMBA huharibika na kutoka yenyewe.

SABABU ya PILI ni KUTOKUA kwa YAI lililorutubishwa. Katika UUMBAJI.

YAI hukutana na MBEGU ya MWANAUME na MCHAKATO wa KIUMBE kukua huanza kwa YAI KUJITENGA mara MBILI .
UPANDE mmoja hutengeneza KONDO la NYUMA na KIFUKO cha kutunza MAJI na SEHEMU ya PILI hutengeneza KIUMBE au MTOTO .
HAPA hutokea SEHEMU ya KONDO la NYUMA ikiendelea KUKUA wakati SEHEMU ya MTOTO HAIKUI kabisa.

Katika MAZINGIRA kama haya,kama MAMA hajafanya VIPIMO vinavyoweza KUANGALIA moja kwa moja, anaweza kuendelea KUJIDANGANYA kama ni MJAMZITO kwani KIPIMO cha MKOJO kinaweza kuendelea KUONYESHA kuwa MAMA ni MJAMZITO.
Hata hivyo bado UJAUZITO utapotea kabla ya WIKI ya 24.

UVUTAJI wa SIGARA na UNYWAJI wa POMBE kupita KIASI wakati wa UJAUZITO huchangia MIMBA kuharibika.

Vilevile MSONGO wa MAWAZO na UKOSEFU wa LISHE huchangia kwa kiasi KIKUBWA UHARIBIKAJI wa UJAUZITO .

MAGONJWA yanayoathiri MWILI wa MAMA TUMBONI kama vile MALARIA , KASWENDE , na kadhalika.

DALILI za MIMBA KUHARIBIKA zinaanza na MJAMZITO kutokwa na MATONE ya DAMU na kupata MAUMIVU ya TUMBO chini ya KITOVU .

WAJAWAZITO wengine wanaweza KUTOKWA na DAMU bila KUHISI MAUMIVU ya TUMBO kabisa.

ASILIMIA kubwa ya MIMBA kuharibika hutokea katika KIPINDI cha AWALI kabisa cha UJAUZITO au NDANI ya WIKI 14 za UJAUZITO .

WANAWAKE wengi aidha kwa UELEWA MDOGO au DHARAU, hupuuza DALILI za KUTOKWA DAMU hasa kama ni KIDOGO huchelewa kwenda kumuona DAKTARI na MATOKEO yake MIMBA huharibika wakati ingeweza KUZUILIKA .

Iwapo MIMBA zinatoka bila KUWA na SABABU inayojulikana unatakiwa ufanyiwe UCHUNGUZI wa MAGONJWA ya KURITHI na MAGONJWA mengine yanayosabaisha MIMBA kuharibika.

ENDELEA KUWA NAMI MAKALA IJAYO TUTAJUA JINSI YA KUFANYA ILI MIMBA ISIHARIBIKE

Tuesday, June 27, 2017

UGONJWA WA MOYO [CORONARY HEART DISEASE]

HABARI ZENU WADAU WA MAKALA ZANGU ?

Leo nimeona nikushirikishe kuhusu
UGONJWA WA MOYO ( Coronary heart disease )

MAGONJWA ya MOYO yamezidi sana siku hizi.
Tatizo hili huanza katika MISHIPA ya DAMU ,na huweza kuendelea mpaka kuanza kuziba MISHIPA hiyo.Hii hufuatiwa na MOYO kukosa HEWA safi (Oxygen) kwa kiasi kinachotakiwa kwa sababu MISHIPA ya kupitisha DAMU imeziba na DAMU ndiyo inayopeleka HEWA ya OKSIJENI kwenye MOYO .

TAFITI mbalimbali zinaonyesha UGONJWA wa MOYO huanza kumwandama MTU pale MAMBO fulani yanaposababisha sehemu ya ndani ya KUTA za MISHIPA ya DAMU kuharibiwa.
MAMBO hayo fulani ni pamoja na kuwepo kiwango KIKUBWA cha aina fulani cha  MAFUTA pamoja na LEHEMU katika DAMU.

CHANZO kingine KIKUBWA ni kutozingatia utaratibu BORA wa ULAJI .Hii ni moja ya MAMBO yanayoongeza uwezekano wa MTU kupata MAGONJWA ya MOYO .

Mfano ULAJI wa VYAKULA vyenye MAFUTA mengi, VYAKULA vyenye SUKARI nyingi, CHUMVI nyingi na LEHEMU nyingi.
Wakati huo ULAJI wa MBOGAMBOGA na MATUNDA ukiwa ni wa KIWANGO cha CHINI.
Pia kuwa na UZITO uliozidi nalo ni TATIZO linaloweza kukusababishia UGONJWA wa MOYO.
Pia UVUTAJI wa SIGARA au UTUMIAJI tumbaku.
Kutofanya MAZOEZI kila siku japo nusu saa SHINIKIZO kubwa la DAMU (high blood pressure),UGONJWA wa KISUKARI na kadhalika.

LEHEMU inahitajika MWILINI lakini kwa kiasi KIDOGO .Hata  hivyo huwezi kujua una LEHEMU nyingi kupita kiasi MWILINI mpaka upime (inatakiwa iwe chini ya 200mg/dl).

Kiasi KIKUBWA cha LEHEMU mwilini husababisha mkusanyiko wa MAFUTA katika MISHIPA ya DAMU.

Punguza HATARI hii kwa kupunguza utumiaji wa MAFUTA yanayotokana na WANYAMA ikiwa ni pamoja na NYAMA iliyonona (nyama ya mafuta),MAZIWA yenye MAFUTA mengi (whole milk),JIBINI (cheese),NGOZI ya KUKU na SIAGI .

Pia ni VIZURI kupunguza ULAJI wa MAYAI , NYAMA (isizidi nusu kilo kwa wiki),MAFUTA tumia kwa kiasi kidogo.
Ongeza MATUMIZI ya NAFAKA hasa zile ZISIZONG'ARISHWA ( whole grains ) kama UNGA wa DONA na kadhalika. ONGEZA pia MATUMIZI ya aina za VYAKULA jamii ya kunde,maharage,mbogamboga na matunda.

Fanya MAZOEZI japo dakika 30 kila SIKU .
Epuka MATUMIZI ya POMBE kupita kiasi pamoja na UVUTAJI wa sigara/tumbaku kwani VITU hivi vina MADHARA katika MOYO na MISHIPA ya DAMU .
Epuka HASIRA ,shinikizo la AKILI na SONONA .

KIUJUMLA ,wingi wa LEHEMU unakadiriwa kusababisha VIFO vya WATU takribani MILIONI 2.6 DUNIANI kila MWAKA.

Kuwepo kwa SUKARI nyingi katika DAMU ,husababisha UGONJWA wa KISUKARI ,ambao unamweka MTU katika HATARI ya kupata UGONJWA wa MOYO au KUPOOZA/KIHARUSI (stroke) mara MBILI zaidi ya ASIYE na KISUKARI .

Kumbuka UGONJWA wa MOYO huweza kumpata MTU yeyote bila kujali UMRI ,na katika siku za karibuni mtindo wa MAISHA umewafanya WATU wengi kupata MARADHI haya kutokana na ULAJI holela wa MLO usiozingatia AFYA na kuacha kufanya MAZOEZI .

Monday, June 26, 2017

TATIZO LA UVIMBE KWENYE KIZAZI KWA WANAWAKE NA TIBA YAKE

TATIZO LA UVIMBE  KWENYE KIZAZI (FIBROID) NA TIBA YAKE !!

Siku hizi kuna ongezeko kubwa sana la huu ugonjwa hebu tega sikio.
Fibroid ni uvimbe ambao hutokea kwenye tumbo la kizazi ambao huu uvimbe unaweza kuwa ndani ya kizazi(ukutani mwa kizazi) au ndani ya nyama ya kizazi na nje kwenye ukuta wa kizazi.

Kuna aina kuuzifuatazo za fibroids:

1.Submucosal fibroids(ndani ya kizazi)
2.intramural fibroid(ndani ya nyama za kizazi)
3. Subserosal(nje ya kizaz)

Watu wafuatao wako hatarini ya kupata ugonjwa huu fibroids

1.Mwanamke ambae hajawahi kupata mtoto mpaka umri mkubwa
2.miaka kuanzia kubarehe mpaka hedhi kukoma
3.kurithi 4.unene 5.kuingia hedhi mapema

Fibroids sio kansa ni uvimbe wa kawaida tu ambao unakua kwa kutegemea kichocheo cha estrogen hormone ndio maana kuanzia kubarehe mpaka kukoma kwa hedhi ndio wako hatarini. Na mara nyingi uvimbe huu waga unaongezeka kukua sana hasa wakati wa ujauzito kwani vichocheo hivi huongezeka wakati huu kulinda makazi ya mtoto.
Ni watu waliofikia kikomo cha hedhi hawapati fibroids au kitaalam leomyoma.

Dalili za fibroids

1.Kutokwa damu kwenye via vya uzazi katikati ya mwezi.
2.kutokwa na uchafu wenye kiaharufu mbaya au ambao hauna harufu lkn mwingi na mweupe.
3.maumivi ya kiuno hasa wakati wa hedthi ambayo husababishwa na kizazi kujaribu kusukuma huo uvimbe..wengi hupata maumivu makali sana.
4.Tumbo kuuma sana chini ya kitovu.
5.hedhi zisizokuwa na mpango
6.maumivu wakati wa tendo la ndoa
7.Kukosa hamu ya tendo la ndoa
8.maumivu makali wakati wa hedhi

Uvimbe unapokua mkubwa unaweza kusababisha dalili zifuatazo.

1.Kukojoa mara kwa mara kwani uvimbe unakandamiza kibofu cha mkojo
2.Mkojo kubaki kwenye kibofu cha mkojo
3.Haja kuwa ngumu
4.miguu kuvimba
5.kupungukiwa damu

Jinsi fibroids zinavyoweza kuzuia kupata mtoto:

1.Fibriods zikikua sana zinakandamiza mishipa ya kupitisha mayai kutoka kwenye kiwanda yan ovari
2.Uvimbe pia unazuia yai lililorutubishwa kujishikiza kwenye kizazi..hasa submucosal fibroids
3.Pia husuia mfuko wa kizazi kukaza kusukuma mbegu kwenda kwenye mishipa ya kupitisha mayai.

MATIBABU

1.Wanawake wengi wanafibroids ndogo ndogo lakini kwa sababu hazina dalili hahawezi kwenda hospitali na hawa ndo sku wakibeba ujauzito uvimbe unaongexeka coz ya vichocheo kuongezeka hvyo hawa watu tunawabaini tunapofanya ultrasoudi ndipo wanakutwa navyo.lkn kitaamu hospitali hawatibu uvimbe wa namna hii

2.Uvimbe ambao ni mkubwa wenyewe hutibiwa kwa namna zifuatazo (hospital)

A.Dawa ambazo ni gharama sana mfano donazol wengi masikini hawawez kumudu kununua
B.Vidonge vya maumivu

C.Vidonge vya kuzuia damu km tranexamic acid na dawa za uzazi wa mpango(COCs)

2.Njia ya pili ni operation nazo zipo operation aina nyingi inategemea na uvimbe ukubwa na wingi wake.
1.Myomectomy hii ni operation ya kuondoa uvimbe mmoja mmoja bila kuondoa kizazi kwa wale wenye uvimbe mmoja uko sehemu nzuri
2.Total abdominal hysterectomy. Hii operation unaondoa kizazi chote kama uvimbe umekaa vibaya na viko vingi.
Swali la kujiuliza kwa nini mpaka upate dalili ndo utaanza kushughulikiwa kutibiwa???? Kwa nini ubebe ujauzito huku una uvimbe kisa bado mdogo???
Kumbuka uvimbe huu sio kansa hvyo ondoa hofu. Mbali na donazole ambayo ni ya gharama na haishauliwi itumiwe kwa mda mrefu ina sababisha mwanamke anakua na sifa za kiume.UKIFANYIWA OPERATION USIDHANI UVIMBE UMEISHA UNAOTA PEMBENI HADI UTAKAPOWEKA VICHOCHEO SAWA.

**AFYA NDIO KILA KITU**

Sunday, June 25, 2017

UFAHAMU UGONJWA WA FIGO (SABABU NA JINSI YA KUJIKINGA)

HABARI ZENU WADAU WA MAKALA ZANGU..?

LEO nimeona ni VYEMA nikushirikishe kuhusu CHANGAMOTO ya UGONJWA wa FIGO.

FIGO ni OGANI inayoshirikiana na MOYO. KUATHIRIKA kwake kuna ATHARI KUBWA kwa MFUMO wa DAMU na MAPIGO ya MOYO.

MAGONJWA SUGU ya FIGO hutokea pale OGANI hiyo inapopoteza UWEZO wa kutenda KAZI zake kikamilifu.

TATIZO huanza TARATIBU na KUDUMU kwa MUDA mrefu hadi kuonyesha DALILI za WAZI .
HUU ni kati ya MAGONJWA yasiyoambukiza kwani UNATOKANA na MIENENDO na MITINDO ya KIMAISHA .

FIGO huwa na KAZI ya kuchuja TAKAMWILI zilizo NDANI MWILINI na kuzitoa NJE kwa NJIA ya MKOJO na KUPUNGUZA kiasi cha MAJI kilichozidi MWILINI.

FIGO hutoa HOMONI inayochochea OGANI zingine MWILINI ikiwamo KUHAMASISHA utengenezwaji wa CHEMBE NYEKUNDU za DAMU,utendaji wa MADINI ya KALSIAMU na HOMONI zinazoongeza MWENDO KASI wa MISULI ya MOYO.

Vilevile ,FIGO hufanya KAZI ya KUFYONZA na KUVIRUDISHA vitu MUHIMU ambavyo vingehitajika kutoka kwa NJIA ya MKOJO.

Hudhibiti MADINI kama POTASIUMU,MAGNESIUMU,na TINDIKALI ili kuweka sawa MAZINGIRA sawia katika DAMU.

FIGO inapopoteza UWEZO wake wa kutenda KAZI husababisha KUKOSEKANA kwa UFANISI wa SHUGHULI za MWILI.
HALI hii husababisha KUWAPO kwa KUSANYIKO na LIMBIKIZO la MAJI,UCHAFU na SUMU hutokea MWILINI mwa MGONJWA.

Pia husababisha KUTOKEA kwa MARADHI mengine kama vile, UPUNGUFU wa DAMU MWILINI, SHINIKIZO la DAMU na ONGEZEKO la TINDIKALI kwenye DAMU.

Vilevile husababisha ONGEZEKO la LEHEMU na MAFUTA kwenye DAMU na MAGONJWA ya MIFUPA.

INAELEZWA kuwa karibu WATU nusu MILIONI wapo katika UCHUJAJI DAMU na MASHINE MBADALA wa FIGO ( dialysis ) na huku WAKIWA wameshawahi kubadilishiwa FIGO.

MAMBO kadhaa YANAHUSISHWA na TATIZO la UGONJWA SUGU wa FIGO ikiwamo UGONJWA wa KISUKARI, SHINIKIZO LA DAMU,UNENE ULIOPITILIZA na UZEE.

Vilevile MABADILIKO katika TABIA na namna WATU wanavyohishi.

Ili KUJIEPUSHA na HATARI ya kupata UGONJWA wa FIGO fanya yafuatayo.

1.USICHELEWE kwenda HAJA.

Kutunza MKOJO kweye KIBOFU chako  kwa muda MREFU ni WAZO BAYA.KIBOFU kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu.  
MKOJO ambao unakaa kwenye KIBOFU  huzidisha BAKTERIA haraka.
Pia MKOJO unaporudi NYUMA ya NJIA husababisha  MAAMBUKIZI katika FIGO pia NJIA ya mkojo "nephritis", pamoja na "uremia".
Wakati WITO ASILI (unahisi mkojo) fanya haraka iwezekanavyo nenda KAKOJOE .

2.Kula CHUMVI kupita kiasi nalo ni TATIZO.

Inatupasa kula Chumvi isiyozidi 5.8 gramu kwa SIKU .

3.Kula NYAMA kupita kiasi.

PROTINI ikizidi sana katika MLO wako inadhuru FIGO zako. MMENG'ENYO wa PROTINI unazalisha AMONIA-  SUMU DUTU ambayo ina UHARIBIFU mkubwa kwa FIGO zako. NYAMA nyingi  inaleta UHARIBIFU zaidi wa FIGO.

4.UNYWAJI mwingi wa "CAFFEINES".

CAFFEINE hutokana na VINYWAJI vya SODA na VINYWAJI vingine LAINI kama KAHAWA, RED BULL n.k.                              Hupandisha SHINIKIZO la DAMU na FIGO zako kuanza kupata MATESO .
Unapaswa KUPUNGUZA kiwango  cha COKE, PEPSI, RED BULL, nk. ambavyo HUNYWA kila SIKU.

5.PIA Kutokunywa MAJI.

FIGO zetu LAZIMA zichakatwe VIZURI kutekeleza MAJUKUMU yake VIZURI .                       

Endapo HATUNYWI MAJI ya KUTOSHA , SUMU DUTU inaweza kuanza KUKUSANYIKA katika DAMU , kama hakuna KIMIMINIKA cha  KUTOSHA kutoa kwa NJIA ya FIGO .                        KUNYWA zaidi ya BILAURI 10 za MAJI kila SIKU.

Kuna NJIA RAHISI ya KUANGALIA kama  unakunywa MAJI ya KUTOSHA nayo ni kuangalia RANGI ya MKOJO wako,WEPESI wa RANGI ndiyo VIZURI.

6.PIA Kuchelewa MATIBABU .


Pia EPUKA VIDONGE hivi ni HATARI sana:-

D- baridi.
Vicks Action- 500
Actified
Coldarin
Cosome
Nice
Nimulid
Cetrizet- D

Hivi VIDONGE vina Phenyl propanol- amide PPA ambayo husababisha STROKE na zimepigwa MARUFUKU huko MAREKANI.

NAMALIZIA kwa KUKUPATIA MAONYO MUHIMU ya AFYA

1. JIBU (pokea) SIMU WITO na SIKIO  la KUSHOTO.
2. Usinywe  DAWA kwa MAJI BARIDI.
3. Usile MILO MIZITO baada ya SAA KUMI na MOJA JIONI .
4. Kunywa MAJI VUGUVUGU mengi ASUBUHI na kiasi USIKU . Usinywe MAJI BARIDI KAMWE .
5. MUDA BORA wa KULALA ni kutoka SAA NNE usiku hadi SAA KUMI alfajiri.
6. USILALE mapema BAADA ya KUMEZA DAWA au BAADA ya MLO wa USIKU, Kula CHAKULA laini.
7. Usipokee SIMU yako ikiwa HAINA CHAJI kwani WAKATI huo MIONZI huwa ina NGUVU mara 1000 .

Saturday, June 24, 2017

TATIZO LA KUNUKA MDOMO NA JINSI YA KUJILINDA

TATIZO KA KUNUKA MDOMO

Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla.
Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni hupunguza mtu kuwa lovable kwani hata unapoongea wengi watakwepa kuongea direct na wewe kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka mdomoni.
Kile unakula kina affect hewa unayotoa iwe mdomoni au sehemu nyingine. Na baadhi ya vyakula vina matokeo mabaya sana kwa hurufu unayotoa mdomoni.

Harufu mbaya mdomoni si ugonjwa wa kuambukiza haina haja kuogopa ukikutana na mtu mwenye harufu mbaya mdomoni kwamba atakuambukiza.

Pia tatizo kubwa ni kwamba watu wenye harufu mbaya mdomoni hawajijui kwamba wana harufu mbaya.
Asilimia 85 – 90% ya tatizo la harufu mbaya mdomoni asili yake ni kinywa chenyewe. Pia kiwango cha harufu hutofautiana kutokana na muda (mchana, usiku na asubuhi).
Harufu nyingi mbaya mdomoni hutokana na vyakula vyenye asilia ya protein.
Kuna zaidi ya aina 600 ya bacteria wanaoishi kwenye kinywa cha Binadamu (sehemu ya juu ya ulimi, fizi na kuzunguka meno).

NINI HUSABABISHA KUWA NA HARUFU MBAYA MDOMONI

Kutokuwa makini na usafi wa kinywa kama vile kupiga mswaki vizuri kunakoacha mabaki ya chakula ambayo huoza na kusababisha harufu mbaya mdomoni.
(Wengi hupiga mswaki haraka haraka na kuacha mabaki ya chakula)
Maambukizi ya magonjwa kama vile fizi kutoka damu, mfumo wa upumuaji na kisukari.
Kinywa kuwa kikavu kutokana na medications
Kuvuta sigara, kunywa kahawa

JINSI YA KUTAMBUA KWAMBA UNA HARUFU MBAYA MDOMONI

Wanasayansi wamekiri kwamba ni ngumu sana mtu kujijua mwenyewe kama ana harufu mbaya kwa sababu ya mazoea (habituation).
Ni rahisi sana kutambua harufu kutoka kwenye kinywa cha mtu mwingine.
Unaweza kutambua kama una harufu mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu unayemuamini.
Pia unaweza kujua harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa, wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa.
Pia unaweza kutumia kijiti cha kuchokonolea meno na kukinusa.
Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama Halimeter, Gas Chromatography na BANA Test.

JINSI YA KUJILINDA NA HARUFU MBAYA MDOMONI (TIBA)

Kula vyakula vyenye afya na pia kula vyakula ambavyo wakati unakula vinaweza kusafisha kinywa vizuri.
Kusafisha meno mara mbili kwa siku asubuhi na baada ya mlo wa usiku, unashauriwa kutumia tongue cleaner kusafisha ulimi.
Tumia chewing gum ambazo husaidia kuongeza kiasi cha mate kwenye kimywa kilichokauka. Baadhi ya gums zina viungo vinavyoondoa harufu mbaya mdomoni na zingine husafisha kinywa na bacteria wanaosababisha harufu mbaya.
Tumia dawa ya kusukutua mdomoni (mouthwash) kabla ya kulala usiku.
Kuwa makini na afya ya kichwa chako kama vile kupiga mswaki vizuri, kuondoa mabaki ya vyakula kwenye meno na kumuona daktari kila unapoona una Matatizo ya meno au kinywa.
Kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku angalau glass mbili za maji.
Mwone daktari wako ukiona una tatizo la harufu mbaya mdomoni.

Tuesday, June 20, 2017

UJUE UGONJWA WA KISUKARI NA JINSI YA KUJIKINGA

UJUE UGONJWA WA KISUKARI (Diabetes)
Kisukari ni ugonjwa unaotokana na mtu kuwa na sukari nyingi kupita kiasi kwenye damu. Ugonjwa huo huvuruga utaratibu wa kuingiza sukari ndani ya chembe kutoka kwenye damu kwa kuwa chembe huhitaji sukari ili kupata nishati.
Ugonjwa wa Kisukari hutokea pale ambapo tezi ya kongosho inaposhindwa kutengeneza kichocheo (Homoni) aina ya insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka kwa sukari (Hyperglycemia) au kushuka kwa kiwango cha sukari (Hypoglycemia). Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababishwa na kuwa na kiwango kidogo cha insulin mwilini, mwili kutosikia kichocheo hicho au yote mawili

KISUKARI NI NINI HASWA?
Sukari mwilini hutokana na vyakula pamoja na vinywaji tunavyotumia kila siku na hutumika kuupa mwili nguvu. Glukosi ni aina ya sukari ambayo huzipa chembe za mwili nishati. Hata hivyo ili glukosi iingie ndani ya chembe hizo inahitaji insulini. Insulini ni kemikali (Homoni) ambayo hutokezwa na kongosho (Pancrease).

NINI CHANZO HASA CHA KISUKARI?

Ili kuelewa vyema ugonjwa wa kisukari ni muhimu kwanza kuelewa namna chakula kinavyovunjwa vunjwa na kutumiwa na mwili ili kuzalisha nguvu. Wakati chakula kinapoyeyushwa matukio kadhaa hutokea. Moja ni sukari inayoitwa glucosi ambayo ni chanzo cha nishati/nguvu mwilini huingia katika damu. Tukio la pili ni kiungo kinachoitwa kongosho (Pancrease) kutengeneza kichocheo cha insulini. Kazi ya insulini ni kuondoa glucosi katika damu na kuingiza katika misuli, seli za mafuta na ini, ambako hutumika kama nishati.
Watu wenye kisukari huwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu kuliko inavyotakiwa kwa sababu miili yao haiwezi kupeleka sukari kwenye seli za mafuta, ini na misuli ili ihifadhiwe kwa ajili ya kuzalisha nguvu. Hii ni kutokana na moja ya sababu zifuatazo, huenda kongosho zao haziwezi kutengeneza insulini ya kutosha au seli za mwili wao haziathiriwi na insini kama inavyotakiwa au sababu zote hizo mbili.
DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
Kama wewe ni mnene kupita kiasi, hufanyi mazoezi kwa ukawaida au una watu wa ukoo walio na kisukari, huenda tayari una kiwango cha juu cha sukari kwenye damu. Ongezeko la sukari kwenye damu mbali na kuwa kisababishi cha kisukari, hali hiyo inahusianishwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa akili uitwao 'DEMENTIA'.

Kula sukari nyingi sio sababu ya ugonjwa wa kisukari. Lakini lazima tuseme kwamba kula sukari nyingi si nzuri kwa afya yako kwani utaongeza uzito wa kuweza kuathiri uwezo wa mwili wako kujikinga na maradhi tofauti. Ugonjwa wa kisukari umeitwa kwa kufaa "ugonjwa unaoathiri kiini cha nishati ya mwili". Mwili unaposhindwa kutumia glukosi, mifumo mbalimbali ya mwili inaweza kuacha kufanya kazi au hata kusababisha kifo
Ugonjwa wa Kisukari kitaalamu hujulikana kama 'DIABETES MELLITUS'. Jina 'Diabetes Mellitus' linatokana na neno la Kigiriki linalomaanisha 'kunyonya' na neno la Kilatini linalomaanisha 'tamu kama asali'. Maneno hayo yanafafanua vizuri sana ugonjwa huo, kwani maji hupita mwilini mwa mtu aliye na ugonjwa wa kisukari kana kwamba yananyonywa na mdomo na kupitia kwenye njia ya mkojo kisha kutoka nje ya mwili. Isitoshe mkojo huwa na ladha tamu kwa kuwa una sukari.
Nyingine ni ngozi kuwa kavu na kuwasha, mgonjwa kupoteza uzito bila sababu, kuwa na ukungu machoni, kuchoka kusiko kwa kawaida, hisia kupungua katika vidole na viganja
mikononi na miguuni na kuwa na ukungu katika fizi, ngozi na kibofu cha mkojo.
NI NANI ANAWEZA KUWA NA UGONJWA WA KISUKARI?
Watu walio katika makundi yafuatayo wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kisukari:
 Wenye uzito uliozidi
 Wenye historia ya kuwa na wagonjwa wa kisukari katika familia zao,
  Wanawake waliozaa watoto wenye kilo 4 au zaidi,
 Watu wasiojishughirisha au wasiofanya mazoezi,
  Wenye shinikizo la damu,
  Wenye msongo wa mawazo na
  Wenye matumizi makubwa ya pombe na sigara
 Watu hawa wanashauriwa kupima sukari yao kila mwaka wakiwa na umri wa miaka 45 na kuendelea.
Kuna hatari kubwa ya kuugua ugonjwa huo ikiwa mtu ana mafuta mengi katika tumbo na kiuno chake kuliko katika mapaja yake. Mafuta katika kongosho na ini huvuruga uwezo wa mwili wa kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu.
Wavutaji wa sigara wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi kwani zoea hilo hudhuru moyo na mfumo wa mzunguko wa damu na kubana mishipa ya damu. Kitabu kimoja kinasema kwamba asilimia 95 ya watu wanaougua kisukari ambao hulazimika kukatwa viungo ni wavutaji wa sigara.

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
  Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati
  Kwenda haja ndogo mara kwa mara. Watoto kukojoa kitandani
  Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati.
  Kupungua uzito au kukonda licha ya kula vizuri.
  Kusikia njaa kila wakati na kula sana.
  Wanawake kuwashwa ukeni.
  Kutoona vizuri.
  Kupungua nguvu za kiume au hamu ya kujamiiana kwa wanawake.
  Ganzi, kuchomwachomwa au kutohisi unapoguswa sehemu za miguu, viganja na vidole
  Miguu kuoza na hata kupata gangrini.
  Kukaukwa na ngozi na pia kupata aina ya ganzi katika miguu.
  Vidonda au majeraha sehemu yoyote ya mwili kutopona haraka.
  Majipu mwilini.

Wenye dalili hizi wanashauriwa kupima sukari ili kubaini kama wana kisukari.
Watu wenye kisukari wanapaswa kubadili jinsi wanavyokula na kuishi.Ufuatao ni ushauri wa kuwasaidia kufanya mabadiliko:
• Anza na mabadiliko madogo madogo. Kwa mfano, badala ya kuacha utumiaji wa vinywaji vilivyokolezwa sukari mara moja, jaribu kupunguza matumizi ya vinywaji hivyo taratibu. Kupunguza taratibu kiasi cha sukari unayokula au kuongeza kiasi cha mazoezi ni rahisi kutekeleza na kuna uwezekano mkubwa utazoea na kuendelea na utaratibu huo.
• Amua mwenyewe unataka kubadili nini. Weka lengo kama vile kutembea zaidi, kupunguza uvutaji au kutovuta kabisa, au kuweza kucheza na wajukuu zako.
• Tafuta msaada. Familia, marafiki, au watu wengine wenye kisukari wanaweza kukusaidia kufanya mabadiliko.
• Tafuta msaada kwa matatizo ya kisaikolojia. Ni jambo la kawaida kwa watu wenye kisukari kuogopa maisha ya baadaye, kuhuzunika juu ya kuugua mara kwa mara, au kuwa na hasira juu ya mabadiliko yanayohitajika. Hisia za uchungu, huzuni, au kukosa matumaini vinaweza kumzuia mtu mwenye kisukari kufanya mabadiliko ambayo yanahitajika au ambayo anataka kufanya.
• Tafuta sababu zako za kutaka kuwa na afya bora zaidi. Unataka kufanya nini na unataka kujisikia vizuri namna gani? Kwa mfano, fikiria familia yako na kwa nini unataka kuendelea kuishi ukiwa mwenye afya ya kukuwezesha kuwasaidia wanafamilia kwa muda mrefu zaidi.
• Ugonjwa wa kisukari ni tatizo ambalo siku hizi husababishwa na mfumo wa maisha tunayoishi hasa vijana, tafiti zilizowahi kufanywa zinaonesha kuwa vijana wapo kwenye hatari kubwa ya kupata kisukari kwa sababu ya mfumo usio sahihi wa maisha wanayoishi vijana.
• Kutokufanya mazoezi, kukosa muda wa kupumzika na kutokula mlo sahihi,unywaji wa pombe na uvutaji sigara wa kupitiliza, hizi ni sababu chache zinazochangia vijana kuishi katika mfumo wa maisha hatarishi wa kupata maradhi ya kisukari.
Baadhi ya dawa za mitishamba zinaweza kusaidia kucontrol sukari mwilini
Waulize wataalam wa tiba za asili dawa gani za mitishamba zinapatikana katika eneo lako kwa ajili ya kupunguza sukari kwenye damu na kuwa kawaida, njia bora zaidi za kuzitumia, na kama ni salama kuzitumia sambamba na insulini na dawa zingine.
Duniani kote, wataalam wa tiba za asili wamegundua vyakula na dawa za mitishamba ambazo zinaweza kusaidia kupunguza sukari kwenye damu. Ifuatayo ni mifano kadhaa:
• Bitter melon , Mdalasin, Binzari ya manjano, Majani ya mlonge, Uwatu (Fenugreek), Forosadi (Mulberry) , Tangawizi , Nopal (cactus, Bitter leaf , Siki
SHARE UJUMBE HUU KWA NDGU NA MARAFIKI KWA MSAADA WA ELIMU JUU YA UGONJWA HUU

SARATANI YA TEZI DUME(VISABABISHI,DALILI PAMOJA NA JINSI YA KUIEPUKA)

HABARI ZENU WADAU WA MAKALA ZANGU..?

LEO NATAKA NIIZUNGUMZIE CHANGAMOTO YA SARATANI YA TEZI DUME.

SARATANI ya TEZI DUME inashika NAFASI YA TATU kwa kusababisha VIFO vinavyotokana na KANSA kwa WANAUME duniani.

UGONJWA huu ni chanzo kikuu cha VIFO vinavyosababishwa na SARATANI kwa WANAUME wenye UMRI wa kuanzia MIAKA 45 na kuendelea, hata hivyo, SARATANI ya TEZI DUME kwa sasa inawapata sana WANAUME kuanzia MIAKA 25.

Kwa ufahamisho tu ni kwamba NENO SARATANI ni JINA la UGONJWA ambalo hutokea wakati CHEMBE HAI au SELI katika sehemu fulani ya MWILI zinapoanza KUKUA bila kufuata UTARATIBU wa MFUMO WA MWILI na kutengeneza VIJIUVIMBE vidogo vidogo.
Kwa kawaida SELI huwa ZINAJIGAWA, KUPEVUKA na baadaye ZINAKUFA.

UTOKEAJI wa SARATANI ni pale ambapo SELI zilizotakiwa KUFA HAZIFI, zinaendelea KUISHI wakati HUOHUO zile MPYA zinazidi KUZALIWA.

UKWELI ni kwamba WANAUME wote WANAZALIWA na TEZI DUME lakini baada ya BALEHE, TEZI DUME huongezeka UKUBWA mara MBILI.
Na ikifika MIAKA 30 TEZI DUME huanza KUKUA haraka zaidi.Hii ni kwa sababu UKUAJI wa TEZI DUME huenda SAMBAMBA na UMRI.

Kuna VIHATARISHI vingi vinavyochangia MWANAUME kupata SARATANI ya TEZI dume.

Vifuatavyo ni baadhi yake:-

-UMRI. Nafasi ya kupata SARATANI ya TEZI DUME huongezeka sana hasa ukifikia UMRI wa karibu MIAKA 50 na kuendelea.

-NASABA ni kihatarishi kingine ambapo WANAUME wenye HISTORIA ya tatizo hili kwenye FAMILIA ZAO,wale ambao MMOJA WA NDUGU ZAO wamewahi kuugua UGONJWA huu, huwa katika HATARI ya kupata SARATANI hiyo kutokana na KURITHI JENI za UGONJWA huo.

-SUALA jingine ni LISHE ambapo WANAUME wanaopenda KULA NYAMA(red meat) na WALAJI wa CHAKULA chenye kiasi KIKUBWA cha MAFUTA hasa ya WANYAMA, huwa katika HATARI KUBWA ya kupata SARATANI ya TEZI DUME.

-Pia WATAALAM wanatumbia kuwa,WANAUME wasiopenda kufanya MAZOEZI,WANENE na WENYE UPUNGUFU wa VIRUTUBISHO vya VITAMIN E pia wako kwenye HATARI ZAIDI ya kupata SARATANI ya KIBOFU cha MKOJO.

-WANAUME wengine walio katika HATARI KUBWA ya kupata SARATANI ya TEZI DUME ni pamoja na wale wenye ASILI ya AFRIKA(Weusi), ikilinganishwa na WAZUNGU.

-WAKULIMA wanaotumia aina fulani ya MBOLEA za KEMIKALI, wanaofanya KAZI katika VIWANDA vya kutengeneza MATAIRI na WACHIMBAJI MADINI, hususani aina ya cadmium

DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME

Katika HATUA zake za AWALI, dalili za saratani ya TEZI DUME hazitofautiani na zile za KUVIMBA kwa TEZI DUME au BPH. Dalili hizo ni pamoja na:-

1.Kupata SHIDA wakati wa kuanza KUKOJOA.

2.Kutiririka kwa MKOJO baada ya KUMALIZA kukojoa.

3.Kukojoa MKOJO wenye mtiririko DHAIFU.

4.Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za USIKU.

5.KUJIKAKAMUA wakati wa kukojoa na KUSHINDWA kumaliza MKOJO wote.

6.Kutoa MKOJO uliochanganyika na DAMU.

KITAALAM imethibitika kuwa endapo MWANAUME HUYU hasa mwenye MIAKA kuanzia 30 atapata VIRUTUBISHO maalum vya VITAMINI na MADINI anaweza KUEPUKA CHANGAMOTO HII.

WANAUME waliopo HATARINI zaidi ni kuanzia MIAKA 45 na kuendelea. Kwani katika kila WANAUME 6 inakadiriwa kuwa MMOJA atakuwa na SARATANI HII.

Featured Post

FAIZA ZA KULA PAPAI

 _*Siri usioijua kuhusu utajiri wa tunda la papai katika kukulinda na magonjwa hatarishi kutokana na faida zake lukuki*_  Hizi ndizo FAIDA 1...